• ePaper
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DK. SAMIA AMREJESHA MAKONDA AFCON

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 18, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
DK. SAMIA AMREJESHA MAKONDA AFCON
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan, amempa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, maagizo matatu kuhusu Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), 2027, ambayo anapaswa kujifunza Morocco.

Miongoni mwa maagizo hayo ni kujifunza mbinu walizotumia Morocco katika mashindano ya AFCON mwaka huu, kuhakikisha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatinga fainali ya mashindano hayo mwakani.

Mambo mengine aliyoagizwa Makonda, ni kupeleka barua yenye ujumbe kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF), Patrice Motsepe na kuhakikisha Tanzania inakuwa namba moja katika kukuza utalii kupitia michuano hiyo.

Makonda aliyataja mambo hayo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), alipokuwa akielekea nchini Morocco.

AFCON 2027 itafanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

 “Tumepata heshima ya kutumwa na Rais Dk. Samia kwenda nchini Morocco kupokea na kutimiza ndoto ya wapenzi wa mpira wa miguu siyo tu Afrika bali duniani, kijiti cha maandalizi ya AFCON 2027.

“Kwa utamaduni uliopo, nchi inayoandaa mashindano yanayofuata baada ya kuhitimisha mashindano yaliopo, hupewa nafasi ya kukabidhiwa na kuanza maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.

Rais Dk.Samia amedhamiria kwa dhati na kwa nguvu zake zote kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika michezo yote duniani,” alisema Makonda.

Waziri Makonda alisema Rais Dk. Samia amewaelekeza yeye, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerson Msigwa na ujumbe waliombatana nao kwenda nchini Morocco kufanya mambo hayo matatu.

“Jambo la kwanza, ametupatia barua mahususi ya kumpelekea Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF), Patrice Motsepe yenye ujumbe mzito kutokana na kazi nzuri ambayo shirikisho hilo lilitambua kazi alioifanya Rais Dk. Samia ya kuwekeza katika michezo na kufikia hatua ya kumpa tuzo kama raisi bora aliyefanya kazi nzuri ya kuinua michezo ndani ya Tanzania kwa fedha nyingi za hamasa lakini, pia kwa kujenga miundombinu.

“Pili, Rais Dk. Samia ametutuma kwakuwa Morocco tulicheza nayo na Taifa Stars ikaleta ushindani wa hali ya juu, tukatazame na kujifunza mbinu zote walizonazo kuhakikisha Tanzania 2027,  kama siyo kucheza fainali basi kombe linabaki nyumbani,”alisema Makonda.

Alisema kutokana na maelekezo hayo, waliambatana na wataalamu mbalimbali, ambao wengine tayari wapo nchini Morocco kujifunza mambo mbalimbali.

Aliongeza, wao wanakwenda  kuendelea kuona mbinu walizotumia Morocco kuifanya timu yao kuendelea kushika hatamu na kutinga fainali ili Taifa Stars iendelee kuvunja rekodi kama ilivyokuwa kawaida yake.

“Jambo la tatu ambalo Rais Dk. Samia ametutuma; ni kwamba kwa kuwa Morocco hivi sasa ndiyo nchi inaongoza kwa utalii kupitia michezo kwa kushika namba moja hivyo, ametaka Tanzania ishike namba moja kwa kuwa ina fursa nyingi kuliko nchi yeyote Afrika hivyo kutakuwa na watu maalumu kwa ajili ya kuangalia hoteli, usafiri, vyakula, utalii kuhakikisha AFCON 2027 inaacha historia njema kwa watanzania kwa kuimarisha uchumi wao,” alisema Makonda.

Makonda alisema ni ndoto ya Rais Dk. Samia kwa kila Mtanzania aliyopo ndani na nje ya nchi, ambaye anayo fursa ya kusaidia na kusapoti mashindano hayo milango ipo wazi kwa wizara ya michezo.

MAANDALIZI

Alisema maandalizi ya AFCON 2027 yataanza tarehe 19, mwaka huu, baada ya kukabidhiwa kijiti Januari 18 katika fainali ya michuano hiyo kati ya Morocco na Senegal.

“Katika maandalizi haya tutakuwa na mashindano ya wasanii kutunga wimbo bora utakaotumika katika mashindano hayo, vikundi mbalimbali na ngoma zitakazoshindana kwa ajili ya mashindano haya,”alisema Makonda.

Katika AFCON 2025, Taifa Stars iliishia hatua ya 16 bora, baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya mwenyeji Morocco.

Previous Post

WATOTO HAWASTAHILI KUCHOMWA VIGANJA KWA KUDOKOA NYAMA

Next Post

TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

Next Post
TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AVUTIA MAELFU KILA KONA

DK. SAMIA AVUTIA MAELFU KILA KONA

6 months ago
DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

6 months ago

Popular News

  • MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    MAAJABU YA DP WORLD SIKU 730 BANDARINI DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘MISS WORLD’ KUIPAISHA TANZANIA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL. 195.66/- KUJENGA BONDE MTO MSIMBAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULEGA AJIBU MAPIGO KUHUSU MTANDAO WA BARABARA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?