• ePaper
Thursday, April 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 23, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na HANIFA RAMADHANI, Zanzibar

TIMU za soka za Simba na Mafunzo zinatarajiwa kupambana leo katika michuano ya Kombe la Muungano  utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Mchezo huo, tayari umevuta  hisia za mashabiki wengi wa soka, umepangwa kuanza majira ya saa 1:15 usiku.

Wakizungumza jana, Amani mjini Unguja, makocha wa timu hizo wamesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

Kocha wa timu ya Simba, Steve Barker alisema, wamekuja Zanzibar katika michuano hiyo kwa malengo makuu matatu, ikiwemo kushinda ubingwa wa mashindano hayo.

Alisema lengo  la pili ni kutoa fursa kwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mengine.

Pia, alisema lengo la tatu ni  kujijenga upya kiakili kabla ya kuendelea na ratiba ngumu ya ligi kuu.

Kwa upande wake, Kocha wa timu ya Mafunzo, Haji Ramadhan Mwambe alisema Simba ni timu kubwa lakini na wao wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

“Tunajua kwamba tunakutana na timu kubwa yenye wachezaji wakubwa,lakini sisi mafunzo tumejiandaa vizuri kushinda,” alisema.

Alieleza kuwa, timu yake ina wachezaji wazuri na vijana ambao wapo tayari kucheza na Simba.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Shomari Kapombe alisema wamejiandaa vizuri na mchezo huo na kwamba wamekuja Zanzibar kushindana.

Alisema, malengo siyo kushiriki tu bali ni kushinda taji hilo la Kombe la Muungano kwa mwaka huu.

Previous Post

MABEKI YANGA SC, AZAM FC KIBOKO

Next Post

MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

Next Post
MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA AHIMIZA KILA MMOJA KUPIGA KURA

WASIRA AHIMIZA KILA MMOJA KUPIGA KURA

6 months ago
KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

7 days ago

Popular News

  • NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATOA MAAGIZO ALAT

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIPOTI YA KUPONYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?