• ePaper
Tuesday, May 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewaonya wanachama walioanza harakati za kusaka urais mwaka 2030 kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujawadia, hivyo wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, miongozo na utaratibu.

Amesema kuanza mapema harakati za kusaka uongozi kabla ya wakati inaweza kukigawa Chama badala ya kukijenga hivyo inapaswa kukemewa.

Wasira ameeleza hayo leo Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za CCM Wilaya ya Bunda ambazo zilichomwa moto katika na vurugu za Oktoba 29, 2025.

Amesema ndani ya Chama kuna kundi la wanachama ambao hawana kazi za msingi ndani ya CCM zaidi ya kujihusisha na makundi ya kisiasa.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti Wasira, kundi hilo limeanza kujipanga kwa kuunda safu kuanzia ngazi za kata, hali ambayo inaweza kusababisha mgawanyiko ndani ya CCM kwa kuwa kila mmoja anataka kuwa na wafuasi wake badala ya kuimarisha umoja.

Wasira alihoji uhalali wa baadhi ya watu kuanza kujitangaza mapema kuwania urais wa 2030, akisema hakuna anayeweza kujihakikishia uwepo wake hadi wakati huo.

“Unazungumziaje urais wa 2030 leo, wakati hata hujui kama utakuwepo? Hiyo ni kama kumjaribu Mungu.

Wakati huu tunapaswa kujikita kwenye kazi za kujenga Chama na nchi,” amesisitiza.
Aidha, ameonya tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha kushawishi wanachama maskini kuungwa mkono, akieleza kuwa hali hiyo ni hatari na inaweza kuharibu maadili ya Chama.

Previous Post

LUKUVI KUAGWA MIKOA MITATU

Next Post

TANZANIA TUNA RAIS JASIRI NA MCHAPAKAZI

Next Post
TANZANIA TUNA RAIS JASIRI NA MCHAPAKAZI

TANZANIA TUNA RAIS JASIRI NA MCHAPAKAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KWAHERI WILLIAM LUKUVI

KWAHERI WILLIAM LUKUVI

2 months ago
TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

9 months ago

Popular News

  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAKONDA ASISITIZA KULINDWA KWA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AHIMIZA MALEZI YA KIMAADILI NA USHIRIKIANO WA KIJAMII

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWA MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?