• ePaper
Sunday, September 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WALIOTELEKEZA NIDA KUBANWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 17, 2026
in Habari
0
WALIOTELEKEZA NIDA KUBANWA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ameitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kutafuta utaratibu wa kisheria kuwawajibisha wananchi wanaoacha kuchukua vitambulisho vyao vilivyokamilika.

Amesema tabia hiyo, inasababisha serikali kupata gharama zisizo za lazima na kuathiri wananchi wengine wanaohitaji huduma hiyo.

Dk. Mwigulu alisema hayo jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Utambulisho Duniani yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City.

Alisema kitambulisho kinapokuwa tayari, mwananchi anapaswa kukichukua, badala ya kusubiri hadi atakapokumbwa na jambo la dharura.

Waziri Mkuu, alisema NIDA imekuwa ikiwafahamisha wananchi kwa ujumbe mfupi wa simu kuwa, vitambulisho vyao vimekamilika, baadhi yao huviacha muda mrefu, baadaye huvifuatilia baada ya muda mrefu kupita.

“Tafuteni utaratibu wa kuwakumbusha ukiwa tayari tunauweka katika sheria… vitu vya muhimu vinabidi uvipe uzito.

“Unapewa kitambulisho tayari, umechukua nafasi ya wale ambao walihitaji zaidi, umekiacha tu mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu, inabidi tuangalie utaratibu, inaweza kuwa chanzo kingine cha mapato,” alisema.

Alisema serikali haiwezi kuendelea kutumia rasilimali kutengeneza vitambulisho ambavyo wananchi wamepewa taarifa kuwa, vipo tayari, wanashindwa kwenda kuvichukua, baadaye wanavihitaji wanapohitaji huduma za msingi.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mwananchi anayepuuza kuchukua kitambulisho chake, atakwama pindi atakapohitaji huduma au fursa inayohitaji utambulisho rasmi, kisha kuanza kuilaumu serikali.

Alisema hali hiyo inaweza kuepukika iwapo wananchi watachukua vitambulisho vyao kwa wakati na kuvitumia, huku NIDA ikiendelea kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wale ambao vitambulisho vyao vimekamilika.

Dk. Mwigulu, alisema umuhimu wa kitambulisho cha taifa, hauishii katika kuwa na kadi, bali utambulisho wa kisheria ni miundombinu muhimu ya kitaifa inayomwezesha mtu kutambulika kwa usahihi, kupata huduma na kushiriki katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Alisema serikali inalenga kuhakikisha taasisi zote zinazohusika na ajira, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi, zinaunganishwa katika mfumo wa NIDA kuimarisha uhakiki na usahihi wa taarifa.

“Taasisi zote nchini zinazojihusisha na ajira, utoaji wa huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi, ziunganishwe katika mifumo kuimarisha uhakiki na usahihi wa utambulisho kwa lengo la kuzuia udanganyifu na matumizi mabaya ya utambulisho na vitendo vya kihalifu,” alisema.

Alisema hivi sasa NIDA inaendelea na kazi ya kusafisha taarifa zake kutokana na kuwepo pengo kati ya wananchi wenye vitambulisho na wale ambao bado hawajawa navyo, hali ambayo imekuwa ikisababisha changamoto katika maeneo mbalimbali.

Alisema changamoto hizo, zimekuwa zikijitokeza katika maeneo ya ajira, uchaguzi na mikopo.

Dk. Mwigulu, alisema hali hiyo, itapungua baada ya Watanzania wote kuwekwa katika mfumo wa utambuzi.

Alisisitiza umuhimu wa wananchi ambao bado hawajasajiliwa kwenda kufanya hivyo, walio tayari wachukue vitambulisho vyao vilivyokamilika.

Aidha, aliitaka NIDA kuendelea kuimarisha usalama wa mifumo na miundombinu ya kubadilishana taarifa za utambulisho na kuongeza matumizi ya taarifa hizo katika taasisi za kifedha na nyingine muhimu.

WATOTO KUSAJILIWA NIDA

Dk. Mwigulu, alisema kuanza kwa usajili wa watoto, kutasaidia kuondoa pengo la utambulisho lililokuwepo kutokana na utaratibu wa awali uliolenga zaidi watu waliofikisha miaka 18, hivyo kuwezesha wananchi kutambulika rasmi mapema.

PONGEZI

Aliipongeza NIDA kwa kuadhimisha kwa mara ya kwanza Siku ya Utambulisho Duniani na kusema, serikali iko tayari kushirikiana na mamlaka hiyo katika kuhakikisha maadhimisho hayo, yanaendelea kufanyika kila mwaka, huku yakitumika kutoa elimu kuhusu umuhimu wa utambulisho wa taifa.

PATROBAS KATAMBI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alisema zaidi ya wananchi milioni mbili, tayari wamesajiliwa na vitambulisho vyao vipo, hawajavichukua.

Aliwataka wananchi hao, kujitokeza kuvichukua wanufaike na huduma zinazohitaji utambulisho.

Katambi, alisema matumizi ya NIDA katika maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba za kulala wageni, yatasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti uhalifu unaofanywa na watu wanaotumia mwanya wa kutotambulika.

Alisema baadhi ya wahalifu hutumia fursa ya kutotambulika kufanya vitendo vya uhalifu, akitoa mfano wa tukio la vijana saba waliofika hotelini, wakalipia vyumba na baadaye kufanya shughuli iliyowapeleka eneo hilo kabla ya kutoweka.

Alisema baada ya vijana hao kutoweka, ufuatiliaji wa tukio hilo ulikuwa mgumu na hata mlinzi wa hoteli alionekana alikuwa na  uhusiano na watu hao, hivyo utambulisho wa wageni kwa majina, sura na vitambulisho ungesaidia kuzuia au kurahisisha uchunguzi wa tukio hilo.

Waziri huyo, alisema changamoto ya watu kutotambulika haipo katika maeneo ya kulala wageni pekee, bali katika taasisi za kifedha na maeneo mengine, hivyo wananchi wavitumie kuongeza usalama na kurahisisha ufuatiliaji wa matukio ya uhalifu.

JAMES KAJI

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, aliwataka wananchi ambao vitambulisho vyao tayari vilishatengenezwa na wamejulishwa, wafike katika vituo husika kuvichukua.

Alisema kuna baadhi ya wananchi wanaacha kwa makusudi au baada ya kuhama maeneo walikojisajilia.

Previous Post

UBUNIFU MITEGO YA PANYA ULIVYOMUINUA KIUCHUMI KILONGOLA

Next Post

FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

Next Post
FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO

8 months ago
MAJIJI SITA MOROCCO KUIPAMBA AFCON

MAJIJI SITA MOROCCO KUIPAMBA AFCON

9 months ago

Popular News

  • NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KIFUA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?