• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 6, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA KATIKA MKUTANO WA IPU
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameyataka mabunge kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma na uwajibikaji wa serikali, akisisitiza kuwa wananchi wanatarajia wawakilishi wao kulinda maslahi yao na kuhakikisha mahitaji yao yanazingatiwa katika maamuzi.

Rais Dk. Samia ametoa ujumbe huo kupitia picha mjongeo iliyooneshwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), leo, Jumatatu, Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais Dkt. Samia katika ufunguzi rasmi wa mkutano huo unaofanyika Oktoba 5–9, 2026.

Amesema mamlaka ya mabunge yanatokana na wananchi, hivyo yana wajibu wa kutunga sheria kwa maslahi ya umma, kuchunguza mgawanyo na matumizi ya rasilimali na kuziwajibisha serikali. Ameeleza kuwa serikali yake inaheshimu jukumu la Bunge la kuisimamia na kuishauri, kwa kuwa linaimarisha utendaji na uwajibikaji kwa Watanzania.

Rais Dk. Samia amesema kaulimbiu ya mkutano kuhusu kuimarisha utawala bora na kuziwezesha jamii kupitia ushirikishwaji, kuaminiana na fursa kwa wote inaendana na changamoto za sasa duniani. Amehimiza mabunge kutathmini makubaliano yanayofikiwa na serikali na kuendeleza ushirikiano unaovuka tofauti za kisiasa na mipaka ya nchi.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu amesema mabunge yana nafasi muhimu katika kuhakikisha taasisi za umma zinaitikia mahitaji ya wananchi kupitia utungaji wa sheria, uidhinishaji wa matumizi ya fedha na usimamizi wa shughuli za serikali. Ametaja kuimarishwa kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyotengewa zaidi ya Sh. bilioni 132 katika mwaka wa fedha 2026/2027, kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma.

Dk. Mwigulu amesema Rais Dkt. Samia anaamini katika utawala wa kikatiba na mgawanyo wa madaraka, akisisitiza kuwa taasisi imara na huru ni muhimu katika kujenga jamii zenye ustawi, utulivu na ushirikishwaji.

Previous Post

SHAKA : DK. SAMIA AMEWAHESHIMISHA WANAWAKE AFRIKA

Next Post

NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI

Next Post
NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI

NDEJEMBI ATOA MSISITIZO TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI KODI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WADAU WAUNGA MKONO MSISITIZO WA RAIS DK. SAMIA KUHUSU MAADILI

WADAU WAUNGA MKONO MSISITIZO WA RAIS DK. SAMIA KUHUSU MAADILI

7 months ago
KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

5 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?