• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA MTIHANI KIDATO CHA NNE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 20, 2026
in Habari, Kitaifa
0
UJUMBE WA RAIS DK. SAMIA MTIHANI KIDATO CHA NNE
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka wenye dhamana ya kusimamia mtihani ya kidato cha nne kutekeleza majukumu yao kwa weledi, umakini, uadilifu na kuhakikisha mitihani inafanyika kwa haki, amani na usalama.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoituma kupitia ukurasa wake wa instagram, aliwatakia kila la kheri wanafunzi wa kidato cha nne wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya sekondari nchini.

Rais Samia, alisema ni imani yake kuwa, wanafunzi hao, wamejiandaa vyema kwa hatua hiyo muhimu katika safari yao ya kielimu.

“Ninamwomba Mwenyezi Mungu awajalie afya njema, utulivu na uwezo wa kufanya mitihani yenu kwa umakini na kujiamini.

“Aidha, ninatoa wito kwa wote wenye dhamana ya kusimamia mitihani hii kutekeleza majukumu yenu kwa weledi, umakini na uadilifu na kuhakikiasha mitihani inafanyika kwa haki, amani na usalama,” alisema Rais Samia.

Juzi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohamed alisema jumla ya watahiniwa 667,040 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu, wakiwemo watahiniwa wa shule 644,085 na watahiniwa wa kujitegemea 22,955.

Mtihani huo umeanza jana hadi Novemba 6, mwaka huu, katika shule za sekondari 6,265 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 802.

Profesa Said Mohamed, alisema kati ya watahiniwa 644,085 wa shule, wavulana ni 297,309 sawa na asilimia 46.16, huku wasichana wakiwa 346,776 sawa na asilimia 53.84.

Alisema watahiniwa wa shule wenye mahitaji maalum ni 910, wakiwemo wenye uoni hafifu 455, wasioona 13, wenye uziwi 98, wenye ulemavu wa akili 21 na wenye ulemavu wa viungo 323, ambao wanapaswa kupata huduma zinazowawezesha kufanya mtihani kwa haki sawa na wengine.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, alisema kati ya 22,955 waliosajiliwa, wavulana ni 10,223 sawa na asilimia 44.53, huku wasichana wakiwa 12,732 sawa na asilimia 55.47.

Watahiniwa wa kujitegemea wenye mahitaji maalumu ni 73, wakiwemo wenye uoni hafifu 69 na wasioona wanne.

Profesa Mohamed, alisema idadi ya watahiniwa wa shule imeongezeka kutoka 569,883 mwaka 2025 hadi 644,085 mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko la watahiniwa 74,202, sawa na asilimia13.02, ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Katibu Mtendaji huyo, alisema mtihani ni muhimu kwa kuwa, unapima umahiri wa watahiniwa katika yale yote waliyojifunza kidato cha kwanza hadi cha nne.

Pia, alisema matokeo hutumika katika uchaguzi wa watahiniwa wanaojiunga na kidato cha tano pia fani mbalimbali za utaalamu wa kazi kama afya, kilimo, ufundi na nyinginezo.

Previous Post

TASAF YAINUA UCHUMI, YABORESHA HUDUMA ZA JAMII

Next Post

NDEJEMBI ATOA SIKU 180 ZA UKAMILISHAJI SERA MAALUMU

Next Post
NDEJEMBI ATOA SIKU 180 ZA UKAMILISHAJI SERA MAALUMU

NDEJEMBI ATOA SIKU 180 ZA UKAMILISHAJI SERA MAALUMU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

1 year ago
NYOTA YANGA WAPEWA TANO

NYOTA YANGA WAPEWA TANO

7 months ago

Popular News

  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?