• ePaper
Saturday, October 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Uncategorized

MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 24, 2026
in Uncategorized
0
MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Dk. Juma Homera, ameshiriki Site Trust Nishati Safi Marathon 2026 iliyofanyika leo, Oktoba 24, 2026, katika Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.

Kupitia marathon hiyo, jumla ya shilingi milioni 102 zimekusanywa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyosaidia kuboresha huduma za matibabu na kuongeza uwezo wa hospitali hiyo kuwahudumia wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Homera amesema serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034, unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Amesisitiza kuwa matumizi ya nishati safi yatasaidia kulinda afya za wananchi na kuhifadhi mazingira.

Aidha, amezipongeza TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na wadau wengine kwa kushiriki katika kufanikisha marathon hiyo na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika kuendeleza juhudi hizo, REA imetoa majiko 1,000 ya nishati safi, yakiwemo majiko yanayotumia gesi, majiko banifu na majiko ya umeme, ili kuongeza uelewa na kuhamasisha wananchi kutumia teknolojia hizo.

Akiwa ametembelea mabanda ya TANESCO na REA katika viwanja vya marathon hiyo, Dkt. Homera amezitaka taasisi hizo kuandaa mikakati ya kuongeza matumizi ya nishati safi nchini, ikiwemo kuanzisha mifumo ya malipo ya awamu inayowawezesha wananchi kupata teknolojia za nishati safi kwa gharama nafuu.

Previous Post

MWIGULU ANUNUA TIKETI ZA SINGIDA BLACK STARS, TUSKER

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

OUNAHI TEGEMEO MOROCCO AFCON 2025

10 months ago
TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

7 months ago

Popular News

  • MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

    MILIONI 102 ZAKUSANYWA KUPITIA MARATHONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ANUNUA TIKETI ZA SINGIDA BLACK STARS, TUSKER

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YALENGA KUWA MZALISHAJI  BORA WA CHAKULA DUNIANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAASISI 2,682 ZAANZA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, SERIKALI YALENGA TAASISI 30,000

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KUWA KITOVU SOKO LA KABONI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?