• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU AKEMEA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU AKEMEA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU, Dk. Mwigulu Nchemba, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuvielekeza vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki na kali kwa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi katika ngazi za vijiji na kata kuhakikisha kuwa uuzaji na ugawaji wa maeneo unazingatia miongozo ya matumizi bora ya ardhi ili kuzuia migogoro inayoweza kujitokeza, ikiwemo migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Dk. Mwigulu ametoa maagizo hayo leo, Oktoba 26, 2026, wakati akizungumza na wabunge wa Mkoa wa Ruvuma, jijini Dodoma kufuatia vurugu zilizotokea hivi karibuni baina ya wakulima na wafugaji, ambazo zimesababisha madhara mbalimbali vikiwemo vifo.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Serikali haivumilii vitendo vya uvunjifu wa sheria na amewataka wananchi kuheshimiana, kuvumiliana na kuzingatia sheria katika kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.

Amesema Serikali haiungi mkono uchukuaji wa sheria mkononi, utaratibu huo ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi, hivyo kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zilizowekwa na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza wajibu wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru na Watanzania wote walioathiriwa na matukio hayo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na makosa hayo.

Kuhusu matumizi ya ardhi, Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha ardhi inatumika kwa kuzingatia mipango na miongozo iliyowekwa kwa lengo la kuimarisha amani, kuzuia migogoro na kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwa usalama.

Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda tunu za Taifa, hususan amani na mshikamano, akisisitiza kuwa tofauti za kiuchumi na matumizi ya ardhi zinapaswa kutatuliwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.

Kwa upande wao, wabunge wa Mkoa wa Ruvuma wameishukuru Serikali kwa hatua inazoendelea kuchukua kukabiliana na migogoro hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa matumizi ya ardhi pamoja na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao.

Previous Post

YAFUNGUA FURSA KWA KAYA MASKINI

Next Post

TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI

Next Post
TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI

TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI

NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI

10 months ago
HISTORIA YA HESHIMA

HISTORIA YA HESHIMA

8 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?