• ePaper
Friday, April 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 20, 2026
in Burudani, Michezo
0
NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KUMALIZIKA kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 juzi ni wazi ndiyo mwanzo wa maandalizi ya fainali za AFCON 2027 zitakazofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Hatua hiyo imejiri baada ya nchi hizo tatu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kukabidhiwa bendera ya CAF ikiwa ishara ya kuwa mwenyeji rasmi wa fainali hizo za 36 Afrika.

Nchi hizo tatu zilikabidhiwa bendera hiyo katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah jijini Rabat, Morocco baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya Morocco na Senegal, ambapo Senegal ilishinda kwa bao 1-0.

Ndoto ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa fainali hizo ilikamilika mwaka 2023 baada ya CAF kuridhia ombi hilo.

Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, ziliomba kuandaa AFCON kwa pamoja kupitia maombi yaliyopewa jina la ‘Pamoja Bid’, ambapo Kamati ya Utendaji ya CAF iliridhia maombi hayo na kuzipiga chini Botswana, Senegal na Misri ambazo nazo ziliomba kuwa mwenyeji. Algeria iliomba, lakini ilijiondoa juzi.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa nchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa fainali za AFCON katika historia ya soka la Afrika.

VIGEZO PAMOJA BID KUKUBALIWA

Moja ya vigezo vya CAF kwa nchi kuwa mwenyeji wa Afcon ni uwepo wa viwanja sita ambapo viwili viwe na uwezowa kuchukua kila kimoja watu 40,000, viwili kila kimoja watu 20,000 na pia viwanja viwili kila kimoja kiwe na uwezo wa kuchukua watu 15,000.

Timu ya maofisa kutoka CAF ilimaliza ukaguzi wa awali wa miundombinu kuona utayari wa nchi hizo katika kuandaa fainali za AFCON.

Katika ukaguzi huo kwa upande wa Tanzania, CAF ilikagua Uwanja wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, upande wa Zanzibar, ujumbe huo wa CAF ulikagua Uwanja wa Amaan, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Hospitali ya Mnazi Mmoja.

MAKONDA AKUTANA NA DK. MOTSEPE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, juzi alikutana na Rais wa CAF, Dk. Patrice Motsepe jijini Rabat, Morocco na kumkabidhi barua kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na kukabidhi barua hiyo, Makonda aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amemhakikishia Dk. Motsepe kuwa Rais Samia yupo tayari wakati wote kushirikiana na CAF katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kandanda ikiwemo mashindano mbalimbali.

Amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika maandalizi ya kuwa wenyeji wa AFCON 2027 sambamba na Kenya na Uganda na kwamba imedhamiria kuonesha tofauti kubwa na mashindano yaliyopita.

Aidha, Makonda amemuomba Dk. Motsepe kuiangalia Tanzania kimkakati ili mipango inayowekwa na Serikali ipate mafanikio makubwa yanayotarajiwa.

Kwa upande wake Dk. Motsepe amemshukuru Rais Samia kwa kumuandikia barua na salamu zake za upendo na ushirikiano kwa CAF na amemhakikishia kuwa CAF ipo tayari kufanya kazi bega kwa bega na Tanzania ili kufikia maendeleo makubwa katika kandanda.

Motsepe ameelezea kufurahishwa na jitihada kubwa zilizofanywa na Rais Samia na Serikali anayoiongoza katika maendeleo ya mpira ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kufanya mashindano ya CHAN 2024 kwa mafanikio makubwa na maandalizi mazuri yanayoendelea kuelekea AFCON 2027.

Alisema CAF itatuma timu ya wataalamu kwenda Tanzania kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kukamilisha maandalizi makubwa ya AFCON 2027 ambayo yanatarajiwa kushirikisha nchi 28 badala ya 24.

Motsepe ameahidi kuja Tanzania hivi karibuni kujionea maandalizi mbalimbali ya AFCON 2027 na kukutana na viongozi kwa mazungumzo.

Previous Post

DEPU, OKELLO WAMOTO, YANGA IKISHINDA 6-0

Next Post

BARKER ALIA NA NAFASI SIMBA

Next Post
BARKER ALIA NA NAFASI SIMBA

BARKER ALIA NA NAFASI SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASHINDI ‘CHANJA KIJANJA’ WAPATIKANA

WASHINDI ‘CHANJA KIJANJA’ WAPATIKANA

2 months ago
KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

KIHONGOSI AMWASHIA MOTO KIGOGO HOSPITALI MANYONI

3 months ago

Popular News

  • 4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

    4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU AWASHUKIA WACHOCHEZI MIGOGORO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKWELI HADHARANI TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YASIJIRUDIE TENA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MSD YABAINISHA DHAMIRA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA YA AFYA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?