• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SANGU : MICHANGO YA WANACHAMA PSSSF INALINDWA, INAKUA NA KUREJESHA FAIDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SANGU : MICHANGO YA WANACHAMA PSSSF INALINDWA, INAKUA NA KUREJESHA FAIDA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF kwenye mradi wa Rock City Mall jijini mwanza ni ishara kwamba michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida kwa Taifa.

Sangu ameyasema hayo jijini Dodoma Oktoba 27, 2026 wakati Kampuni ya Mwanza Rock City Ltd ambayo ndiyo inasimamia mradi huo ikitoa gawio la jumla ya Shilingi 1.18 bilioni kwa wabia wake watatu ambao ni; PSSSF ambayo imepokea Shilingi 1.07 bilioni; Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepokea Shilingi 71.3 milioni na Manispaa ya Ilemela imepokea Shilingi 47.56 milioni. PSSSF ambayo ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), ndiye mwekezaji mkuu katika mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Constatine Sima, Mstaiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe. Sarah Ng’wani, na Mstaiki Meya wa Halmashauri ya Ilemela, Mhe Renatus Mulunga pamoja na Waheshimiwa Madiwani.

“Ninapenda kutoa pongezi za dhati kwa Bodi na Menejimenti ya Mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii, hususan PSSSF, kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuhakikisha michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida kwa Taifa. Leo hatupokei gawio tu, tunapokea uthibitisho kuwa mfumo wetu wa hifadhi ya jamii uko imara, unakua na unalipa.” Alisema Sangu.

Waziri Sangu alisema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaogozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Dira hiyo inatuambia kuwa Tanzania tunayoitaka ni ya uchumi imara, wa viwanda, usio na umaskini, na wenye ajira zenye staha kwa kila Mtanzania.

“ Hivyo, jitihada hizi zinaonekana kwa wabia wote wa mradi huu wa Rock City Mall ambao ni PSSSF, Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Ilemela kwa usimamizi mzuri wa mradi ambao pia umezalisha ajira. Bila usimamizi wenu pengine leo tusingekuwa hapa kushuhudia tukio hili kubwa kwa wabia hawa. Hongereni sana….!” Alisema.

Nawapongeza PSSSF kwa uwekezaji huu wenye tija kwa taifa letu, kwani nimeelezwa mpaka sasa asilimia 98 ya jengo lina wapangaji. Pamoja na kupendezesha jiji letu la Mwanza, mradi huu unanufaisha watu zaidi ya 1000 kupitia ajira za kudumu na za muda, kwa kufanya hivyo mnaunga mkono juhudi za Serikali kwa kuzalisha ajira kwa vijana wetu, alisema Sangu.

Aidha, Sangu ametoa wito kwa PSSSF na taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) kuhakikisha wanafuata miongozo ya uwekezaji inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania pamoja na sera za uwekezaji za taasisi husika ili kuweza kufanya uwekezaji wenye tija kama huu ambao leo tunashuhudia ukitoa gawio kwa wabia wake.

“Lengo la kuwekeza ni kulinda thamani ya michango ya Wanachama ili wanapokuja kustaafu waweze kulipwa mafao ambayo ni zaidi ya michango yao waliyokuwa wanachangia katika Mfuko, hivyo, kutokana na mafanikio ya mradi huu tunaamini sehemu hii ya gawiwo itachangia katika kuwafanya wanachama wa PSSSF KULIPWA JANA.” Alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mwanza Rock City Company Limited, Fortunatus Magambo, amelinganisha tukio hilo na siku ya mavuno.

“Hakika ile mbegu tuliyopanda, ilimea vyema na hatimaye leo tunavuna tulichopanda, hakika leo ni siku muhimu sana.” Alisema Magambo.

Magambo alisema, Rock City Mall ina mchango kwa jamii na maendeleo ya Jiji la Mwanza kwa kuwa kituo cha huduma mbalimbali, ambapo faida zake ni pamoja na; Kurahisisha upatikanaji wa huduma, inakusanya huduma mbalimbali katika eneo moja, zikiwemo maduka, huduma za benki na migahawa mbalimbali.

“Hii huwasaidia wananchi kuokoa muda na kurahisisha shughuli zao, Rock City Mall inatoa nafasi za biashara na ajira, inatoa maeneo ya kufanyia biashara na kuchangia fursa za ajira kupitia maduka, migahawa na huduma nyingine zinazopatikana hapo.

Aidha, Magambo alisema, PSSSF inawekeza ili kulinda thamani ya michango ya Wanachama ili wanapokuja kustaafu waweze kupata mafao zaidi ya michango yao waliyokuwa wanachangia katika Mfuko.

“ Uwekezaji wa Mfuko unaongozwa na Mwongozo wa Uwekezaji kutoka Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Sera ya Uwekezaji ya Mfuko. Sehemu kubwa ya uwekezaji upo katika dhamana za serikali, hisa za kampuni na amana za mabenki na si kwenye majengo kama wengi wanavyodhani.” Alisisitiza.

Previous Post

MAGEREZA: LISSU  HAJAGOMA KULA, YUPO SALAMA

Next Post

WAZIRI HOMERA ATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA WA FUTI ZA UJAZO BILIONI 223

Next Post
WAZIRI HOMERA ATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA WA FUTI ZA UJAZO BILIONI 223

WAZIRI HOMERA ATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA WA FUTI ZA UJAZO BILIONI 223

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

MAFUNZO YA ITIKADI MSINGI IMARA KATIKA KUIMARISHA UHAI WA CCM

1 month ago
MGOMBEA Mwenza wa Urais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Butiama, mkoani Mara. (Picha na Abdurahman Jumanne)

BALOZI DK. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI MWALIMU NYERERE

1 year ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?