• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imeimarisha uwezo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa kulipatia leseni nne za utafutaji, hatua inayoliwezesha Shirika hilo kumiliki vitalu vyake na kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa rasilimali hizo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Dk. Juma Zuberi Homera, Oktoba 28, 2026, wakati wa hafla ya utiaji saini wa leseni nne za utafutaji wa mafuta na gesi asilia iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Homera amesema hatua hiyo ina msingi katika Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, inayowezesha TPDC kuwa na vitalu vyake vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, hivyo kuimarisha uwezo wa Shirika hilo kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utafutaji wa rasilimali hizo.

“Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi asilia kwa kuhakikisha shughuli zote zinafanyika kwa kuzingatia sheria, usalama, utunzaji wa mazingira na maslahi mapana ya Taifa,” amesema Dk. Homera.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Wizara ya Nishati, TPDC, Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na wadau wengine wa sekta hiyo ili kuhakikisha shughuli za utafutaji na uendelezaji zinatekelezwa kwa ufanisi na kila taasisi inatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, Dk. Homera amesema Serikali inaendelea na juhudi za kuongeza akiba ya gesi asilia nchini, akibainisha kuwa uchimbaji wa visima vitatu katika kitalu cha Mnazi Bay, mkoani Mtwara, umekamilika. Visima viwili ni vya uzalishaji na kimoja ni cha utafiti.

Sambamba na kuimarisha shughuli za utafutaji na uzalishaji, Serikali inaendelea kupanua matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa umeme, majumbani, viwandani, taasisi na vyombo vya moto kupitia teknolojia ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG).

Kwa mujibu wa takwimu za hadi Septemba 2026, Tanzania ilikuwa na vituo 22 vya CNG vinavyotoa huduma, karakana 20 za kufunga mifumo ya gesi asilia katika vyombo vya moto na zaidi ya vyombo vya moto 20,000 vinavyotumia CNG. Aidha, viwanda 57, taasisi 31 na takribani kaya 3,000 zilikuwa zimeunganishwa na miundombinu ya gesi asilia.

Dk. Homera amesisitiza kuwa Serikali inalenga kuhakikisha kuimarika kwa uwezo wa TPDC na maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi asilia yanaleta manufaa ya moja kwa moja kwa Watanzania kupitia fursa za ajira, mafunzo, ujenzi wa uwezo wa wataalamu wa ndani na kuongeza ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika utoaji wa bidhaa na huduma.

Previous Post

DC HANANG’ AWATAKA VIONGOZI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KWA WAKATI

Next Post

KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI

Next Post
KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI

KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA

PAWASA, MTEMI WAZIPA MCHONGO YANGA, SIMBA

9 months ago
KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

KIHONGOSI: TANZANIA HAIWEZI KURUDI UKOLONI

11 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?