• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KINANA ATAJA MAMBO MATATU YA UJASIRI ALIYOFANYA DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 3, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
KINANA ATAJA MAMBO MATATU YA UJASIRI ALIYOFANYA DK. SAMIA

MAKAMU Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana

0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Arusha

MAKAMU Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, ameyataja mambo matatu ambayo Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan ameyatekeleza kwa ujasiri mkubwa na kuthibitisha uwezo wake katika kuendelea kuliongoza Taifa.

Ameyataja mambo hayo ni utekelezaji wa ilani ya CCM, ahadi za aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli na ahadi ambazo Dk. Samia, alizitoa katika ziara zake mbalimbali kwa wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Kinana amesema Dk. Samia, ametekeza kwa vitendo mambo hayo matatu kwa ujasiri mkubwa.

“Ilani ya CCM imetekelezwa, ahadi za mgombea zimetimizwa kwa asilimia 100, ahadi zake binafsi alizozitoa alipotembelea wananchi mikoani, nazo amezitekeleza kwa asilimia 100.

“Taifa linahitaji kiongozi mwenye busara, ushirikiano wa dhati na wenzake ili kuongoza kwa kuweka vipaumbele vinavyotekelezeka ambapo Dk. Samia amethibitisha sifa hizo,”amesema.

Kinana ameeleza kuwa, kazi za Dk. Samia, zimeonekana kila kata na kila mkoa nchini, huku mashahidi wa kweli ni wananchi wanaofaidika kupitia miradi mbalimbali.

Pia, amesema kauli mbiu ya CCM katika uchaguzi mkuu ya ‘Kazi na Utu’ ina maana kubwa, kwani inatambua msingi wa utu na haki kwa Taifa.

“Baba wa Taifa alikuja na kauli mbiu Uhuru na Kazi, baadaye ikaja Uhuru ni Kazi, leo tunasema Kazi na Utu. Dk. Samia ameonyesha mfano bora, anafanya kazi kwa kujituma na kuwajali Watanzania wote,” alisema.

Ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29, mwaka huu kumpa kura Dk. Samia kwa kuwa, ameonesha uongozi wa mfano na ufanisi mkubwa.

“Dk. Samia anafanya kazi kwa kujituma na kuwajali wananchi, mimi binafsi nakuombea kura na ninaamini Watanzania wote tutaungana kumpa kura,” alisema.

Naye, Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu anayewakilisha vijana, Lilian Mwacha, alisema vijana wa Arusha wana kila sababu ya kumuunga mkono Dk. Samia kutokana na matokeo makubwa katika utalii.

Amesema hali hiyo, imefanya ongezeko kubwa la watalii kutoka 600,000 hadi milioni tano hali iliyowezesha vijana wengi kunufaika na ajira.

Previous Post

DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

Next Post

DK. SAMIA AAHIDI MKAKATI WA NGANO

Next Post
DK. SAMIA AAHIDI MKAKATI WA NGANO

DK. SAMIA AAHIDI MKAKATI WA NGANO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

3 weeks ago
POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

3 weeks ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?