Na MWANDISHI MAALUMU,
Songea
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, amewaonya watendaji wa serikali wanaokwamisha shughuli za maendeleo ya vijana katika maeneo yao, hawatavumiliwa.
Akizungumza wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, ambako alikutana na vijana wajasiriamali, wanaofanya shughuli katika Soko la Bombambili na Stendi ya magari ya Ruhuwiko, jana, Nanauka alisema kwamba, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ana dhamira ya kweli kuhakikisha vijana wanafanikiwa.
Nanauka ambaye alitumia mikutano yake wilayani humo kukutana na kusikiliza mawazo na ushauri wa vijana ikiwemo kutatua kero zao.
Alisema Rais Dk. Samia, ana dhamira ya dhati kuona vijana wanashiriki kikamilifu ujenzi wa nchi, hivyo aliwasihi waitunze amani na kutumia njia ya mazungumzo, kutatua changamoto ndiyo maana akaunda wizara maalumu inayohusika na vijana.
Aidha, Waziri Nanauka, aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya, kuweka utaratibu wa kutoka ofisini na kuwafuata vijana walipo, kusikiliza hoja na kero zinazowakabili.
DC SONGEA
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilhelm Ndile, alisema wamepokea maelekezo ya waziri huyo na kwamba, wataratibu vikao na wajasiriamali vijana na waendesha bodaboda kuzitafutia suluhisho changamoto walizozitoa katika ziara ya Nanauka.
Akizungumza katika kikao na Waziri Nanauka, Arnold Mgawo, Mkazi wa Bombambili, alisema anapenda kuona Rais Dk. Samia, anadhibiti vitendo vya utekaji na kuimarisha demokrasia hasa vijana kuwa na uhuru wa kuzungumza .
Naye Benedict Tembo, alimshauri Waziri Nanauka, kutowasikiliza watendaji wa serikali wasiochapa kazi, wenye kupotosha ukweli wa changamoto zao, badala yake, achukue hatua dhidi ya wazembe.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Mary Maganga, mkoa huo una vijana 676,144 kati ya watu 1,848,394. Mary alisema




