• ePaper
Monday, January 19, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI ATOA MAAGIZO KWA MADIWANI 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 8, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
KIHONGOSI ATOA MAAGIZO KWA MADIWANI 

KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi

0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka madiwani kufanya kazi zinazobeba ajenda za wananchi, zitakazotoa majawabu ya kero katika maeneo yao.

Pia, CCM imesema itaendelea kusimamia vyema misingi ya uadilifu kwa watendaji wa Chama.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, jijini Dar es Salaam, alipozungumza na UHURU.

“Wito wangu kwa madiwani wote, mhakikishe mnatunga sheria ambazo ni rafiki kwa watu na sio kandamizi zitakazowaumiza wananchi, mkawe watetezi na washauri wa kulinda maslahi ya umma katika maeneo yenu,” alisema.

Kihongosi alisema Chama kitatoa miongozo ya namna bora ya kufanya kazi kwa madiwani wa CCM.

“Madiwani wakafanye kazi zinazobeba ajenda za wananchi ambazo zitatoa majawabu ya kero katika maeneo yao.

Kwa watakaokwenda kinyume na maagizo ya Chama, Chama kina utaratibu wake, kina vikao vyake katika ngazi husika iwapo mtu amekosea watamwita kwenye vikao na kufanya uamuzi ambao unakubalika kikatiba ndani ya Chama,” alisema Kihongosi.

Aliwataka madiwani hao kuwa mstari wa mbele kukisemea Chama kwa wananchi, kutokana na   maendeleo yaliyopatikana nchini, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wao, baadhi ya madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam, waliahidi kuwatumikia wananchi ipasavyo katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Diwani wa Kata ya Kigogo (CCM), Manispaa ya Kinondoni, Nassib Limira, alisema amejipanga kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu.

“Tumeingia kazini rasmi, katika ahadi zipo za muda mfupi na mrefu, wananchi wa Kigogo wanipe muda niwatumikie.

Tuliahidi mambo mengi katika kampeni, mfano upanuzi wa shule ya sekondari na kituo cha afya, kwa hiyo hayo yote tunaanza kuyafanyia kazi mara moja,”alisema.

Diwani wa Kata ya Somangira (CCM), Manispaa ya Kigamboni, Juma Luja, alisema aliahidi ajira kwa vijana na miradi ya ujenzi wa barabara kazi ambayo imeanza.

 “Sasa nakwenda kuwasimamia vijana wa kata yangu wenye sifa kuhakikisha wanaingia katika mchakato wa kupata ajira,”alisema.

Diwani wa Viti Maalumu (CCM), Manispaa ya Temeke, Nuru Cassian, alisema atasimamia mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu iwafikie kwa muda sahihi.

Previous Post

AMANI YAWAIBUA WABUNGE

Next Post

LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI

Next Post
LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI

LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JESS NAZ APATA MAJANGA

JESS NAZ APATA MAJANGA

1 month ago
NUSU FAINALI YA VIGOGO AFCON

NUSU FAINALI YA VIGOGO AFCON

5 days ago

Popular News

  • KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

    KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MIGIRO KATIBU MKUU WA  KWANZA MWANAMKE NA MIKAKATI YA KUIMARISHA MASHINA KATIKA MITAA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SAFARI KUMALIZA CHANGAMOTO UMEME IRINGA, DODOMA YAIVA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA YAINGIA 10 BORA KUVUTIA UWEKEZAJI AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AMREJESHA MAKONDA AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?