• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 8, 2025
in Habari, Kitaifa
0
LATRA YAONGEZA VIBALI 70 MABASI MIKOANI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imeongeza zaidi ya vibali 70 vya muda kwa mabasi yanayosafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali nchini.

Imesema hatua hiyo imelenga kukabiliana na ongezeko la uhitaji wa usafiri kuelekea msimu wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

Akizungumza na UHURU, Ofisa Mfawidhi wa LATRA katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, Rukia Kibwana, alisema mwisho wa mwaka ni kipindi ambacho abiria huongezeka, hivyo mamlaka kuongeza idadi ya mabasi ni jambo la kawaida kuondoa msongamano.

“Hadi kufikia jana mchana, vibali zaidi ya 72 vilikuwa vimetolewa kwa mabasi ya ziada, hatua iliyolenga kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bila usumbufu,” alisema.

“Hadi leo (jana) mchana tulitoa vibali zaidi ya mabasi 72. Usafiri mwingi ni jioni, unapoona watu wamejaa stendi wanakuja kusubiri mabasi yao na wengine wanawahi kukata tiketi,” alisema.

Rukia aliwataka wananchi kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, akieleza LATRA inafahamu idadi kubwa ya watu husafiri kwenda kuungana na familia zao mikoani, hivyo mamlaka inaendelea kusimamia na kuratibu uongezaji wa mabasi kadri inavyohitajika.

“Niwaombe sana wananchi kuwa na uvumilivu kwa sababu tunajua baadhi ya watu wanapenda kwenda kuwasalimia ndugu zao katika mikoa mbalimbali. Niwaombe kuendelea kutuamini,” aliongeza.

LATRA imekuwa ikitoa vibali vya muda kila kipindi cha msimu wa sikukuu na sherehe kubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa usafiri unakuwa wa uhakika hususani mikoa ya kaskazini.

Previous Post

KIHONGOSI ATOA MAAGIZO KWA MADIWANI 

Next Post

RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

Next Post
RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

MWIGULU: MAMBO MAZURI YANAKUJA, AIPA TANO SERENGETI BOYS

1 week ago
GAMONDI ALIA NA MUUNGANIKO

GAMONDI ALIA NA MUUNGANIKO

9 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?