• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WANNE ‘BYE BYE’ YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 12, 2025
in Burudani, Michezo
0
WANNE ‘BYE BYE’ YANGA
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufunguliwa rasmi, Januari 15, mwaka huu uongozi wa Klabu ya Yanga unatarajia kuwatoa kwa mkopo wachezaji wanne, kwenda kuongeza kiwango katika timu mbalimbali.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa timu hiyo imepanga kuwatoa kwa mkopo wachezaji wake wanne ambao ni Faridi Mussa, Denis Nkane, Aziz Andambwile na Offen Chikola.

Tayari Klabu ya Yanga, imepokea ripoti kutoka kwa Kocha Pedro Goncalves ili kufanya uboreshwaji wa kikosi chao ikiwemo kuwatoa baadhi ya wachezaji kwenda kwa mkopo timu zingine.

Kwa hivi sasa, Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa muda kupisha michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinazotarajiwa kuanza Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani nchini Morocco.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa kwa hivi sasa viongozi wa timu hiyo wanaendelea na mchakato wa kuipitia ripoti kuhakikisha wanaifanyia kazi mapema ili kukamilisha wa wachezaji wanaohitajika.

Kamwe alisema mwalimu ameamua kutoa ripoti hiyo mapema lengo kubwa ni kama ataongezewa wachezaji wapya, waweze kujiunga na wengine katika maandalizi ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri utakaochezwa Januari mwaka huu.

“Tayari tumeshapokea ripoti kutoka kwa mwalimu ambapo katika ripoti hiyo amejumuisha wachezaji ambao anawahitaji na wale ambao wanatakiwa kutolewa kwa mkopo, hiyo yote ni kuboresha kikosi kiweze kuwa cha ushindani zaidi na kufanya vizuri katika mechi za ligi ya ndani na michuano ya kimataifa,” alisema Kamwe.

Kamwe alisema wao hawatasajili kwa mihemko endapo watamhitaji mchezaji yeyote, watafuata utaratibu ili kuhakikisha wanaisa saini yake.

Alisema kuwa lengo la Kocha Pedro  kuwasilisha ripoti yake mapema ni kutaka viongozi wafanyie kazi mapema na kukamilisha usajili kwa wakati.

Kamwe alisema kwa hivi sasa uongozi unaendelea kuhakikisha wanatafuta wachezaji wenye kiwango bora watakaowaletea mafaniko ndani ya timu hiyo.

KUHUSU YAO NA MZIZE

Kamwe alisema kuhusiana na mchezaji wao Clement Mzize kwa hivi sasa anaendelea vizuri na anaweza kurejea katika kikosi hicho mwishoni mwa Januari, mwakani.

“Tunajua wengi wanahitaji kumwona tena Mzize, ila niwatoe hofu mchezaji huyo anatarajiwa kurejea dimbani mwishoni mwa Januari, mwakani,” alisema.

Kuhusu Yao Kouassi, alisema kwa hivi sasa wanasubiria ripoti ya kocha wa viungo ili kujua kama ataweza kurudi katika hali yake ya ubora kama ilivyokuwa mwanzoni.

Alisema bado Yao ni mchezaji wa Yanga na analipwa, walimwondoa katika kikosi sababu alikuwa na majereha, akishapona Januari, mwakani wataangalia kama kocha bado atakuwa anamuhitaji.

“Tunasubiria kocha aseme kama bado anamuhitaji sababu katika nafasi yake kuna watu wawili wengine ambao ni Israel Mwenda na Kibwana Shomari hivyo mwalimu yeye atachagua nani wa kumuondoa hivyo nafasi yake ipo kwa Kocha Pedro,” alisema Kamwe.

Previous Post

DK. SAMIA APOKEA HATI ZA MABALOZI, ATEUA VIGOGO PSSSF, TANESCO 

Next Post

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

Next Post
SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WACHINA WANAODAIWA KUKUTWA NA MABILIONI WAPANDISHWA KORTINI

WACHINA WANAODAIWA KUKUTWA NA MABILIONI WAPANDISHWA KORTINI

4 months ago
CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

8 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?