• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

UPATIKANAJI MAJI DAR SASA KWA USAWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 13, 2025
in Habari, Kitaifa
0
UPATIKANAJI MAJI DAR SASA KWA USAWA
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

WAZIRI wa Maji, Juma Aweso, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kugawa maji kwa usawa, uwazi na kutoa ratiba ya eneo husika, wananchi wapate muda wa kujiandaa.

Aweso, alisema hayo katika mkutano kati ya DAWASA na Wahariri wa Vyombo vya habari, kuzungumzia hali ya upatikanaji maji Jijini Dar es Salaam.

“Ni wazi kuna vitu vingine viko nje ya uwezo wetu ikiwemo kuchelewa kunyesha mvua ya vuli, lakini niwaombe wananchi tuendelee kuwa na mshikamano katika kipindi hiki cha mpito.

“Nasisitiza DAWASA, hiki kilichopo au tunachozalisha, gaweni maji hayo kwa usawa na uwazi kwa kueleza ratiba zenu ni saa ngapi, maji yatatoka katika eneo linalokusudiwa huduma hiyo, wananchi wajiandae kupokea hayo maji, kwa kufanya hivyo, itapunguza malalamiko kutoka kwa wananchi,” alisema.

Pia, alisema jambo hilo liwe shirikishi kwa watu wote, wakiwemo wadau wa sekta binafsi, watengeneze namna nzuri ya kugawa maji kwa kushirikiana na DAWASA katika visima vilivyochimbwa.

Pia, kutoa elimu kwa jamii juu ya namna ya kutunza vyanzo vya maji na kuepuka uharibifu wa mazingira.

MTENDAJI MKUU DAWASA

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,  Mhandisi Mkama Bwire, alisema upatikanaji maji katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani, umeendelea kukumbwa na changamoto kubwa kutokana na ongezeko la mahitaji.

“Takwimu za sensa ya mwaka 2022, zinaonesha eneo hili lina watu takribani milioni saba, huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia karibu milioni 17 ifikapo mwaka 2050 katika kipindi cha mwaka 2023–2026.

“Ongezeko hili limeongeza shinikizo kwa mifumo ya usambazaji maji iliyopo, ambayo tayari ilikuwa na upungufu hata kabla ya changamoto za msimu wa sasa,” alisema.

Alisema mahitaji ya maji, yamezidi kuongezeka siyo kwa sababu ya idadi ya watu pekee, bali kutokana na ongezeko la shughuli za kiuchumi na kubadilika kwa matumizi ya maji kwa kaya.

Akitolea mfano, alisema mtu aliyekuwa akitumia lita 40 kwa siku, sasa anatumia lita 60,  hivyo kuongeza mzigo kwa mifumo ya uzalishaji.

Mtendaji huyo, alisema hadi sasa, uwezo wa uzalishaji upo katika lita milioni 534 kwa siku, asilimia 93 hutegemea vyanzo vya juu ya ardhi na asilimia saba, hutokana na visima.

Alisema kipindi hiki cha kiangazi, chanzo kikubwa cha maji hususan Mto Ruvu Chini, kimeathirika zaidi kutokana na upungufu wa mvua misimu ya vuli na masika.

Alieleza hali hiyo, imeshusha uzalishaji kutoka zaidi ya lita milioni 270 kwa siku, hadi takribani lita milioni 50 kwa sasa na kuathiri maeneo mengi ya utoaji huduma, yakiwemo ya Tegeta, Kawe, Mbezi, Kinondoni, Tabata, Kinyerezi na maeneo ya katikati ya jiji.

Alitaja sababu nyingine zinazochangia upungufu ni shughuli za kibinadamu ndani ya bonde la mto, ambazo zimebadilisha mikondo ya maji na kupunguza kiasi kinachofika katika mitambo ya uzalishaji.

Pia, kupanda kwa joto, kumesababisha uvukizaji mkubwa katika vyanzo vya juu ya ardhi, hali iliyosababisha kupungua kwa kiwango cha maji yaliyokuwepo.

Katika baadhi ya maeneo, mito midogo imetoka katika mkondo wake wa asili, hivyo kupunguza maji yanayoelekea katika chanzo kikuu.

Katika hatua za muda mfupi, DAWASA imeimarisha uchimbaji na ufufuaji visima katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo yake ya pembezoni.

Visima ambavyo awali vilikuwa vikizalisha lita milioni 17 hadi 20 kwa siku, sasa vinaboreshwa kufikia lita milioni 35 hadi 40.

Pia, maji kutoka visima hivyo, yanatumika kuimarisha huduma katika maeneo katikati ya jiji kama Kariakoo ili kupunguza utegemezi kutoka vyanzo vya juu ya ardhi.

“Kampeni za elimu kuhusu uhifadhi wa maji zinaendelea kutolewa kwa wananchi, wakihimizwa kuhifadhi maji kwa matumizi ya siku kadhaa kutokana na hali isiyotabirika ya upatikanaji wa maji.

“Hatua hizi, zimeanza kusaidia kupunguza ukubwa wa tatizo kwa kiwango fulani,” alisema.

Vilevile mtendaji, huyo alitaja hatua za muda mrefu ikiwepo serikali kuendelea kutekeleza ujenzi wa Bwawa la Kidunda, ambalo limefikia zaidi ya asilimia 35 ya kazi.

“Bwawa hilo, linatarajiwa kusaidia kudhibiti mtiririko wa Mto Ruvu, kuhakikisha upatikanaji wa maji katika vipindi vyote vya mwaka na kuzalisha megawati 20 za umeme.

“Miundombinu ya msingi ya kusafirishia maji tayari, imeanza kukamilika, hatua itakayowezesha mradi kuingia katika awamu ya kasi ya juu ya ujenzi,” alisema.

“Hatua ya kimkakati zaidi ni kuanzishwa kwa Mradi wa Maji wa Gridi ya Taifa, utakaotumia maji kutoka Mto Rufiji kuongeza uzalishaji wa zaidi ya lita bilioni 1.5 kwa siku ifikapo mwaka 2050.

Alisema mradi huo, utasaidia kuunganisha vyanzo vikubwa vya maji na kupunguza utegemezi wa chanzo kimoja na kuendelea kuchimba visima vipya katika maeneo ya pembezoni mwa jiji, kuimarisha upatikanaji wa maji.

Previous Post

DK. NCHIMBI KUONGOZA KUAGWA JENISTA MHAGAMA

Next Post

UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

Next Post
UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

TRA YABAINI MCHEZO MCHAFU UKWEPAJI KODI  BANDARI KAVU

2 months ago
UKWASI MIFUKO HIFADHI YA JAMII NCHINI, WAPAA

UKWASI MIFUKO HIFADHI YA JAMII NCHINI, WAPAA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?