• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 14, 2025
in Burudani, Michezo
0
UWANJA WA SOKA DODOMA WAFIKIA 2.7%

Mwonekano wa Uwanja wa mpira wa miguu Dodoma

0
SHARES
80
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema ujenzi wa Uwanja wa soka wa kisasa jijini Dodoma, unaendelea kwa kasi na hivi sasa umefikia asilimia 2.7.

Hatua hiyo ni sehemu ya ahadi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa kuongoza nchi katika kipindi cha pili cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza.

Rais Dk. Samia aliahidi hayo katika mikutano mbalimbali ya kampeni za Uchaguzi Mkuu, kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu.

Akizungumza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema, kazi ya ujenzi wa Uwanja wa michezo Dodoma imeanza na hivi sasa umefikia asilimia 2.7.

Msigwa alisema hayo wakati wa kikao kazi na kampuni inayojenga uwanja huo ya LIMONTA kutoka nchini Italia ambapo alisisitiza kazi ya ujenzi imechelewa kuanza kutokana na kuhamishwa kwa eneo la ujenzi lililopangwa awali.

Vilevile, Msigwa alitoa maagizo kwa mkandarasi huyo kuongeza mitambo ya kufanyia kazi, watumishi na wataalamu ambao ni wazawa ili kuwezesha vijana kupata ajira sambamba na kupata ujuzi zaidi kwa wazawa hao.

“Mpaka hivi sasa kuna jumla ya wakandarasi 34 ambapo 27 ni Watanzania na wanaendelea kufanya kazi na wengine wataendelea kuajiriwa.

“Lengo ni kuhakikisha Watanzania wanapata ajira kwa wingi kupitia ujenzi wa miundombinu ya michezo nchini,” alisema Msigwa.

Katika hatua nyingine, Msigwa amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha kazi kwa wakati ambayo itakua na hadhi ya makao makuu ya nchi.

Alisema kwa upande wa Uwanja wa Arusha, ujenzi unakwenda vizuri ambapo hivi sasa umeshafikia asilimia zaidi ya 70.

“Katika ujenzi wa Uwanja wa Arusha, hivi sasa umefikia zaidi ya asilimia 70 ambapo mkandarasi anaendelea na ujenzi kwa kasi, tunaamini ujenzi wa viwanja vyote utakamilika kwa wakati kabla ya kuanza kwa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambapo Tanzania tutakuwa wenyeji tukishirikiana na Kenya na Uganda,” alisema Msigwa.

Naye Mwakilishi wa kampuni ya LIMONTA Angelo Redolfi, ameahidi kufanya kazi hiyo kwa bidii na uwazi kwa kuzingatia maelekezo ya serikali ili kukamilisha uwanja wenye viwango bora vinavyotakiwa.

 “Ninaahidi kufanya kazi kwa bidii na uwazi kwa kuzingatia maelekezo ya serikali ili kukamilisha uwanja wenye viwango bora vinavyotakiwa,” alisema.

Previous Post

UPATIKANAJI MAJI DAR SASA KWA USAWA

Next Post

KAPOMBE AFUNGUKA STARS

Next Post
KAPOMBE AFUNGUKA STARS

KAPOMBE AFUNGUKA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

STARS IFANYE NINI KUTOBOA AFCON?

STARS IFANYE NINI KUTOBOA AFCON?

7 months ago
TAJI LAONGEZA MZUKA YANGA

TAJI LAONGEZA MZUKA YANGA

6 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?