NEW YORK, Marekani
MCHEZAJI mahiri wa mpira wa kikapu, LeBron James yupo mbioni kuingia mabadiliko mapya katika mchezo huo.
Nyota huyo siri yake imevuja ambapo Wakala wa LeBron James amedokeza uwezekano wa kuhama Lakers huku New York Knicks ikionekana kumwania.
KAULI YA TAJIRI
Tajiri Paul hivi karibuni ametoa maoni yake juu ya mshambuliaji huyo kuhama Los Angeles Lakers na kutua New York Knicks.
“Kuna kitu hicho, lakini ni mapema mno kusema zaidi juu ya jambo hilo,” alisema Paul.
LeBron James amehusishwa na uwezekano wa kufanya biashara na New York Knicks, licha ya kucheza mechi saba pekee msimu huu ndani ya timu yake ya sasa.
ALAMA ALIYOWEKA
LeBron James kwa asilimia kubwa tayari ameacha alama isiyoweza kusahaulika kwa mashabiki wa Los Angeles Lakers.
Kwani kikosi hicho, kimefanikiwa kuweka rekodi ya 17-6 na kushika nafasi ya pili katika Mkutano wa Magharibi wa NBA.
MASWALI
Hata hivyo, maswali kuhusu uwezekano wa kutwaa ubingwa wa timu hiyo yameibuka.
Kulingana na tathmini ya uangalifu ya wakala wa James, Rich Paul ambaye amezungumzia hadharani tetesi za kuhamia New York Knicks alisema kuna uwezekano timu hiyo ikakosa ubingwa.
Lakini bado mashabiki wa timu hiyo, wana imani kwamba itafanya vizuri na kutwaa ubingwa NBA.
UTANI
LeBron hivi karibuni alimtania shabiki wa timu yake mbele ya umati kuwa bado hana furaha.
Katika kipindi cha hivi majuzi cha Game Over na Max Kellerman, Rich Paul aliweka msimamo wake wazi kuhusu nafasi ya Lakers kufanya vizuri.
"Sidhani wanatosha kufika fainali, lakini ubingwa kazi ipo, sidhani kama wana kikosi cha kushindana, kwa mtazamo wangu,”alisema Paul.
Licha ya utendaji mzuri wa Lakers, wakiwa na rekodi ya 6-1 katika michezo iliyomshirikisha James na rekodi ya 11-5 bila yeye, Paul alisema ana mashaka kuhusu uwezo wao wa kushindana.
MSISITIZO WA PAUL
Tajiri huyo alisisitiza kwamba James amejitolea kumaliza msimu wa 2025-26 akiwa na Lakers.
Lakini Paul, aliacha mlango wazi kwa uvumi wa nyota huyo kuhama.
UGUMU UPO HAPA Lakers hivi sasa wanakabiliwa na njia ngumu ya kutwaa ubingwa wa kikapu.
Hata kwa uwepo wa James ,Luka Doncic na Austin Reaves bado kunaonekana timu hiyo ina shida.
UWAZI HUU HAPA
Tajiri Paul aliweka wazi kwamba LeBron anaweza kubaki ndani ya timu hiyo lakini kwa tathmini yake ya umakini. Paul alithibitisha uaminifu wa wa mchezaji huyo wa Lakers kuwa muda uliosalia wa msimu huu ni mdogo. "Ataondoka lakini swali la msingi anaenda wapi?, LeBron anafanya kazi nzuri ndani ya Knicks kuwa bora zaidi,” alisema Paul. UANGALIZI
Pasul alieleza kwamba uchezaji wa LeBron na uwezo wa Lakers umekuwa ni kitu kimoja cha k ukuzau wezo wa mchezaji huyo. “Lakini zaidi ya hayo, mlango ni wazi kwa biashara inayowezekana kufanyika ya kumuuza,”alidokeza Paul. MJADALA WAZUKA Baada ya kauli ya Paul, mjadala umezuka kuhusu uwezekano wa kufanyika biashara ya kuuzwa kwa mchezaji huyo kutoka Knicks. Baadhi ya mashabiki na wachambuzi wameanza kujadili nini kitatokea kama mchezaji huyo ataondoka. Mashabiki hao, wanaonekana kuhoji James ataiongoza Lakers katika kipindi kilichosalia cha msimu na matarajio mapya ya ubingwa. Hali ya kutoridhishwa kwa Paul kunaonesha kwamba hata wasomi kama James wanahojia juu ya kuwepo jambo hilo. KAULI YA LeBRON JAMES
LeBron James hivi karibuni alikataa kuzungumzia mipango yake ya siku zijazo.
“ Kwa sasa nipo Lakers, inaweza kuwa wakati mechi za mchujo zitakapowasili mwezi Aprili, mwakani nikawa bado ninacheza hapa,”alisema nyota huyo.
Mshambuliaji huyo alikiri kwamba mawazo yake yapo katika mechi za mchezo wa robo fainali ya Kombe la NBA.
“Nafahamu tumepoteza mechi, Lakers tulifungwa na San Antonio Spurs kwa vikapu 132-119, kwa maana hiyo nina mambo mengi ya kufikiri, juu ya jambo hili,” alisema.
Alifafanua kuwa miaka miwili iliyopita, Lakers walipokwenda Las Vegas na kutwaa ubingwa wa kwanza wa Kombe la NBA, aliwahi kutahadharisha kwamba walikuwa na safari ndefu ya mafanikio.
“Lakini hii ilikuwa baada ya kuangalia baadhi ya mambo, nikasema hivyo, haikuwa njia ya kuashiria kitu kibaya,”alisema mchezaji huyo wa kikapu.
MAISHA YAKE LeBron Raymone James Sr. ni mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu wa Los Angeles Lakers.
Mchezaji huyo alizaliwa Desemba 30, mwaka 1984 na hivi sasa ana umri wa miaka 40.
Alizaliwa sehemu inayoitwa Akron, Ohio nchini Marekani na hivi sasa anaichezea timu ya Los Angeles Lakers.
Anatumia jezi namba 23 ambapo amekuwa anacheza nafasi ya mshambulizi katika timu yake.
Alijiunga mwaka 2018 na Los Angeles Lakers kwa uhamisho wa thamani ya dola bilioni 1.3 za Marekani.
Jarida la Forbes liliwahi kutoa taarifa kwamba mchezaji huyo ana mchumba wake, Savannah James.
Wapenzi hao, wamejaliwa kupata watoto wawili ambao ni Bronny James na Bryce James.
Lakini mshambuliaji huyo ana marafiki zake wa karibu ambao ni Stephen Curry, Kobe Bryant na Kevin Durant.




