• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. MWIGULU ASHUSHA PRESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 30, 2025
in Habari, Kitaifa
0
DK. MWIGULU ASHUSHA PRESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ameagiza kukamilika haraka usanifu wa mradi wa kutoa maji Mto Rufiji, ambao ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025/2030.

Ilani ya CCM inaielekeza serikali kuanzisha Gridi ya Taifa ya Maji, kwa kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya Ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika.

Gridi hiyo itahakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya nyumbani, mifugo na shughuli za umwagiliaji.

Dk. Mwigulu alitoa maagizo hayo, katika ziara ya kikazi aliyofanya mkoani Pwani, kukagua hali ya uzalishaji na usambazaji wa maji Ruvu Chini.

“Nataka nipate taarifa kamili ya usanifu wa mradi unaopangwa Mto Rufiji yakiwemo makadirio ya gharama, waanzilishi wake na utekelezaji uanze mara moja kutokana na dharura iliyopo,”alisema.

Alisema hatua hiyo ni miongoni mwa mikakati ya serikali kuondoa changamoto ya upungufu wa maji.

Katika kuhakikisha changamoto hiyo inapungua, Dk. Mwigulu alisema serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni 100 za miradi ya maji na miundombinu mingine.

Alisema mikakati hiyo inajumuisha kutekeleza miradi mikubwa ya maji, kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji na kuhakikisha maji yanapatikana kwa uhakika katika maeneo yote yanayokabiliwa na ukame.

Dk. Mwigulu alisema hatua ya serikali ni endelevu na imepangwa muda mrefu, ikilenga kutoa suluhisho la kudumu kuondoa changamoto ya maji.

Alisisitiza miradi ya maji ni jambo la uhai kwa wananchi na hayawezi kuahirishwa, huku akihakikisha mpango wa kitaifa wa rasilimali za maji unatekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi.

Aidha, Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa Wizara ya Maji kushirikiana na Wizara ya Fedha, kuhakikisha miradi yote ya maji inakamilika kwa wakati.

MABADILIKO YA TABIANCHI

Dk. Mwigulu alisema upungufu wa maji ni janga la dunia, kutokana na ukosefu wa mvua na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatambua kazi inayofanywa na viongozi, wataalamu wa serikali kukabiliana na changamoto hiyo.

Dk. Mwigulu alisema serikali iko macho muda wote kuhakikisha changamoto ya maji inapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Alieleza licha ya serikali kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la Mwalimu Nyerere wenye thamani ya zaidi ya sh. trilioni 6.5 kwa fedha za ndani, haikusitisha utekelezaji wa miradi mingine muhimu ya maji, umeme na umwagiliaji.

Alisema kukamilika Bwawa la Nyerere kumeondoa tatizo la mgawo wa umeme, huku miradi mingine ya kimkakati, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) na Daraja la Kigongo–Busisi ikitekelezwa kwa wakati.

Waziri Mkuu alisema kuchelewa mvua na kiwango kidogo cha mvua katika mwaka uliopita, imetoa funzo kwa taifa umuhimu kuwa na maandalizi ya muda mrefu.

Alimpongeza Rais Dk. Samia kutekeleza kwa kasi miradi ya maji iliyokwama muda mrefu ikiwemo ya Same, Mwanga, Butiama, Butimba, Simanjiro na Kidunda.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu alisema serikali imezingatia masuala ya afya, usalama na ubora wa kazi katika miradi yote inayoendelea.

WAZIRI AWESO

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema kutokana na mabadiliko tabianchi, uzalishaji maji katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ulipungua kutoka mita za ujazo 534,600 zilizozalishwa kwa siku hadi mita za ujazo 270,000 kwa siku ikiwa ni upungufu wa mita za ujazo 264,600 kwa siku.

Alisema wizara hiyo imepitia mtikisiko wa huduma ya maji kutokana na ukame uliosababisha uzalishaji kushuka, hata hivyo kupitia DAWASA hatua za dharura zilichukuliwa ikiwemo mgawanyo wa maji kwa usawa, kufungua visima vya chini ya ardhi na kushirikisha wadau wenye vyanzo binafsi.

Alieleza changamoto hiyo imedhihirisha athari ya mabadiliko ya tabianchi, ambapo Rais Dk. Samia alielekeza Wizara ya Maji kubadili mbinu kujikita katika miradi ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa mabwawa na matumizi ya maji ya chini ya ardhi.

Alisema serikali imetoa sh. bilioni 23.6 kwa mradi wa Kigamboni na kuanza ujenzi wa Bwawa la Kidunda, litakalohifadhi zaidi ya lita bilioni 190 za maji, wenye gharama ya sh. bilioni 336 na utekelezaji wake umefika asilimia 40.

RC PWANI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alisema mkoa huo ni wa kimkakati na una nafasi kubwa katika utekelezaji wa vipaumbele vya serikali.

Alisema maji ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vya Rais Dk. Samia na akisisitiza kuwa ni huduma ya kijamii, kiuchumi na uhai wa maendeleo.

Previous Post

JOSHUA APATA AJALI NIGERIA

Next Post

SIMBACHAWENE AZINDUA NAMBA YA KUFUATILIA NIDA

Next Post
SIMBACHAWENE AZINDUA NAMBA YA KUFUATILIA NIDA

SIMBACHAWENE AZINDUA NAMBA YA KUFUATILIA NIDA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU

DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU

3 weeks ago
DK. CHIMBI AFICHUA KIINI ONGEZEKO LA WAWEKEZAJI

DK. CHIMBI AFICHUA KIINI ONGEZEKO LA WAWEKEZAJI

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?