• ePaper
Sunday, March 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIKU YA HISTORIA MPYA TAIFA STARS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 30, 2025
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
SIKU YA HISTORIA MPYA TAIFA STARS
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

ILE siku ya Watanzania kuishuhudia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikiandika historia mpya katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inaweza kuwa leo kikosi hicho hicho kitakapochuana na Tunisia katika mchezo wa mwisho wa kundi C.

Taifa Stars itachuana na Tunisia kesho saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah uliopo Rabat, Morocco.

Katika mtanange huo wa aina yake, Taifa Stars itaingia na mambo mawili makubwa, kwanza kuandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika AFCON na pili kutinga hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza.

Katika kundi hilo, Taifa Stars ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja sawa na Uganda inayoburuta mkia, kinara Nigeria tayari imeshafuzu ikiwa na pointi sita wakati Tunisia ikifuatia kwa pointi tatu.

Ili kutinga hatua ya mtoano, Taifa Stars chini ya Kocha Miguel Gamondi, inapaswa kupata ushindi katika mtanange huo dhidi ya miamba hiyo kutoka Kaskazini mwa Afrika.

Akizungumzia mechi hiyo, Kocha Gamondi, alisema kikosi chake kipo tayari kuwania pointi tatu katika mtanange huo wa aina yake.

Gamondi alisema lengo la timu yake ni kuvuna pointi tatu na kuandika historia ya kutinga katika hatua ya 16 ya fainali hizo kubwa zaidi katika soka Afrika.

”Tupo tayari kupambana katika mechi yetu ya mwisho ya makundi dhidi ya Tunisia, tupo hapa  kulipambania taifa  la Tanzania na inawezekana kesho (leo) tukaandika historia ya kushinda na kufuzu raundi ya 16 bora.

“Kila mtu anaweza kuwa kocha baada ya mechi ila tuangalie uhalisia wa ubora wa viwango vyetu katika soka muda mwingine tunapaswa tu kuweka uhalisia, mimi naipenda kazi yangu na napambana kwa kadri ya uwezo wangu tuwe vizuri, ” alisema.

Kocha huyo aliongeza kuwa, wankwenda kucheza na Tunisia ambayo mechi yake ya mwisho ilifungwa hivyo utakuwa mchezo mgumu kutokana na kila moja kuhitaji ushindi.

Nyota wa Taifa Stars, Novatus Dismas, alisema wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanapata mabao na kuyalinda mabao ambayo watayapata katika mchezo dhidi ya Tunisia.

“Kuruhusu bao ni sehemu ya nyakati za mchezo tu, mechi ya leo tumejipanga kuhakikisha tunafunga bao lakini tunalinda isiwe kama michezo miwili iliyopita tukafanya makosa ya kuruhusu mabao mepesi,” alisema Dismas.

Kocha wa Tunisia, Sami Trabelsi alisema mechi hiyo ni muhimu kwao kwani malengo yao ni kuhitaji kufika hatua nyingine katika mashindano hayo.

“Tunafahamu umuhimu wa mechi dhidi ya Tanzania hivyo tuna matumaini tutashinda mchezo huo kwa kucheza vizuri, kwetu ni muhimu ni kama fainai ya kufuzu kwenda hatua nyingine, kiakili tumejiandaa na tumetumia muda mwingi kujiandaa,” alisema.

Katika michuano hiyo ya nne kwa Tanzania kushiriki, miamba hiyo haijawahi kushinda hata mechi moja kati ya mechi 11 ilizocheza katika AFCON, ikitoka sare mara nne na kufungwa mara saba.

Katika michuano ya mwaka 1980 iliyofanyika Nigeria, Taifa Stars ilipangwa kundi A na timu za Nigeria, Misri na Ivory Coast.

Taifa Stars iliburuta mkia kwa pointi moja baada ya kutoka sare na Ivory Coast. Awali, ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Nigeria na mabao 2-1 ilipovaana na Misri.

Katika AFCON mwaka 2019 zilizofanyika nchini Misri, Tanzania ilipangwa kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya.

Taifa Stars ilimaliza katika kundi hilo ikiwa nafasi ya nne baada ya kufungwa mechi zote tatu.

Kikosi hicho kilichokuwa kikinolewa na Amunike, kilianza kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Senegal, kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kenya na kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.

Pia, Taifa Stars iliburuta mkia katika hatua ya makundi ya AFCON mwaka 2023 zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Ikiwa imepangwa kundi F, Stars ilivuna pointi mbili (nyingi zaidi ya AFCON ilizoshiriki awali), ikianza kwa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Morocco, sare ya bao 1-1 kutoka kwa Zambia na suluhu dhidi ya DRC.

Mwaka huu, Tanzania ilianza kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Nigeria kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 kutoka kwa Uganda katika kundi C.

YAAHIDIWA MAMILIONI

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, alisema timu hiyo itapewa sh. milioni 200 kwa kila bao itakalofunga katika mtanange wa leo.

“Goli moja mtakalofunga ni sh. milioni 200, Watanzania wameniambia tunanunua goli moja katika mechi na Tunisia sh. milioni 200, Watanzania wanataka ushindi,” alisema.

Makonda ameitaka timu hiyo kujitoa kwa dhati kuhakikisha inafunga mabao mengi na kupata ushindi katika mtanange huo ili kujizolea mamilioni ya fedha na kuwapa furaha Watanzania.

Previous Post

TUME YAUNDWA KUBAINI TUHUMA UZIMAJI X -RAY

Next Post

TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

Next Post
TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

TAKWIMU ZAMBEBA MNIGERIA ALIYEKANDWA NA MWAKINYO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

RAIS DK. SAMIA: HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI

3 months ago
TUMEJIPANGA

TUMEJIPANGA

3 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI

    DK. MWIGULU AKERWA MICHANGO SHULENI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWALILIA WATUMISHI WALIOFARIKI AJALI YA BOTI KIGOMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA KIHONGOSI MWANZA YAREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • IBENGE FURAHA TELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?