• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

‘PENALTI’ STARS YAIGAWA DUNIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 6, 2026
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
‘PENALTI’ STARS YAIGAWA DUNIA
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

WAKATI timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikitolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco juzi, waamuzi wakongwe kutoka maeneo mbalimbali duniani, wametoa maoni tofauti kuhusu tukio la nyota Idd Nado kuanguka ndani ya boksi kama lilistahili adhabu ya penalti au siyo penalti.

Taifa Stars ilitolewa na mwenyeji Morocco katika hatua ya 16 bora ya AFCON 2025 kwa kichapo cha bao 1-0 katika mchezo ulipigwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat.

Katika mtanange huo uliokuwa wa aina yake, Stars ilionyesha kiwango cha juu dhidi ya miamba hiyo ya Afrika ambayo ilifunga bao lake pekee katika dakika ya 64 kupitia kwa Brahim Diaz.

Hata hivyo, dakika za nyongeza kipindi cha pili, Nado alianguka ndani ya boksi baada ya kuchuana na beki wa Morocco, Adam Masina ambaye picha mjongeo za marudio zilimwonyesha Mmorocco huyo akimsukuma Nado mgongoni kwa mkono wa kulia.

Hata hivyo, tukio hilo halikutafsiriwa kama faulo na kustahili adhabu ya penalti na mwamuzi wa kati raia wa Mali, Boubou Traore ambaye licha ya wachezaji wa Stars kumtaka akajiridhishe katika video (VAR), mwamuzi huyo hakwenda kuangalia huku akiamuru mpira uendelee.

Kwa mujibu wa Bodi ya Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (IFAB), sheria namba 12 ya soka kuhusu faulo na vitendo visivyo vya michezo, mwamuzi atakuwa na mamlaka ya kuamuru adhabu ya faulo ya moja kwa moja kama tukio limefanyika nje ya boksi au penalti ndani ya boksi, kama mchezaji atafanya makosa dhidi ya mpinzani ikiwemo kusukuma, kumrukia, kumzuia kwa mguu bila ya kucheza mpira, kumshambuliaji au kujaribu kumshambulia kwa miguu, mikono au kichwa.

Wakati IFAB inaeleza hivyo, baadhi ya waamuzi wakongwe wa soka duniani, wamesema tukio la Masina kumsukuma Nado lilistahili kuadhibiwa kama penalti wakati wengine wakidai halikustahili kuwa penalti.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, Katibu wa Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (FRAT), Salum Chama, alisema tukio la Nado kuangushwa ndani ya 18, lilistahili kuwa penalti kwa kuwa ni rafu iliyochezwa ndani ya eneo hilo.

Chama alisema mwamuzi Traore hakutafsiri vyema tukio hilo na kama angetafsiri kwa usahihi basi ni wazi angetoa adhabu ya penalti.

“Mwamuzi amefanya makosa makubwa, Stars ilitakiwa kupewa penati, haiwezekani ukawanyima watu haki yao ambayo walitakiwa kupatiwa.

“Laiti yule mwamuzi angekuwa yupo Tanzania binafsi ningemfuta katika orodha ya waamuzi maana amefanya kitendo cha aibu kabisa,” alisisitiza katibu huyo.

Katibu huyo aliongeza kuwa, mwamuzi alijipa majibu yake bila ya kuangalia VAR na kama angekwenda kuangalia anaamini angebadili uamuzi.

Hata hivyo, maoni ya Chama yalipingwa na aliyewahi kuwa mwamuzi wa soka nchini, Ezekiel Mwansasu, ambaye alidai kuwa mwamuzi Traore alikuwa sahihi kutoweka adhabu ya penalti katika tukio la Nado kwa kuwa haikuwa rafu.

Mwansasu alisema yapo baadhi ya matukio ambayo Traore alishindwa kutafsiri vyema, lakini katika tukio la Nado anaamini alikuwa sahihi.

Wakati zawawa hao wakitoa maoni hayo, baadhi ya waamuzi wakongwe kutoka nje ya nchi, wametoa kauli tofauti kuhusu tukio hilo.

Kupitia tovuti ya michezo ya winwin kutoka Qatar, mwamuzi mkongwe raia wa Misri, Gamal El-Ghandour ambaye aliwahi kuwa mwamuzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuanzia miaka ya 1990 hadi 2002 na kuamua baadhi ya mechi katika mashindano ya AFCON, Euro, Kombe la Mabara na Olympic, alisema  tukio la Nado na Masina lilistahili kuwa penalti.

“Kulikuwa na kusukumwa na kuvutwa dhidi ya straika wa Tanzania (Nado) katika dakika ya 90+4 ndani ya eneo la penalti, wakati ambao (Nado) alikuwa anamiliki mpira.

Mwamuzi hakutoa uamuzi wowote wala refa wa VAR hakusema chochote kwa mwamuzi wa kati.

Kwa uelewa wangu, ilikuwa adhabu ya penalti ambayo haikutolewa kwa Tanzania katika tukio hili, na namlaumu mwamuzi wa VAR zaidi ya mwamuzi wa kati,” alisema.

Hata hivyo, maoni hayo yalipigwa na Jamal Al-Sharif raia wa Syria ambaye amewa kuchezesha mechi mbalimbali zikiwemo Kombe la Dunia mwaka 1994 kati ya Mexico na Bulgaria.

Kwa mujibu wa tovu ya soka ya Foot Africa, mkongwe huyo amesema kuwa, tukio hilo halikupaswa kuwa penalti hivyo mwamuzi alikuwa sahihi.

Al-Sharif alidai kuwa, mgusano kati ya Masina na Nado ulikuwa wa asili na hivyo hakukuwa na kitendo cha wazi cha kuvuta au kusukuma ambacho kingehalalisha kuwa penalti.

Pia, mkongwe huyo alisisitiza kwamba, tukio hilo halikukidhi vigezo vya kuangaliwa katika VAR.

NDIMBO HUYU HAPA

Akizungumza kutoka Morocco, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema CAF ndiyo ina mamlaka ya kutathmini waamuzi kila baada ya mechi hivyo kama kuna jambo lolote sio sahihi wanaliachia shirikisho hilo.

“Mchezo umeonekana duniani kote, kama kuna jambo lolote kuhusu mwamuzi basi wenye mashindano (CAF) wanaweza wakaona nini wanaweza kukifanya,” alisema.

Previous Post

HOFU YA WANAUME KUOA WANAWAKE WAREMBO IKO HAPA

Next Post

RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

Next Post
RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

RAIS DK. SAMIA APOKEA TUZO TELE ZA UTALII

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

2 months ago
FIFA YADHAMIRIA KUWEKA NGUVU TANZANIA

FIFA YADHAMIRIA KUWEKA NGUVU TANZANIA

3 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?