• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA URUSHWAJI WA HELIKOPTA YA UTAFITI WA KINA WA MADINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 1, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MAVUNDE AZINDUA URUSHWAJI WA HELIKOPTA YA UTAFITI WA KINA WA MADINI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

IKIWA ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali kuhakikisha inafikia lengo la kuongeza eneo la utafiti kufikia asilimia 50 ifikapo 2030, Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) azindua urushwaji wa Helkopta iliyofungwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya utafiti wa madini nchini.

Amefanya uzinduzi huo leo tarehe 01 Februari, 2026 katika eneo la Buzwagi Wilayani Kahama kuashiria kuanza rasmi utafiti utakaofanywa na Kampuni ya Barrick kwa ajili ya uanzishwaji wa mgodi mpya.

“Kupitia Dira ya Madini 2030: Madini ni Maisha na Utajiri, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza kuhakikisha tunaongeza eneo la utafiti wa kina wa madini kupitia uwekezaji wa Serikali na Sekta binafsi”

“Tunachokifanya leo hapa ni kiashiria tosha kwamba maono hayo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yanakwenda kufikiwa ipasavyo. Tunaishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuamua kuunga mkono juhudi hizi za Serikali kwa vitendo” alieleza Mhe. Mavunde.

Waziri Mavunde pia amebainisha kwamba utafiti huo unaofanywa na Barrick unahusisha helkopta kuruka katika maeneo ya Msalala, Nzega, Igunga, Mbogwe na Nyangh’wale kwa lengo la kupata taarifa zitakazosaidia uanzishwaji wa mgodi mpya.

Kwa maeneo ambayo Barrick itafanya utafiti na kuona hayakidhi vigezo vya uchimbaji mkubwa, Mhe. Mavunde alielekeza kuwa maeneo hayo yatagawiwa kwa wachimbaji wadogo ili kuwaongoza na kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.

Awali, Meneja Mkazi wa Kampuni ya Barrick Tanzania, Dkt. Melkiory Ngido amesema kwamba tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania mwaka 2020, Kampuni imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 100 kwenye utafiti wa kina wa madini na kupitia migodi mitatu inayoiendesha imeweza kuleta nchini thamani ya zaidi ya trilioni 14 kwenye mzunguko wa uchumi wa ndani.

Akitoa Salaam za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh.Mboni Mhita aliishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini ambayo yamewezesha Kampuni ya Barrick kuendelea kufikiria kuongeza uwekezaji nchini.

Nao wabunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Mh. Benjamin Ngayiwa na  wa Jimbo Msalala, Mh. Mabula Magangila wameishukuru Serikali kwa namna inavyowezesha uwekezaji Wilayani Kahama na kueleza matarajio ya wananchi kuwa watakwenda kupata ajira na kuwainua kiuchumi kupitia miradi itakayokwenda kuanzishwa.

Previous Post

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

Next Post

TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

Next Post
TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

TANZANIA YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI NA UMOJA WA ULAYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MACHO YA MASHABIKI AFCON 2025 YAPO HAPA RABAT, MOROCCO

MACHO YA MASHABIKI AFCON 2025 YAPO HAPA RABAT, MOROCCO

4 months ago
NI HESHIMA YA TANZANIA

NI HESHIMA YA TANZANIA

4 days ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?