• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NSSF YAWANOA WAAJIRI, YASISITIZA UWASILISHAJI WA MICHANGO KWA WAKATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NSSF YAWANOA WAAJIRI, YASISITIZA UWASILISHAJI WA MICHANGO KWA WAKATI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewapa mafunzo waajiri 129 wa sekta binafsi, yakilenga kuwaongezea uelewa wa kina kuhusu utekelezaji sahihi wa sheria za hifadhi ya jamii pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kurahisisha huduma.

Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Meneja wa Uandikishaji, Ukaguzi na Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi, alisema ushirikiano kati ya Mfuko na Chama hicho umeendelea kuzaa matunda kwa kuwajengea uwezo waajiri katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Lengo letu ni kuhakikisha mwajiri anatekeleza sheria ya NSSF kwa uelewa, si kwa kulazimishwa. Ndiyo maana tunaendelea kutoa elimu ili wajue wajibu wao kikamilifu,” alisema Sasi.

Alieleza kuwa mafunzo hayo yalijikita katika masuala muhimu, ikiwemo usajili wa waajiri na wafanyakazi, pamoja na uwasilishaji wa michango kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa kisheria.

Sasi alisisitiza kuwa uwasilishaji wa michango kwa wakati ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata mafao yao bila vikwazo wanapoyahitaji.

Katika hatua nyingine, aliwahimiza waajiri kutumia kikamilifu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), akibainisha maboresho yaliyofanyika kwenye mfumo wa NSSF Portal unaowezesha utekelezaji wa huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Kupitia mfumo huo, waajiri wanaweza kujisajili, kusajili wafanyakazi, kuwasilisha michango, kufanya ukaguzi, pamoja na kuomba semina kwa ajili ya wafanyakazi wao.

“Tumeboresha mifumo yetu ili kumrahisishia mwajiri kutekeleza majukumu yake kwa haraka na kwa ufanisi zaidi,” aliongeza Sasi.

Aidha, waajiri walielimishwa kuhusu namna ya kufungua madai mtandaoni pamoja na wajibu wao wa kuhakiki taarifa za wafanyakazi wanaowasilisha madai hayo.

Pia, walipatiwa ufafanuzi kuhusu mfumo mpya wa uhakiki wa wastaafu unaofanyika kidijitali, hatua inayookoa muda na kurahisisha huduma.

Sasi aliwataka waajiri kuendelea kushirikiana na NSSF kwa kuhakikisha wafanyakazi wote wanasajiliwa na michango yao inawasilishwa kwa wakati.

Kwa upande wao, baadhi ya waajiri walieleza kuridhishwa na huduma za NSSF. Mariam Issa alisema Mfuko huo umekuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi, akitoa mfano wa mfanyakazi wao aliyenufaika na matibabu hadi akapona.

Naye, James Bidianguze aliipongeza NSSF kwa huduma bora, akibainisha kuwa mafao ya matibabu yanayotolewa na Mfuko yamekuwa mkombozi kwa wafanyakazi wengi wa sekta binafsi.

Mafunzo hayo yameongeza uelewa kwa waajiri na kuimarisha ushirikiano na NSSF katika kuhakikisha utekelezaji bora wa sheria za hifadhi ya jamii nchini.

Previous Post

WATANZANIA WAMKUMBUKA KWA KAZI KUBWA ALIYOIFANYA ENZI ZA UHAI WAKE

Next Post

GAMONDI AITA JESHI LA MAANGAMIZI, MANULA NDANI

Next Post
GAMONDI AITA JESHI LA MAANGAMIZI, MANULA NDANI

GAMONDI AITA JESHI LA MAANGAMIZI, MANULA NDANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU

YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU

2 weeks ago
AZAM FC KUANZA TIZI DESEMBA 23

AZAM FC KUANZA TIZI DESEMBA 23

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?