• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

GAVU AHIMIZA WANANCHI PERAMIHO KUENDELEA KUIUNGA MKONO CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 10, 2026
in Habari, Kitaifa
0
GAVU AHIMIZA WANANCHI PERAMIHO KUENDELEA KUIUNGA MKONO CCM
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na DUSTAN NDUNGURU, Songea

KATIBU wa NEC, Idara ya  organaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Issa Haji Gavu, amewataka wananchi wa Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, kujipanga kwa uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu, kwa kuendelea kukiunga mkono Chama kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Gavu amesema hayo alipozindua kampeni za ubunge wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo zilizofanyika Kata ya Magagula, wilayani Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.

Amesema kamwe wananchi wa jimbo hilo wasijaribishe kumchagua mbunge asiye sahihi, wakifanya hivyo watapoteza fursa muhimu, kwani mgombea anayetokana na CCM ndiye mtu sahihi kumchagua siku ya kupiga kura ikifika.

Katibu huyo aliwataka wananchi wa Peramiho wamchague Dk. Lazaro Komba,  aendeleze kazi nzuri iliyofsnywa na mtangulizi wake Jenista Mhagama aliyefariki dunia  Desemba 11, mwaka jana.

Kwa mujibu wa Gavu, wanachama wa CCM wanapaswa kuendelea kueneza mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, umeme, kilimo na mifugo, kumwezesha mgombea wa CCM kupita kwa urahisi katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa, CCM imejipanga kuendelea kuleta maendeleo katika sekta zote na imekuwa ikigusa maendeleo kwa Watanzania bila kubagua, hivyo kumchagua Dk. Komba ni kuchagua maendeleo.

“ CCM haitashinda katika uchaguzi huo kwa sababu ya mabavu bali itashinda kwa sababu ya umoja na mshikamano uliopo ndani ya Chama, sanjari na utekelezaji wa yale ambayo imekuwa ikiahidi wakati wa kampeni za uchaguzi,”alisema.

Alisema CCM inaamini wakati wote kuwa, suala la amani ni muhimu katika nchi na ndiyo maana Chama na serikali kimeendelea kusimamia, kikitambua bila ya amani hakuna shughuli za maendeleo ambazo zinafanyika katika nchi.

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Dk. Komba alisema hana shaka na ushindi wa Chama kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM  chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Dk. Komba alisema akichaguliwa kuongoza jimbo hilo atahakikisha anasimamia kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kushirikiana na madiwani, watendaji na wananchi,  maendeleo yanayokusudiwa yaonekane  hilo ndilo lengo la Chama na serikali.

Aliwaomba wananchi wa jimbo kujitokeza kwa wingi Februari 26, mwaka huu, kukipigia kura Chama,  ndicho Chama pekee nchini chenye nia ya dhati ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.

Previous Post

MAELEKEZO YA RAIS DK. SAMIA YATEKELEZWA KARIAKOO

Next Post

DK. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027

Next Post
DK. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027

DK. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

10 months ago
NI SAFARI YA MABILIONI YA FEDHA AFCON 2025

NI SAFARI YA MABILIONI YA FEDHA AFCON 2025

7 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?