• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 15, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
CHINA YAENDELEZA UHUSIANO, USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KWA BARA LA AFRIKA
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Hamis Shimye

USHIRIKIANO wa kidiplomasia kati ya China na nchi za Afrika umeendelea kuwa wa kindugu, kihistoria na wenye malengo ya kimkakati kunufaisha pande zote mbili kupitia sekta mbalimbali.

Rais wa China, Xi Jinping akiielezea Afrika anasema ni “ndugu na mshirika wa kimkakati.” Kupitia hotuba mbalimbali amekuwa akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kihistoria kati ya China na bara hili.

Pia, amekuwa akielezea mwelekeo wa ushirikiano huo katika miaka ijayo ambapo amekuwa akionyesha uhusiano wa China na Afrika una mizizi ya kihistoria, pande mbili hizo zinaunganishwa na uzoefu wa pamoja katika kupigania uhuru na maendeleo. 

Rais Xi alisema China na Afrika ni “ndugu wa kweli,” wakikumbatia maadili ya usawa, haki, na ushirikiano huku akisistiza pamoja na maendeleo ya haraka ya China, nchi za Afrika zimekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya dunia, na taifa lake linatambua mchango wa bara hilo katika jukwaa la kimataifa.

USHIRIKIANO WA KIUCHUMI, MAENDELEO ENDELEVU

Rais Xi Jinping anauelezea uhusiano wa China na Afrika, ni ushirikiano wa kiuchumi unaotokana na malengo ya pamoja ya maendeleo. 

China inataka kutoa msaada wa kiuchumi kwa Afrika, kwa kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi.

Aliongeza “China itakuwa mstari wa mbele kusaidia Afrika kuboresha miundombinu, kukuza viwanda, na kuongeza nafasi za ajira kupitia miradi ya maendeleo.”

Katika mkutano wa kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), Rais Xi alieleza dhamira ya nchi yake kuimarisha miundombinu ya Afrika kupitia uwekezaji mkubwa katika miradi ya barabara, reli, viwanja vya ndege, na mitambo ya nishati.

Alisema China inajitahidi kuisaidia Afrika kuwa na miundombinu ya kisasa kutimiza malengo ya ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030.

MISAADA, MIKOPO

Rais Xi alipokuwa akizungumza na viongozi wa Afrika, alisisitiza China itaendelea kutoa misaada na mikopo nafuu kwa nchi za Afrika kuziwezesha kuendeleza miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, alisema misaada hiyo itakuwa sehemu ya ushirikiano wa kiuchumi, na kwamba China haitaki kuwa na uhusiano wa kihafidhina, bali inahimiza ufanisi wa pamoja.

Alisema umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya utamaduni na elimu kati ya pande mbili hizo umekuwa na tija kubwa.

Aliweka wazi kwamba, China itazidi kusaidia kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni kwa kuongeza ubadilishanaji wa vijana, wanafunzi na wataalamu kati yake na Afrika. 

Kwa mujibu wa Rais Xi, kupitia elimu, Bara la Afrika linaweza kupata ujuzi wa kitaalamu utakaowezesha kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Rais Xi Jinping alisema China na Afrika wanapaswa kushirikiana kutatua changamoto zinazoikumba dunia yakiwamo mabadiliko ya tabianchi, migogoro ya kisiasa, na changamoto za afya. 

Hivyo, China inajiunga na Afrika kutatua changamoto hizo kwa kutoa msaada wa kiufundi, fedha, na maarifa.

Aidha, alielezea ushirikiano wa China na Afrika katika masuala ya kimataifa ambapo taifa hilo litaendelea kuiunga mkono Afrika kupigania haki zake katika majukwaa ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN), huku akisisitiza nchi yake kuisaidia Afrika kupata nafasi inayostahili katika utawala wa kimataifa.

Kwa miongo miwili iliyopita, uhusiano kati ya China na Afrika umebadilika kwa kiasi kikubwa, sasa nchi hiyo imejitokeza kuwa mmoja wa washirika wakuu wa kibiashara na kiuchumi kwa bara hilo. 

Uwekezaji wa China katika sekta mbalimbali, hususani miundombinu, biashara, na maendeleo, umeleta tija na mabadiliko makubwa kwa nchi nyingi za Afrika.

TANZANIA YAZIDI KUNUFAIKA

Katika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi aliyoifanya nchini Januari, mwaka huu, alisema nchi hiyo limeweka wazi msimamo wake kuhusu uhusiano mkubwa baina yake na Tanzania kuwa wa kindugu na wa kihistoria.

Alisema serikali ya China ipo tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za maendeleo, huku akiahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Waziri Wang alisema Tanzania na China zina ushirikiano wa kimkakati uliopita kiwango cha nchi mbili, na sasa unaendana na mwelekeo wa kihistoria wa kuinuka kwa mataifa ya Kusini mwa Dunia (Global South).

Alisema utekelezaji wa miradi mikubwa, ukiwemo wa kufufua Reli ya TAZARA, ambayo karibuni kulishuhudiwa uwekaji wa jiwe la msingi la ukarabati wake wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.4 kuongeza ufanisi wa usafirishaji.

“China ina dhamira ya dhati na Tanzania katika kuendeleza ushirikiano” alisema.

Aliongeza kuwa “China imedhamiria kusimama kidete kufanya utekelezaji wa maelekezo mbalimbali na kutekeleza miradi ya kimkakati Tanzania.”

Wang Yi aliendelea kusema kuwa “China inaunga mkono juhudi za Tanzania kulinda mamlaka yake, usalama, na maslahi ya maendeleo.”

Kwa mujibu wa Wang, China itaendelea kuwa mshirika wa kuaminika wa Tanzania na Afrika nzima kutekeleza ajenda za maendeleo ya pamoja na kuhakikisha uhusiano uliopo unadumu zaidi.

Alisema kuwa “utayari huo utadhihirika zaidi kupitia miradi ya maendeleo iliyo chini ya Mpango wa Ukanda na Njia (Belt and Road Initiative) na Jukwaa la FOCAC, ambayo yamekuwa nguzo muhimu kukuza uchumi na miundombinu.”

WAZIRI KOMBO

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru serikali ya China kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania, hususani utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya miundombinu, afya, elimu, nishati na viwanda.

Alisema “Tanzania imedhamiria kuendelea kushirikiana na China kuvutia uwekezaji, biashara na teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.”

HISTORIA YA USHIRIKIANO

Historia ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania ni wa muda mrefu, ukiwa umedumu kwa zaidi ya miongo sita ukijikita katika msingi wa urafiki wa hali na mali.

China ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanganyika (Tanzania Bara) Desemba 9, 1961, na baadaye na Zanzibar Desemba 11, 1963.

Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, China iliutambua muungano huo na kuendeleza uhusiano na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa muda wote waasisi wa ushirikiano huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong na aliyekuwa Waziri Mkuu wa China, Zhou Enlai walisimama imara.

Februari mwaka 1965, Mwalimu Nyerere alifanya ziara ya kwanza nchini China na kupitia ziara hiyo, nchi hizo zilitia saini mkataba wa urafiki, ambao ulikuwa wa kwanza kwa China kusaini na nchi ya Mashariki au Kusini mwa Afrika.

1971, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuiunga mkono China kurejesha kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa (UN) na Baraza la Usalama, ikichukua nafasi ya Taiwan.

Reli ya TAZARA ni alama ya uhusiano wa kudumu baina ya China na Tanzania ikiwa na historia kubwa ambapo wakati nchi za Magharibi zikikataa kufadhili mradi huo unaoziunganisha Tanzania na Zambia, nchi hiyo ilisimama kidete kuijenga.

China ilikubali kutoa mkopo usio na riba na wataalamu kujenga TAZARA yenye kilometa 1,860 kati ya mwaka 1970 na 1975. Huu unabaki kuwa mradi mkubwa zaidi wa miundombinu uliowahi kufanywa na China barani Afrika kwa wakati huo.

Ziara ya Rais wa China, Xi Jinping nchini mwaka 2013, ilikuza ushirikiano wa mataifa hayo na kuufanya kuwa wa kisiasa na kimkakati.

Rais Xi alitumia ziara hiyo kutangaza sera ya China kuhusu Afrika.

Aidha, Rais Samia pia alifanya ziara nchini China, Novemba mwaka 2022, uhusiano ulipandishwa hadhi na kuwa ‘Ushirikiano wa Kimkakati’.

Katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania mwaka 2024, nchi hizo zilitia saini mikataba mipya ya kibiashara na kuanzisha miradi ya ukarabati wa reli ya TAZARA.

China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Tanzania na chanzo kikuu cha uwekezaji wa moja kwa moja (FDI), huku Tanzania ikisalia kuwa lango kuu la China katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Hivyo, ushirikiano wa Tanzania na China umekuwa na mafanikio makubwa tangu ulipoasisiwa kwa nia ya kuendeleza gurudumu la maendeleo na umeonyesha tafsiri sahihi ya undugu baina ya nchi hizo.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATAJA FAIDA ZA MPANGO WA NISHATI

Next Post

TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

Next Post
TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

TRA IMEANZA KUTEKELEZA  MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KARATU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

1 month ago
MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

17 hours ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?