• ePaper
Wednesday, June 24, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SABABU ‘DABI’ YANGA, SIMBA KUPELEKWA Z’BAR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 19, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SABABU ‘DABI’ YANGA, SIMBA KUPELEKWA Z’BAR
0
SHARES
21
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imesema sababu ya kuupeleka mchezo wa ‘Dabi ya Kariakoo’ visiwani Zanzibar ni kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa na matumizi mengine.

Yanga itakuwa wenyeji wa mchezo huo unaotarajiwa kufanyika Machi Mosi, mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan, visiwani Zanzibar kuanzia saa 2:15, usiku.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda alisema walipokea taarifa ya ombi la kuuhamisha mchezo huo kutoka Yanga na tayari walishawajibu.

Alisema wamekubali mchezo huo utafanyikia Uwanja wa New Amaan Complex, kwani unakidhi vigezo vya kanuni za soka, kutumika katika mechi mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tuliandikiwa barua na Yanga kwenda kucheza mechi yao na Simba visiwani Zanzibar katika uwanja wa New Amaan Complex.

“Klabu inaruhusiwa kikanuni kuchagua uwanja mwingine kwenda kuchezea mechi zake kama uwanja wa awali unaweza kuwa na changamoto.

“Tumekubali mchezo ukafanyikie Zanzibar kwani uwanja unakidhi vigezo na Yanga wanaruhusiwa kikanuni kuhamisha mchezo kwenda sehemu nyingine.

“Tumejiridhishwa na uwanja kwani ule wa awali ambao ulitakiwa kutumika, utakuwa na shughuli nyingine,” alisema Boimanda.

Timu hizo, zilipambana Septemba16, mwaka jana ambapo Yanga iliichapa Simba 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Bao la Yanga lilifungwa dakika ya 54 na  Pacome Zouzoua aliwainua mashabiki katika viti baada ya kufunga bao la kuongoza kwa shuti kali akiwa ndani ya eneo la hatari.

Pacome alifunga bao hilo kufuatia kupokea mpira  kutoka kwa Maxi Nzengeli.

Previous Post

KIHONGOSI AANIKA UIMARA WA CCM KWA WATANZANIA

Next Post

CARDINAL PENGO AFARIKI DUNIA

Next Post
CARDINAL PENGO AFARIKI DUNIA

CARDINAL PENGO AFARIKI DUNIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

6 months ago
DK. MWIGULU ATANGAZA AHUENI WAFANYABIASHARA SIMU 2000

DK. MWIGULU ATANGAZA AHUENI WAFANYABIASHARA SIMU 2000

3 months ago

Popular News

  • YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATUTAVUMILIA UHUJUMU WA MIRADI – NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA KUZINDUA JENGO LA BILIONI 17/- KCMC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BODABODA WAKINGIWA KIFUA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?