• ePaper
Sunday, May 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WILLIUM PAUL, Same 

MAKAMU wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, amesema suala la utalii mahali popote duniani linaendana na amani na utulivu.

Amewasihi wananchi kuhakikisha wanalinda amani kukuza utalii nchini na kuendelea kunufaika kupitia sekta hiyo.

Malecela alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa Tamasha la Same Utalii, lililofanyika kwenye viwanja vya Stendi wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa, baadhi ya nchi duniani zinaendeshwa kwa fedha za utalii, hivyo kuwataka wananchi kuitazama sekta hiyo kama fursa ya kukumbatia.

Kiongozi huyo alisema misingi ya utalii ni ukarimu kwa wageni na kuwataka wananchi wa Same kuwa mfano kwa ukarimu, kukuza utalii wilayani humo.

“Hata sehemu kukiwa na njiwa 10,000 wamejaa lakini jiwe likigonga tu wote wanakimbia, kwa hiyo na sisi utalii wetu uanze na sisi wenyewe Watanzania kuwa na amani, ni jambo la msingi. Amani ndio italeta na kuwakaribisha watalii na ndio itatufanya tuendelee kukua kiuchumi,” alisisitiza. 

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Nkoba Mabula, alisema wizara hiyo inaunga mkono juhudi za Same kutangaza utalii na kwamba itaendelea kutoa ushirikiano kuendelea kuukuza.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, alisema wilaya yake imejaliwa vivutio vingi vya asili na kihistoria vinavyoweza kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi na kwamba, lengo kuu la kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kuhifadhi maliasili zilizopo.

Pia, kutangaza na kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani humo kuchochea maendeleo ya kiuchumi. 

VIVUTIO

Alitaja baadhi ya vivutio hivyo ni Mlima Shengena, Kilele cha Mlima Kidenge, Maporomoko ya maji ya Thomthorn (Water Falls), Ziwa Ranzi na maeneo ya kihistoria kama majabali ya Mkumbavana na Makemane. 

Previous Post

DK. NCHIMBI: NYERERE MFANO WA UADILIFU

Next Post

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

Next Post
UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

SIMBA, NSINGIZINI BALAA ZITO CAFCL

7 months ago
DK. SAMIA AWAPA FARAJA WENYE MAHITAJI MAALUMU

DK. SAMIA AWAPA FARAJA WENYE MAHITAJI MAALUMU

7 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?