• ePaper
Saturday, May 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. NCHIMBI: NYERERE MFANO WA UADILIFU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 12, 2026
in Habari, Kitaifa
0
DK. NCHIMBI: NYERERE MFANO WA UADILIFU
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW, Dodoma

MAKAMU wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa vijana kulinda amani na kukataa vishawishi vitakavyolitumbukiza taifa katika vitendo vya ubadhirifu; huku akimtaja Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa kielelezo cha uadilifu.

Amesema kufanya hivyo ni kuenzi misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Dk. Nchimbi aliyasema hayo jijini Dodoma alipozungumza katika kongamano la vijana kuhusu Mwalimu Nyerere, lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Makamu wa Rais alisema Nyerere alitamani nchi iongozwe na mtu mkweli, mwadilifu na aliye tayari kutumia nguvu na akili zake, akibainisha kwamba alikuwa akitafuta kiongozi mwenye sifa hizo kwa vitendo.

Aliongeza kuwa licha ya kuwa Rais wa nchi, Mwalimu Nyerere aliishi maisha ya kawaida bila ubadhirifu wala anasa, jambo lililomfanya kuwa mfano wa uongozi wa kuigwa hadi leo.

“Alikuwa Rais wa nchi, lakini aliishi maisha ya kawaida, hakukuwa na ubadhirifu wa mali za umma na hata leo watu wakisikia kuna changamoto katika familia yake, viongozi wa sasa wanaguswa kwa sababu wanajua hakutumia nafasi yake kwa maslahi binafsi bali kwa maslahi ya taifa,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Nchimbi, Nyerere alitamani kuona mali ya taifa inalindwa na kubaki kuwa ya Watanzania wote, akionya kuwa matumizi mabaya ya madaraka ni kinyume cha misingi hiyo.

Aidha, alisema kosa kubwa ambalo baadhi ya viongozi hufanya ni kutumia vibaya imani wanayopewa na wananchi, badala ya kuitumia kwa manufaa ya umma.

“Ukipewa dhamana ya uongozi, wananchi wanatarajia uitumie kwa maslahi yao, sio kwa maslahi binafsi,” alisisitiza.

Mbali na hilo, Dk. Nchimbi alibainisha kuwa Baba wa Taifa alikuwa kiongozi wa kipekee aliyesisitiza elimu kwa wote, haki na utu wa binadamu, hali iliyochangia pia Tanzania kuwa mstari wa mbele kusaidia ukombozi wa bara la Afrika.

Alisema hakuna nchi barani Afrika iliyopata uhuru bila kuguswa na mchango wa Nyerere, iwe kwa maneno, rasilimali au msaada wa kifedha.

MSHIKAMANO WA KITAIFA

Nchimbi aliongeza kuwa, Mwalimu Nyerere alijenga taifa lenye mshikamano licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120, hivyo aliondoa mipasuko ya kidini na kikabila.

“Alijenga misingi imara ya amani na umoja. Tukiharibu tulichojengewa, tutakuwa tunajiharibia wenyewe,” alionya.

Dk. Nchimbi alionya kuwa, vitendo vya ubaguzi wa kidini, kikabila au kukosekana kwa usawa vinaweza kusababisha mipasuko katika jamii na kuhatarisha mshikamano wa taifa.

Akihitimisha, aliwataka vijana kujiuliza maswali muhimu kuhusu hatma ya taifa, ikiwemo kama wako tayari kulinda amani, kukataa rushwa na kutumia elimu waliyonayo kwa maendeleo ya nchi badala ya maslahi binafsi.

PINDA

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, aliwataka vijana kutokata tamaa na kujifunza kutoka kwa viongozi waliotangulia kwa kuiga mema yao.

Pinda alisema taasisi hiyo inalenga kukuza kizazi cha viongozi waadilifu watakaotumikia wananchi badala ya kujinufaisha binafsi.

“Kiongozi bora ni yule anayetumikia watu, sio tumbo lake,” alisema.

MAHAKAMA

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Profesa Elisante Ole Gabriel, aliwataka vijana kubadilika kifikra na kuzigeuza changamoto kuwa fursa.

Ole Gabriel aliwahimiza kufanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi, akisisitiza uzembe wa leo unaweza kuwaathiri watakapokuwa wazee.

Aidha, aliwataka vijana kutumia fursa zilizopo ikiwemo mikopo ya maendeleo ya vijana na miundombinu iliyowekwa na serikali kuwawezesha kujiajiri.

Previous Post

RAIS MSTAAFU MALAWI AWAUSIA WATAZANIA

Next Post

MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

Next Post
MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

MZEE MALECELA ASEMA  HAKUNA UTALII BILA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

8 months ago
SINGIDA BS YAIPANIA SIMBA

SINGIDA BS YAIPANIA SIMBA

3 months ago

Popular News

  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?