• ePaper
Sunday, April 5, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

– NI salamu za Rais Dk. Samia kwa Waislamu na Watanzania, mgeni rasmi Baraza la Eid leo.

REHEMA MAIGALA NA SIMON NYALOBI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewatakia Waislamu na Watanzania wote sikukuu njema na kuwahimiza kuyaishi na kuyaendeleza mema waliyojifunza mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kupitia taarifa yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika: “Tuyaishi na kuyaendeleza mema yote tuliyojifunza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, upendo, huruma na kusaidiana kuimarisha maadili na mshikamano katika jamii zetu.

“Tusherehekee kwa utulivu, tukidumisha umoja na kulinda amani ya nchi yetu, kwa kuwa amani ndiyo msingi wa ustawi wa maendeleo ya taifa letu.”

MGENI RASMI BARAZA LA EID LEO

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyotiwa saini na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi, Rais Dk. Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Eid litakalofanyika leo jioni katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Baraza hilo litafanyika baada ya swala ya Eid itakayofanyika Msikiti wa Mfalme Mohamed V1 uliopo Kinondoni.

SHEIKH MATAKA

Akizungumza na UHURU, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA, Sheikh Hamisi Mataka aliwaomba Waislamu kusheherekea sikukuu ya Eid kwa amani, utulivu, mshikamano na umoja.

Alisema Tanzania ni nchi ya amani, hivyo jamii inatakiwa kulinda amani kwa lengo la kurithisha vizazi vijavyo.

Sheikh Mataka alisema kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, waislamu walifunga pamoja na kuwasaidia watu wasiojiweza.

“Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fundisho linalotutaka Waislamu kuwa na subira kwa kila jambo, hivyo tuendelee kuitunza amani ya nchi yetu,”alisema.

Alisema amani inamsaidia kila Mtanzania kufanya mambo ya maendeleo na hata kusherehekea sikukuu kwa utulivu.

DUA MAALUMU

Aidha, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Baraza la Kiislamu la Madrasatu-l- Qamariyyati-I-Islaamiyyah, Alhaji Sheikh Rajabu Mtuguta, aliwasisitiza waumini wa dini ya Kiislamu kusherehekea Eid kwa utulivu na kuepuka kufanya mambo maovu.

Sheikh Mtuguta alieleza hayo jana baada ya dua maalumu ya kumaliza mfungo wa Ramadhani na kuwaombea viongozi wakuu wa nchi, iliyofanyika Msikiti wa Kheri ulioko Shimo la Udongo, Kata ya Kurasini, Temeke, Dar es Salaam.

Alisema waumini hao wanapaswa kuonesha matendo mema ambayo waliyatenda kipindi cha Ramadhani.

“Nawaomba waumini wenzangu tuendeleze tabia njema katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri, baadhi ya waumini wakati wa mfungo wa Ramadhan wanakuwa watu wema na ukiisha wanarejea kufanya maasi, kitu ambacho hakikubaliki,” alisema.

Aliongeza: “Huwezi kusherehekea kwa kulewa au kufanya utovu wa nidhamu kwa kisingizio cha sikukuu.”

Sheikh Mtuguta ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA), Wilaya ya Kinondoni, alisema waumini hao wanapaswa kuwaombea viongozi wakuu akiwemo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Tujenge tabia ya kuwaombea viongozi wetu na amani ya taifa letu, sisi baraza tulifanya dua ya kuwaombea Rais Dk. Samia, Makamu wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, wapate afya njema na kuongoza taifa kwa uadilifu,”alisema.

Alisisitiza jamii kudumisha amani na umoja na kuvumiliana katika maisha ya kila siku taifa liendelee kuwa na amani na utulivu.

MWANZA

Naye, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, aliwataka waislamu mkoani humo kuendeleza mema waliyoyafanya mwezi wa Ramadhani.

“Nawaomba waislamu tuendeleze umoja nchini, kwa lengo la kujenga utulivu tuliouzoea,”alisema Sheikh Kabeke.

Hata hivyo, aliwasihi waislamu mkoani Mwanza kuhudhuria kwa wingi Baraza la Eid litakalofanyika Nyamagana baada ya swala ya eid, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.

“Baraza la Eid litafanyika asubuhi kwa sababu ya kuwapa nafasi waislamu wamsikilize kwa makini Rais Dk. Samia ambaye leo atakuwa mgeni rasmi katika baraza la eid la kitaifa jijini Dar es Salaam,” alisema.

POLISI KANDA MAALUMU

Kwa upande mwingine, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limesema hali ya usalama itakuwa shwari katika kipindi chote cha sikukuu ya eid.

“Tutahakikisha usalama wa hali ya juu kwa raia wetu katika kipindi chote cha sikukuu wakisherehekea bila ya kuwa na changamoto yoyote,”alisema Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro.

Aliongeza katika kuhakikisha amani na utulivu vinatawala, polisi watakuwa wakifanya doria sehemu mbalimbali za mkoa huo.

Previous Post

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

Next Post

DK. MWINYI: MEMA YA MFUNGO WA RAMADHANI YAENDELEZWE

Next Post
DK. MWINYI: MEMA YA MFUNGO WA RAMADHANI YAENDELEZWE

DK. MWINYI: MEMA YA MFUNGO WA RAMADHANI YAENDELEZWE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KOCHA SIMBA AIPANIA MASHUJAA

KOCHA SIMBA AIPANIA MASHUJAA

2 months ago
DK. MWINYI ACHUKUA FOMU ZANZIBAR, AHADHARISHA CHUKI

DK. MWINYI ACHUKUA FOMU ZANZIBAR, AHADHARISHA CHUKI

7 months ago

Popular News

  • CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    CHAMUDATA YAZUNGUMZIA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIONGOZI WA DINI WAHUBIRI AMANI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?