• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 27, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemshushia ‘rungu’ kipa wa Yanga, Djigui Diarra, kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu aliyoyaonesha katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyofanyikia Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Hbari wa TPLB, Karim Boimanda, Diarra amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya sh. milioni mbili kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati wa mchezo huo, Gilbert Mrina mara baada ya kumalizika.

“Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

“Lakini pia Diarra ametozwa faini ya sh. milioni mbili kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

“Diarra ametenda kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji, kwa sababu kitendo hicho kinaashiria matusi na dharau,” alisema Boimanda.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema mwamuzi wa kati wa mchezo huo Mrina kutoka Kilimanjaro, ameshushwa daraja la uamuzi kwa kosa la kushindwa kuchukua hatua stahili kwa mchezaji Diarra kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu (kumshambulia mwamuzi) kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 42:1(1.6) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Taarifa hiyo ilieleza adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kuwa ni kosa la kujirudia ambapo mwamuzi Mrina alitenda kosa la aina hiyo katika mchezo namba 65 wa Ligi Kuu kati ya Mbeya City vs Namungo na akaadhibiwa kwa kufungiwa mizunguko mitatu.

Wakati huo huo, TPLB imetoa adhabu kwa klabu ya Simba kwa kuitoza faini ya sh. milioni 10 kufuatia utovu wa nidhamu wa mashabiki wake.

Adhabu hiyo imetokana na tukio la mashabiki wa Simba kuwarushia chupa za maji waamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Pamba Jiji, uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kosa hilo la pili kwa Simba ndani ya miezi miwili kwa mashabiki wake kufanya hivyo, baada ya tukio kama hilo kutokea Februari 25 dhidi ya Dodoma Jiji na adhabu hiyo imetolewa chini ya Kanuni ya 47:1 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Previous Post

CHANJO YA POLIO MUHIMU KUNUSURU WATOTO KUPOOZA 

Next Post

KOCHA GAMONDI AWAANGUKIA MASHABIKI

Next Post
KOCHA GAMONDI AWAANGUKIA MASHABIKI

KOCHA GAMONDI AWAANGUKIA MASHABIKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MWIGULU ACHARUKA

MWIGULU ACHARUKA

4 months ago
PEDRO RAHA TUPU YANGA

PEDRO RAHA TUPU YANGA

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?