• ePaper
Saturday, May 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PROFESA CHIJORIGA ACHAMBUA AMANI INAVYOLETA MAENDELEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 2, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PROFESA CHIJORIGA ACHAMBUA AMANI INAVYOLETA MAENDELEO
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SIMON NYALOBI

MKUU  wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu  Julius Nyerere(MJNLS), iliyopo wilayani Kibaha,  Mkoa wa Pwani, Profesa Marcellina  Chijoriga, amesema amani ni tunu inayopaswa kuenziwa na Watanzania wote kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo.

Profesa Chijoriga, alisema hayo, alipozungumza na UHURU na kwamba wananchi wanapaswa kulifahamu hilo katika maisha yao ya kila siku.

“Ukiwa na amani mambo mengi yanawezekana na bila ya amani hakuna maendeleo, tukumbuke amani inaanzia kwa mtu binafsi, jamii na baadaye kwa taifa kwa ujumla.

“Hivi sasa hapa nchini tuna miradi mikubwa ya maendeleo ya kitaifa, iwe katika barabara, maji na umeme, miradi yote hii inafanyika kwa sababu nchi ina amani, sasa ukienda katika nchi zenye vita huwezi kukuta miradi ya maendeleo inafanyika,”alisema.

KUENDELEZA AMANI

Akizungumzia mambo yanayoweza kuimarisha na kuendeleza amani, aliweka wazi kuwa ni muhimu kuwepo kwa umoja na mshikamano ndani ya taifa.

“Ili  amani iwepo ni lazima umoja na mshikamano utamalaki, kusiwe na chokochoko za kuleta mifarakano na hata Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alisisitiza taifa liwe na umoja na mimi naongeza la kwangu upendo lazima uwepo,”alisema.

Profesa Chijoriga alisema tofauti za watu katika itikadi za vyama vya siasa au dini au tofauti za makabila hazina shida, lakini itikadi hizo zitakuwa na shida iwapo itikadi hizo zitakuwa zinachochea kutokea kwa mifarakano ndani ya jamii.

Alisisitiza mitizamo ya kisiasa isifanye watu wafarakane na kuvunja amani na umoja wa kitaifa, kwa kuwa nchi imejengwa katika misingi ya amani na umoja.

Profesa Chijoriga alisema viongozi wanaohubiri chuki na mifarakano hawafai na dhamira zao zisipewe nafasi katika taifa; kwa kuwa zitavunja amani na utulivu uliopo.

“Watanzania tuogope mifarakano ya aina yoyote inayotugawa katika umoja wetu, tumeshajengewa misingi mizuri na waasisi wetu; kwa mfano mimi ni mwenyeji wa Songea lakini niliolewa na mtu wa Musoma, hii ni tofauti na mataifa mengine watu wanaulizana makabila ndipo waamue waoane,”alisema.

Profesa Chijoriga alikumbusha msingi wa amani na umoja wa taifa wa nchi ulijengwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ambao uliwaunganisha wananchi wote na matumizi ya Lugha adhimu ya Kiswahili.

Kuhusu namna raia wa kigeni wanavyoichukulia amani na umoja uliopo nchini, alisema raia hao hususan wanaokwenda kusoma katika Shule ya MJNLS  wanastaajabu fahari ya amani iliyopo nchini.

“Wageni wanaosoma katika shule yetu wanashangaa amani iliyopo na maendeleo tuliofikia, wageni hao ni wale waliotoka katika vyama vilivyopigania ukombozi wa Kusini mwa Bara la Afrika.

“Wanashangaa namna tunavyoendesha mambo yetu katika kuleta amani kupitia tume tunazounda wenyewe ikiwemo,  Tume ya Uchunguzi kuhusu matukio ya machafuko wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025,” alisema.

Aliweka wazi kuwa, wanashanga kuona jitihada zinazofanywa na serikali katika kuleta utulivu na amani nchini ni tofauti na nchi zao.

Profesa Chijoriga akizungumzia kutokuwepo kwa ubaguzi katika masuala ya maendeleo ya umma hususan usafiri wa umma, alisema raia hao wa kigeni wanashangazwa na maendeleo yanayoletwa na serikali yanayogusa kila raia wa nchi.

Alifafanua, raia hao wa kigeni wamekuwa wakishangaa namna raia yeyote kutumia usafiri wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na usafiri wa treni inayotumia Reli ya Kisasa(SGR) bila ya ubaguzi.

Kwa mujibu wa Profesa Chijoriga, kushangaa kwao huko kunatokana na baadhi ya nchi zao ambako usafiri wa aina hiyo unafanyika kwa matabaka, kwani si kila mtu anayeweza kufurahia huduma ya usafiri wa aina hiyo.

Previous Post

DK. MWIGULU ASHUSHA MAAGIZO YA KAZI NA UTU

Next Post

RAIS DK. SAMIA AUNGWA MKONO ULINZI WA RASILIMALI ZA NCHI 

Next Post
RAIS DK. SAMIA AUNGWA MKONO ULINZI WA RASILIMALI ZA NCHI 

RAIS DK. SAMIA AUNGWA MKONO ULINZI WA RASILIMALI ZA NCHI 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

1 month ago
WITO WA DK. NCHIMBI KWA VIONGOZI WA DINI

WITO WA DK. NCHIMBI KWA VIONGOZI WA DINI

8 months ago

Popular News

  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?