• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

HAKUNA ALIYEPOTEZA NYETI-WAZIRI KATAMBI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 7, 2026
in Habari, Kitaifa
0
HAKUNA ALIYEPOTEZA NYETI-WAZIRI KATAMBI
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, amelitaka Jeshi la Polisi nchini, kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaodai kupotelewa sehemu zao za siri  kwani kila aliyedai hivyo alipochunguzwa alikutwa nazo.

Katambi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, akiwa katika ziara ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, alipokwenda kukagua ajali ya moto iliyoteketeza vibanda zaidi ya 500 katika Soko la Mawasiliano Simu 2000 iliyotokea Aprili 4, mwaka huu.

Alisema baada ya kuibuka taarifa hizo potofu katika mikoa ya Mbeya na Songwe,  Jeshi la Polisi nchini lilichukua hatua haraka.

“Jambo hilo limefanyiwa uchunguzi wa kina kupitia Jeshi la Polisi mara moja na kubainika kila aliyeshutumu nyeti zake kupotea alifanyiwa uchunguzi na ukaguzi ulibaini nyeti hizo zipo. Ilibainika ni uzushi na uongo uliosababisha kupoteza maisha ya watu.

“Ni mila potofu na uzushi unaoleta madhara makubwa kwa Watanzania, wapo watu wenye ualbino walipoteza maisha kwa kuamini wakiwachanja viungo vyao au kuchukua uhai wao baadaye unaweza kupata nafasi za kibiashara, uongozi au kushinda katika uchaguzi

“Sisi wote tulioingia katika siasa hakuna aliyeshinda kwa viungo hivyo na kama ingekuwa hivyo wote tungekuwa wabunge ama kupata nafasi ya uongozi,” aliongeza.

Katambi alisema jambo hilo ni uzushi ambao unapaswa kukemewa kwa sura zote za kidini, kimila na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kusimamia sheria.

Waziri huyo pia alitoa onyo kwa wananchi wanaoeneza uzushi kama huo au kuchukua sheria mkononi, kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Pia, alilitaka Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaotoa taarifa za uzushi kupitia mitandao ya kijamii zinazohatarisha amani ya nchi.

MATUKIO

Juzi, Jeshi la Polisi nchini, lilitoa onyo kali dhidi ya wanaoendekeza upotoshaji na uzushi  wa nyeti za wanaume kutoweka na kuusambaza katika mitandao ya kijamii, hali iliyosababisha madhara makubwa kwa watu na familia zao.

Polisi walielekeza kwa yeyote anayejirekodi, anayetengeneza vichekesho kwa kutumia uzushi huo na wanaosambaza nao wasakwe, wakamatwe kwa hatua za kisheria.

Onyo hilo lilitolewa kupitia taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime.

Kwa mujibu wa Misime, imani hizo potofu za uzushi na za kusingizia watu wengine mpaka hivi sasa zimesababisha vifo vya watu saba ndani ya siku nne na wengine majeruhi wakiendelea na matibabu hospitalini. 

Previous Post

DK. MWIGULU ATANGAZA AHUENI WAFANYABIASHARA SIMU 2000

Next Post

RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

Next Post
RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

RAIS WA MUZIKI AHIMIZA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI AMTAJA DK. SAMIA UJENZI BANDARI YA KWALA

DK. NCHIMBI AMTAJA DK. SAMIA UJENZI BANDARI YA KWALA

10 months ago
UKIFUATA USHAURI HUU WA KITAALAMU ‘UTATOBOA’ 2026

UKIFUATA USHAURI HUU WA KITAALAMU ‘UTATOBOA’ 2026

7 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?