• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 10, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dodoma
Na Waandishi Wetu

HATUA ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kupunguza matumizi ya mafuta katika ofisi yake, imeelezwa ni ya kizalendo na kielelezo cha uongozi makini.

Katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Dk. Samia aliwaagiza viongozi na watendaji serikalini, kupunguza matumizi ya mafuta, kufuatia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia, kunakotokana na vita vya Mashariki ya Kati.

“Ndani ya serikali tuna matumizi makubwa sana ya mafuta, magari ni mengi na safari ni nyingi, hivyo ni muhimu kuanza kupunguza matumizi,” alisema Rais Dk. Samia, katika tukio hilo ambalo Profesa Palamagamba Kabudi aliapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu, akichukua nafasi ya marehemu William Lukuvi.

Rais Dk. Samia alionyesha mfano alipotangaza kwamba kuanzia sasa, atakapokuwa anasafiri watendaji katika ofisi ya rais watakaofuatana naye, watatumia usafiri wa pamoja wa mabasi madogo, hatua itakayopunguza matumizi ya mafuta na gharama za uendeshaji.

Wabunge, wasomi na wananchi kwa jumla, wamepongeza uamuzi huo wa Dk. Samia wakieleza ni wa kizalendo na busara katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kuwa salama.

WABUNGE

Mbunge wa Kisarawe, Dk. Selemani Jafo,  amesema Rais Dk. Samia ametoa somo la nini maana ya kuwa kiongozi makini na ana imani taifa litavuka salama dhidi ya changamoto ya bei ya mafuta kupaa.

“Nina imani tutatoka salama katika eneo hili na nchi itazidi kusonga mbele, tumuombee  Mwenyezi Mungu amlinde katika utekelezaji wa majukumu yake,” alisema Jafo.

Mbunge wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa,  amesema Rais, amefanya jambo la kizalendo na kutoa mwanga kama taifa  nini kifanyike, akianza  na ofisi yake  kubana matumizi ya mafuta.  

“Hii ndiyo maana ya uongozi wa kuonyesha njia.”alisema Mbunge Kadogosa.

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, ameeleza kuwa hatua ya Rais kuanza   kubana matumizi ni uwajibikaji, kwa kuwa kuhusika na matatizo ya Watanzania ni kujali kwa kiongozi.

“Haijalishi ni kwa kiwango gani tutapunguza matumizi ya mafuta,  lakini kwa kiongozi mkuu kufanya hivyo kwa vitendo, ni kuagiza taifa lote kuishi kwa kufunga mkanda kipindi hiki cha uhaba wa mafuta. Ni matarajio yangu serikali na taasisi zake watapunguza matumizi ya mafuta,”alisema.

Mbunge wa Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu,  alisema kitendo cha Rais kupunguza  idadi ya magari katika  safari zake ni cha kizalendo na mapenzi kwa nchi.

“Rais ameonesha kuguswa na jambo la matumizi serikalini, wakati huu ambapo wananchi wanaenda kuwa na mzigo wa uzalishaji kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani, nimefarijika sana,” amesema mbunge huyo.

Alisema wananchi wanapenda kuona viongozi wanaguswa na hisia zao na maumivu yao, kwa hiyo uamuzi huo wa Rais Dk. Samia hapana budi ufuatwe na viongozi na watendaji wote serikalini.

Kingu alishauri utolewe waraka  wa serikali utakaowaelekeza  viongozi wakiwemo wa kitaifa, mawaziri na wakuu wa mikoa kubana matumizi kwa    kuhakikisha misafara yao inaepukana na msururu wa magari.

“Siku zote tunasema Rais Samia ni msikivu na anajali shida za watu anaowaongoza, nimefarijika kwa sababu mimi naona Rais amejibu kwa matendo,  huu ndiyo uongozi, angalia namna wananchi wamepokea kwenye mitandao, hii inajenga imani kubwa ya wananchi kwa uongozi wa nchi yao,” alisema Kingu.

Mbunge wa Mbeya Vijijini, Patali Shida Patali,  amesema hatua ya Rais Samia ya kutangaza kubana matumizi ni mtazamo mpya wa utawala bora kwa nchi.

Mchumi Dk. Hildebrand Shayo, amesema uamuzi wa Rais Dk. Samia wa kuanza kupunguza matumizi ya mafuta kupitia magari ya msafara wake ni nzuri.

Alisema hatua  kubana matumizi kukabiliana na changamoto ya kupaa kwa bei ya bidhaa za petroli,  isiwe kwa viongozi  na watendaji serikalini pekee,  hata walio katika sekta binafsi wapunguze safari zisizo za lazima.

“Rais Dk. Samia ameamua kuanza na ‘nyumbani’ ni jambo zuri ambalo linatakiwa kuungwa mkono na watu wengine hata wa sekta binfsi ili kupunguza matumizi ya mafuta kwa wingi,” alishauri msomi huyo.

WANANCHI  

Juma Mfaume, mkazi wa Mipango mjini Dodoma,  alisema uamuzi  wa rais unaonesha mfano wa uongozi wa vitendo na  uzalendo kwa taifa.

“Hii ni ishara nzuri sana. Kama Rais mwenyewe anaweza kupunguza matumizi, basi hata viongozi wengine wanapaswa kuiga,” alisema.

Mfanyabiashara ndogo ndogo katika Soko la Majengo, Rehema Said;

“Tunapambana na hali ngumu ya maisha, tukiona viongozi wanapunguza matumizi tunajisikia kuthaminiwa. Ina maana wanawafikiria wananchi.” 

Previous Post

NETIBOLI WATAKA AMANI MICHEZONI

Next Post

TUMAINI JIPYA LA MIKOPO KWA VIJANA

Next Post
TUMAINI JIPYA LA MIKOPO KWA VIJANA

TUMAINI JIPYA LA MIKOPO KWA VIJANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UWEKEZAJI WA SHILINGI BILIONI 50 KITUO CHA MPOMVU WAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME KANDA YA ZIWA

UWEKEZAJI WA SHILINGI BILIONI 50 KITUO CHA MPOMVU WAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME KANDA YA ZIWA

1 month ago
UNDANI WA REKODI YA MSUVA AFCON

UNDANI WA REKODI YA MSUVA AFCON

4 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?