• ePaper
Sunday, May 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAMBO YAANZA KUNOGA MEI MOSI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAMBO YAANZA KUNOGA MEI MOSI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi, katika kukuza uchumi na maendeleo ya taifa.

Dk. Mwigulu alisema hayo jijini Dodoma, katika hafla ya maandalizi ya Mei mosi, mwaka huu, ambayo kitaifa inafanyika mkoani Njombe.

Alisema serikali inaendelea kuwaenzi wafanyakazi nchini kutokana na umuhimu wao mkubwa kwa taifa.

Katika hafla hiyo ya awali, sh. bilioni 1.105 zilikusanywa ambapo Dk. Mwigulu alisema fedha hizo zitasaidia mkoa mwenyeji kukamilisha shughuli za maandalizi ya tukio hilo.

Pia,Waziri Mkuu alilipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) kwa ubunifu wa kuhakikisha maadhimisho ya Mei Mosi yanaacha alama katika mkoa mwenyeji.

“Wenzetu TUCTA wamekuja na ubunifu kwamba shughuli za Mei Mosi zinaacha alama katika mkoa husika kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama walivyofanya katika maadhimisho ya mwaka 2025 mkoani Singida kwa kujenga uwanja wa Bombadia mkoani humo.

“Uwanja ambao sasa umekuwa na manufaa makubwa kwa Wanasingida na Njombe nako wamejiandaa kuacha alama kubwa,”alisema.

Kwa upande wake,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Uhusiano, Deus Sangu, alisema maandalizi ya maonesho ya Mei Mosi, mwaka huu, yanaendelea vizuri akisisitiza kuwa kwa siku zilizosalia, maandalizi yote yatakamilika ndani ya wakati.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, alisema maadhimisho hayo ni fursa kwa mikoa yote ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kwa kuwa ugeni wa watu wasiopungua 5, 000 unatarajiwa kushiriki sherehe za Mei Mosi Kitaifa mkoani humo.

Naye, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, alishukuru na kupongeza kuimarika ushirikiano kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi, akisema ushirikiano huo umechangia kuwepo kwa utulivu miongoni mwa wafanyakazi nchini.

Previous Post

MUOSHA MAGARI AAMRIWA KUFANYA USAFI MAHAKAMANI

Next Post

RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

Next Post

RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU

DIARA ASHUSHIWA ‘RUNGU’ LIGI KUU

2 months ago
IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342

IDADI WAGONJWA FIGO YAFIKIA 3,342

2 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?