• ePaper
Sunday, May 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU, Dodoma

WANANCHI wameaswa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika biashara ya kaboni kwa kuanzisha miradi mbalimbali kulingana na jiografia ya eneo husika na kuacha dhana ya upandaji miti na misitu ndiko inakopatikana biashara hiyo.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Richard Muyungi wakati akifungua kikao cha makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kuhusu

Programu ya Mageuzi ya Kimkakati ya Mazingira Endelevu Tanzania, kilichofanyika Dodoma, jana, akieleza kuna fursa katika program hiyo ikiwemo biashara ya kaboni.

Alisema fursa ya biashara ya kaboni haipo pekee katika upandaji miti kama ambavyo wengi wanadhani, bali katika nishati safi ya kupikia, miradi ya taka, usafishaji wa miji, taka ngumu na nyingine zote zinazoweza kuwa fursa katika biashara hiyo.

“Ili tuwe na mchango mkubwa kwenye Dira 2050 tunatakiwa kuwa na mpango maalumu na hatutakuwa tukiangalia katika upandaji miti pekee, bali tutaangali pia kwenye nishati safi ya kupikia kuwafikia wananchi,” alisema.

Aliongeza kutokana na heshima ambayo mazingira yamepewa na kuwekwa kwenye Dira 2050 ni vyema sekta ya mazingira nayo ibadilike mchango wake uonekane kwa kuyasimamia mazingira vizuri.

Awali, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda alisema programu hiyo inalenga kuchagiza matokeo makubwa na ya haraka katika kurejesha uoto wa asili, ustawi wa mifumo ikolojia na kuimarisha huduma za kiikolojia ambazo zinachangia katika sekta za uzalishaji nchini.

“Programu hii itatekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuongeza eneo lenye uoto wa kijani kupitia upandaji miti kwa wingi na usimamizi wa mazingira. Pia, kupunguza uharibifu wa ardhi na ardhi-oevu, kurejesha ardhi na misitu iliyoharibiwa na kukijanisha miji yetu.

“Jitihada hizi zitachangia kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa; kurejesha hekta milioni tano za ardhi, misitu, ardhi-oevu na nyanda za malisho zilizoharibiwa, kuhamasisha usafi wa mazingira na uchumi rejeshi katika usimamizi wa taka.

Aliongeza maeneo ya kimkakati ya utekelezaji wa programu ya mageuzi ya kukijanisha Tanzania ni upandaji miti katika mkoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Geita, Singida, Simiyu, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Rukwa na Zanzibar.

Shughuli nyingine ni pamoja na uanzishwaji bustani za kijani katika maeneo ya miji; utunzaji na urejeshaji wa maeneo oevu ya Ziwa Natron, Bonde la Mto Mara, Bonde la Mto Malagarasi Myovosi na Bonde la Mto Kilombero, kudhibiti viumbe vamizi katika maeneo ya mikoa ya Dodoma, Arusha, Mara, Mwanza na Manyara; usafi wa mazingira na urejelezaji wa taka ngumu.

Aidha, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa, alisema katika utekelezaji wake, pogramu hiyo muhimu itaweka mkazo katika hatua za kimkakati ikiwemo kukuza uelewa wa umma kuhusu masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira, kuhamasisha ushiriki wa wadau katika ngazi zote hususan mamlaka za serikali za mitaa na kuweka mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji.

Previous Post

KAMATI YA UTALII, BIASHARA NA KILIMO BARAZA LA WAWAKILISHI YADHAMIRIA MAMLAKA YA VIPIMO ZANZIBAR IFIKIE VIWANGO VYA WMA BARA

Next Post

KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

Next Post
KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

6 months ago
DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

2 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?