• ePaper
Sunday, May 17, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIGOGO CHAUMMA ‘AIPA TANO’ TUME YA JAJI CHANDE
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SIMON NYALOBI

ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka jana, ina umuhimu mkubwa katika kujenga mustakabali wa maridhiano ya kitaifa na huku akisifia weledi, ubobevu na uzoefu wa wajumbe wa tume hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam, Mwalimu aliwataka wananchi kuelewa umuhimu wa tume na wajumbe wa tume hiyo, kwa kuwa wana sifa stahiki kutekeleza majukumu hayo.

“Hii tume ina umuhimu mkubwa sana kwa wananchi, kwa sababu wananchi watatamani kujua kilichotokea waliohusika wanawajibikaje eeh na kadhalika…, pia wananchi wanatamani kuona kabisa tukio lile halitokei tena katika nchi yetu.

“Kwa hiyo ni tume ya wananchi kimsingi, inaitwa Tume ya Rais, kwa sababu imeundwa na rais kwa niaba ya mamlaka aliyopewa na wananchi, ila ukweli ni tume ya wananchi wenyewe,” alisema.

Akizungumzia umuhimu wa tume hiyo, alisema matokeo yake yatayagusa maisha yao moja kwa moja na itawafikisha wananchi katika maridhiano.

“Matokeo ya tume hii yatawagusa maisha yao moja kwa moja kama ambavyo yaliyotokea Oktoba 29, yaliwagusa na wengine yakawaathiri moja kwa moja, kwa hiyo ‘there is no doubt’, tume itatufikisha kwenye maridhiano.

“Kwa sababu mwisho wa jambo hili lazima Watanzania tuzungumze, hakuna namna nyingine na mwisho wa mazungumzo ni maridhiano,” alisema.

Mwalimu alisema katika maridhiano ni kukiri kwa makosa kwa kuombana radhi, fidia na kukubalina kama taifa kulaani vitendo vya aina hiyo visitoke tena katika taifa.

UAMINIFU NA WELEDI

Kuhusu uaminifu na weledi wa wajumbe wa tume hiyo, alisema wajumbe hao wamesheheni sifa lukuki za kutekeleza jukumu hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, ambaye anaaminika kimataifa.

Mwalimu aliwashangaa wanaohoji weledi wa Jaji Mkuu mstaafu Chande katika kutekeleza jukumu hilo.

“Nani anayeweza kuuliza uaminifu wa mheshimiwa Jaji Chande, unawezaje kuhoji, unaweza kuja na kuhoji uwezo wake, huyu mtu ameshafanya kazi mahakama za ndani, ameshafanya mahakama za kimataifa kimataifa.

“Inawezekana ni yale mambo ya nabii havumi kwao, hivi nchi gani ingepata tatizo lile lisingemchukua Jaji Chande kuwa mwenyekiti wa hiyo tume anakosa nini…, hata huyo mwingine ambaye angeletwa ingewezekana angekuwa kama Jaji Chande au pengine sifa zake zisingekuwa toshelevu kumzidi Jaji Chande,” alisema.

Alifafanua, sifa za mjumbe wa tume hiyo Inspekta wa Jeshi la Polisi mstaafu (IGP) Said Mwema, kuwa aliacha alama katika jeshi hilo kulifanyia mabadiliko, uadilifu na umakini.

Mwalimu alisema alitumikia taifa kwa uadilifu na kujenga heshima katika jeshi hilo enzi zake akiwa madarakani.

Aidha, alisema mjumbe wa tume hiyo Balozi Ombeni Sefue, ni ofisa mwandamizi wa serikali aliyeitumikia serikali kwa muda mrefu.

Pia, alisema mjumbe mwingine wa tume hiyo, Dk. Stergomena Tax, ana sifa ya kuwepo katika tume hiyo kutokana na utumishi wake katika taasisi mbalimbali za ndani na kimataifa.

Previous Post

MUYUNGI ASISITIZA WANANCHI KUFANYA BIASHARA YA KABONI

Next Post

RAIS DK. SAMIA ATOA MWELEKEO WA KITAIFA

Next Post
RAIS DK. SAMIA ATOA MWELEKEO WA KITAIFA

RAIS DK. SAMIA ATOA MWELEKEO WA KITAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI

NI ZAMU YETU LINAKUJA NYUMBANI

4 months ago
DK. SAMIA AMETEKELEZA MIRADI MINGI YA MAENDELEO – DK. NCHIMBI

DK. SAMIA AMETEKELEZA MIRADI MINGI YA MAENDELEO – DK. NCHIMBI

9 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    DK. MWIGULU AHIMIZA WANANCHI KUIOMBEA AMANI YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU MOGAE WA BOTSWANA, AKIMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA KUWA NA HADHI YA  UTALII WA JIOLOJIA (GEOPARK MUSEUM)

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAIPONGEZA PUMA ENERGY KWA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?