• ePaper
Sunday, April 19, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

AJIRA 45,000 ZANUKIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
AJIRA 45,000 ZANUKIA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, Dodoma

SERIKALI imepanga kutoa vibali vya ajira 45,000 za kada mbalimbali kujaza nafasi katika taasisi za umma kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Hayo yalibainishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka huo wa fedha.

“Katika mwaka 2026/2027, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepanga kushughulikia vibali vya nafasi 45,000 za ajira mpya kwa ajili ya kujaza nafasi zitakazoidhinishwa katika ikama za taasisi za umma na kuzihakiki,” alisema.

Pia imepanga kuidhinisha madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma katika taasisi 425.

YAOMBA SH. TRILIONI 1.5

Kwa mujibu wa Kikwete, ofisi hiyo imeliomba Bunge kuidhinisha matumizi ya jumla ya sh. trilioni 1.5 katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Alisema kati ya fedha hizo, sh. trilioni 1.4 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida, huku sh. bilioni 163 zikielekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Katika hatua nyingine, Kikwete alisema hadi Machi mwaka huu, jumla ya wasailiwa 91,126 katika ajira za serikali walipangiwa vituo vya kazi, huku ujazaji wa nafasi 12,722 ukiendelea.

Alisema wasailiwa 41,102 wamehifadhiwa katika kanzidata baada ya kufaulu usaili wa mahojiano, wakiwemo wanaume 21,899 na wanawake 19,203 wa kada mbalimbali.

Vilevile, alisema katika kipindi hicho, saili sita za mchujo zilifanyika kutokana na waombaji ajira 845,042 kuwasilisha maombi, ambapo wanaume walikuwa 490,514 na wanawake 354,528.

“Jumla ya wasailiwa 9,836 walifanya usaili wa vitendo, wakiwemo wanaume 6,928 na wanawake 2,908. Ujenzi wa mfumo wa kupima haiba na tabia kwa wasailiwa umekamilika na kwa sasa upo katika hatua za majaribio,” alisema.

AJIRA 43,866

Ridhiwani alisema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi mwaka huu, ofisi hiyo pamoja na taasisi zake imeboresha utendaji kazi serikalini kwa kuimarisha upatikanaji na usimamizi wa rasilimali watu kwa kutoa vibali vya ajira 43,866 katika sekta mbalimbali.

Alisema serikali imeidhinisha ajira mbadala, uhamisho, likizo bila malipo na nafasi za uongozi zaidi ya 7,000, hatua iliyoongeza ufanisi wa kiutendaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Serikali imehakiki na kulipa madai ya mishahara na malimbikizo kwa zaidi ya watumishi 14,600 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 22, hatua iliyoongeza motisha na ufanisi kazini kwa watumishi wa umma. Uboreshaji wa mifumo ya kiutumishi umeimarisha usimamizi wa rasilimali watu na kuongeza tija katika utoaji huduma za serikali,” alisema.

MATAMKO YA VIONGOZI

Akizungumzia matamko ya viongozi, alisema serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeimarisha maadili ya viongozi wa umma, ambapo asilimia 85 ya viongozi wamewasilisha matamko ya mali na madeni.

Alisema hatua hiyo inaonesha kuimarika kwa uwajibikaji wa viongozi na kuongeza uaminifu wa wananchi kwa taasisi za umma ikiwa sehemu ya juhudi za kujenga serikali inayowajibika, yenye uwazi na inayoaminika.

“Wananchi 34,334 wamepatiwa elimu ya maadili, hatua ambayo inachangia kukuza utamaduni wa uadilifu na uwajibikaji katika jamii. Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia maadili kwa vitendo kwa sababu uadilifu wa viongozi ndio msingi wa haki, maendeleo na imani ya wananchi kwa serikali yao,” alisema.

Aliongeza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo watumishi wake, kwa kuwa mtumishi bora ni msingi wa huduma bora kwa mwananchi.

Jumla ya viongozi 4,867 walitia saini hati ya ahadi ya uadilifu, ambapo wanaume ni asilimia 69 na wanawake asilimia 31.

KUUNGANISHA MIFUMO YA SERIKALI

Kwa mujibu wa Ridhiwani, serikali imeboresha utoaji huduma kwa wananchi kwa kuwekeza katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Alisema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026, jumla ya mifumo 252 ya serikali imeunganishwa katika mtandao, hatua ambayo inawawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi, haraka na bila ulazima wa kufika ofisini, hivyo kupunguza gharama na muda.

“Uboreshaji huo umepunguza urasimu katika utoaji wa huduma na kuongeza uwazi, na hatimaye kuimarisha uwajibikaji katika taasisi za umma,” alisema.

Previous Post

KIBANO CHA WAZIRI MKUU DK. MWIGULU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

5 months ago
YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

YANGA, PRISONS KIVUMBI LEO

1 month ago

Popular News

  • AJIRA 45,000 ZANUKIA

    AJIRA 45,000 ZANUKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIBANO CHA WAZIRI MKUU DK. MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • USALAMA MZURI KUWALETA NCHINI WABUNGE 2000 IPU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. JAKAYA AKUTANA NA RAIS RUTO JIJINI NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?