• ePaper
Thursday, July 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

‘KNOCKOUT YA MAMA’ KUWAVUTA MABONDIA KIMATAIFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 23, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
‘KNOCKOUT YA MAMA’ KUWAVUTA MABONDIA KIMATAIFA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

SERIKALI imesema pambano la ngumi za kulipwa la ‘Knockout ya Mama’ litakuwa chachu ya kufungua milango ya  mabondia wakubwa kutoka mataifa mbalimbali duniani, kuja nchini.

Pamoja na hilo, pambano hilo litasaidia kukuza tasnia ya ndondi na kuongeza fursa kwa mabondia hapa nchini

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Mafia na +Alvin Camique kutoka Ufilipino.

Mafia na Camique watadundana katika pambano la marudiano la raundi 10, litakalofanyika Ukumbi wa EACLC uliopo Ubungo, Dar es Salaam.

Katika pambano la awali lililofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 10, mwaka jana, Mafia alipoteza kwa TKO raundi ya nne.

Makonda alisema pambano hilo litaitangaza Tanzania kimataifa na kuwavutia mabondia wenye majina makubwa kuja nchini kupambana na mabondia wetu.

Waziri huyo alisema ujio wa mabondia kutoka Uingereza, Urusi, Marekani, Ujerumani na Falme za Kiarabu utasaidia kukuza tasnia ya ndondi pamoja na kuongeza fursa kwa mabondia hapa nchini.

“Pambano hili linapaswa kufungua milango kwa mabondia wakubwa kuja nchini, si tu kushiriki mashindano bali  kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mambo mazuri yaliyopo,” alisema Makonda.

Aidha, Waziri huyo alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo na kuwaunga mkono mabondia wa ndani watakaopanda ulingoni kupeperusha bendera ya nchi.

Akizungumzia maandalizi ya pambano lake,  Mafia alisema hatakubali kupoteza pambano    baada ya kufanya mazoezi makali chini ya kocha Kanda Kabongo.

“Nimejifua vikali kwa lengo la kulipa kisasi, kocha ameniongoza kufanya mazoezi makali ambayo naamini yatanisaidia kumtwanga mpinzani wangu,” alitamba Mafia.

Mwanamasumbwi huyo alisema amenolewa na makocha wawili ambao wamempa mbinu tofauti za kumchapa Camique.

Kocha wa bondia huyo, Kabongo, alisema katika pambano la marudiano, mashabiki wa ndondi wajiandae kushangilia ushindi wa bondia wake ambaye amepikwa kikamilifu.

Kabongo aliwaomba Watanzania na wadau wa masumbwi kujitokeza kwa wingi kumshangilia Mafia.

Previous Post

SHILOLE AMSHUKURU RAIS DK. SAMIA

Next Post

MABEKI YANGA SC, AZAM FC KIBOKO

Next Post
MABEKI YANGA SC, AZAM FC KIBOKO

MABEKI YANGA SC, AZAM FC KIBOKO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

KIBANO KIKALI WALIOZIMA ‘X-RAY’ TEMEKE

7 months ago
YANGA, SIMBA NI VIKUMBO

YANGA, SIMBA NI VIKUMBO

7 months ago

Popular News

  • MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • 50 BORA ‘FORM SIX’ KUSOMA AI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2/- YAKAMATWA IKITOROSHWA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAKA UADILIFU, USHIRIKIANO NA MATOKEO KWA VIONGOZI WAPYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?