• ePaper
Wednesday, May 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 13, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI Yanga ikihesabu siku na pointi za kutangaza ubingwa, Yanga leo inajitupa tena dimbani kuivaa Dodoma Jiji katika katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pambano hilo, limepangwa kupigwa katika Uwanja wa Airtel uliopo  Singida Mjini, kuanzia saa 10:15 jioni.

Yanga itacheza mechi hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Coastal Union ya Tanga na kushinda mabao 3-0.

Kikosi hicho chenye maskani mitaa ya Twiga na Jangwani itaingia dimbani  ikiwa kileleni na pointi 54 huku Dodoma Jiji ikishika nafasi ya nane na baada ya kukusanya alama 29 baada ya wote kushuka dimbani 22.

Kocha  Msaidizi wa timu hiyo, Abdihimid Moallin,  alisema timu itaingia dimbani huku ikiwa na kumbukumbu ya kufanya vyema katika michezo iliyopita.

“Tunatambua ugumu wa ratiba na  mechi yenye upinzani dhidi ya Dodoma Jiji, timu yangu imejipanga kwa ushindi kwa kuwa tunataka alama tatu kwa l engo la kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa,” alitamba Moalin.

Moalin amesema pamoja na kikosi chake  kutwaa ubingwa  mara nne  mfululizo, wachezaji wake bado wana njaa ya kubeba ubingwa.  

Amesema  amezifanyia kazi kasoro zote zilizojitokeza  katika mechi iliyopita hivyo anaamini kuwa mechi ya leo haitakuwa na mapungufu.

“Tunataka kuendelea kufanya vizuri na kutopoteza mchezo wowote katika mechi nane zilizobaki na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji,” aliongeza.

Pia, amesema Mohamed Hussein aliyekuwa majeruhi ameanza mazoezi.

Kipa wa Yanga, Hussein Masalanga, amesema kikosi chao kipo tayari kuendeleza  wimbi la ushindi.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho (leo), kila mmoja wetu anajua umuhimu wake. Kwa sasa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo,” amesema Masalanga.

Kocha wa Dodoma Jiji, Amani Josiah, alisema pamoja na Yanga kuwa na kikosi bora, timu yake haitabweteka na kukubali kufungwa.   

Alisema timu yake  imejipanga kuizuia Yanga au kupata alama zote au walau kugawa pointi.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wetu na Yanga, tunajua ugumu wa mchezo na tutaingia uwanjani kwa kuwaheshimu wapinzani wetu,” alisema Josiah.

Kocha huyo aliwaomba mashabiki na wapenzi wa timu yao kuendelea kuwapa sapoti  ili waweze kufanya vizuri katika michezo iliyobakia ya ligi.

Previous Post

MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

Next Post

TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

Next Post
TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA : DK. SAMIA ANASTAHILI ‘MITANO TENA’

WASIRA : DK. SAMIA ANASTAHILI ‘MITANO TENA’

9 months ago
HIZA SALUM ‘KHIZZER’ AWASIHI WASANII KUTIMIZA MALENGO

HIZA SALUM ‘KHIZZER’ AWASIHI WASANII KUTIMIZA MALENGO

5 months ago

Popular News

  • BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BALOZI DK. BASHIRU AONGOZA JUMUIKO LA KADEFO AKITAJA JITIHADA ZA RAIS DK. SAMIA KUENDELEZA KAGERA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YATANGAZA KUPUNGUZA TOZO YA UENDESHAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • POINTI UBINGWA YANGA SC KUSAKWA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?