• ePaper
Saturday, May 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA SELINA MATHEW

AMIRI Jeshi Mkuu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Jeshi la Polisi, kutopuuza taarifa na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Alisisitiza jeshi hilo linapaswa kuwa makini kukabiliana dhidi ya changamoto za kiusalama zinazobadilika kila siku.

Rais Dk. Samia aliyasema alipofunga mafunzo ya upandishaji vyeo kwa Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi 719 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Tunataka kuona jeshi ambalo halidharau taarifa yoyote. Kiashiria chochote cha hatari kifanyiwe kazi kwa haraka sana. Tulijaribiwa na matukio yaliyotokea Oktoba 29 mwaka jana, lakini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilifanikiwa kuyadhibiti kwa muda mfupi,” alisisitiza.

Alisema iwapo jeshi hilo litakuwa na ushirikiano, mawasiliano ya karibu na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kubadilishana taarifa za viashiria vya hatari, litajenga imani kubwa kwa wananchi.

Pia, aliwataka askari kuzingatia miiko, maadili, sheria katika utekelezaji majukumu yao, ili kuongeza ufanisi na kujenga taswira nzuri ya Jeshi la Polisi mbele ya wananchi.

“Tunataka kuona jeshi ambalo limesimama katika mstari sawa sawa. Rushwa, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka visiwe sehemu ya utendaji wa askari wetu,” alisema.

Rais Dk. Samia alisema jeshi hilo linapaswa kutumia vizuri rasilimali zinazotolewa na serikali katika kuimarisha uwezo wa kiutendaji, mafunzo, ulinzi wa raia na mali zao.

“Tusiseme tu tunachukua hatua, lazima tuone matokeo. Tunataka kuona namna jeshi linavyotumia rasilimali zinazotolewa kuimarisha uwezo wa kiutendaji na kuongeza ufanisi wa kazi,” alisema.

Kuhusu kujenga imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Polisi Jamii, alisema wananchi wanapaswa kuona vituo vya polisi kama sehemu salama ya kupata msaada  wanapokumbana na changamoto za kiusalama.

Alisema taarifa zinaonesha wananchi wengi hawana imani kubwa ya kukimbilia polisi wanapopata matatizo, jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa kuimarisha ushirikiano kati ya jeshi hilo na jamii.

“Tunataka kuona namna Jeshi la Polisi linavyojenga kukubalika kwa wananchi, sekta binafsi na jumuiya ya kimataifa iliyopo nchini. Niliona tathmini moja kuhusu kiwango cha imani kwa majeshi ya polisi katika nchi za Afrika Mashariki, ambapo nchi iliyofanya vizuri zaidi ilikuwa na asilimia 25 ya wananchi wanaoamini wanaweza kukimbilia polisi kupata msaada wanapopata shida.

“Kwa Tanzania ilikuwa asilimia 12 pekee. Hizi ni taarifa ambazo hatupaswi kuzibeza, bali tujiulize mapungufu yako wapi na tuyafanyie kazi ili wananchi waone polisi kama sehemu salama ya kupata msaada,” alisema Rais Samia.

Alisisitiza wananchi wakielimishwa vizuri watalindana na kutoa taarifa za uhalifu mapema, kwa kuwa polisi jamii ni msingi muhimu wa usalama wao.

Aidha, Rais Dk. Samia aliwataka wahitimu kwenda kutumikia taifa kwa uzalendo, nidhamu na uadilifu akisisitiza vyeo walivyopata vinapaswa kuonekana kupitia ubora wa kazi zao na siyo kwa mamlaka pekee.

“Uzalendo wa kweli ni kuwa tayari kulitumikia taifa lako wakati wowote unapohitajika, hata pale ambapo hakuna anayekupongeza,” alisema.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alisema serikali itaendelea kusimamia nidhamu, haki na uwajibikaji ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kuishi kwa amani na kupata huduma bora za kiusalama.

Katambi aliwataka askari kufanyakazi kwa weledi, uadilifu, kuzingatia sheria na viapo vyao vya kazi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita, imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika Jeshi la Polisi kupitia ujenzi wa vituo vya kisasa, ununuzi wa vitendea kazi, ajira mpya, mafunzo yanayolenga kuongeza ufanisi wa jeshi hilo kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Waziri huyo alisisitiza askari wanaokwenda kinyume cha maadili, sheria na taratibu watachukuliwa hatua bila upendeleo, akibainisha wizara hiyo itaendelea kulinda haki za wananchi kuhakikisha sheria zinafuatwa na kila mtu.

Katambi aliwataka Watanzania kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kudumisha amani, kulinda maadili ya jamii na kuimarisha uzalendo.

IGP WAMBURA ASIFU MAGEUZI MAKUBWA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camilius Wambura, alisema Jeshi la Polisi limepiga hatua kubwa ya maendeleo kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia, kupitia uboreshaji miundombinu, vitendeakazi na ajira mpya zilizoongeza ufanisi wa utendaji ndani ya jeshi hilo.

Wambura alisema serikali imewezesha utekelezaji miradi zaidi ya 320 ya ujenzi wa ofisi, vituo vya polisi na makazi ya askari, huku majengo mengi ya zamani yasiyofaa kwa makazi yakiondolewa na kujengwa maghorofa ya kisasa.

Pia alisema Jeshi la Polisi limepata magari mapya zaidi ya 1,300, pikipiki za doria, boti na kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utendaji kazi.

Wambura alisema serikali pia imeendelea kutoa ajira kwa vijana kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo yatima na wenye mazingira magumu, jambo ambalo limeongeza nguvu kazi ndani ya jeshi na kutoa matumaini kwa vijana wengi.

Aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuzingatia uzalendo, nidhamu na uadilifu wanapotekeleza majukumu yao huku akisisitiza Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha polisi jamii, matumizi ya teknolojia na mapambano dhidi ya uhalifu kwa kushirikiana na wananchi.

KAULI YA MKUU WA CHUO

Mkuu wa Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dk. Lazaro Mambosasa, alisema wahitimu wa mafunzo ya uofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi, wanapaswa kuongeza ufanisi, nidhamu na uwajibikaji katika utendaji wa kazi zao.

Mambosasa alisema wanafunzi 720 waliripoti kuanza mafunzo hayo yaliyofunguliwa Desemba 18, mwaka jana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema wahitimu 718 walihitimu baada ya wawili kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Alisema wahitimu hao wamepatiwa mafunzo ya kitaaluma na vitendo yaliyolenga kuwajengea uwezo wa uongozi, uchunguzi wa makosa ya jinai, haki za binadamu, matumizi ya silaha na mbinu za kisasa kukabiliana na changamoto za kiusalama katika maeneo yao ya kazi.

Alisema serikali imeendelea kuwekeza katika Jeshi la Polisi kupitia ajira mpya na kuboresha mafunzo ya askari, jambo ambalo limeongeza uwezo wa jeshi hilo katika kulinda raia na mali zao kuendana na mabadiliko ya teknolojia na uhalifu wa kisasa.

MKUU WA MKOA

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alisema watu waliohusika katika mauaji ya mwekezaji kutoka China yaliyotokea hivi karibuni jijini humo, watakamatwa.

Chalamila alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanapatikana haraka ili kulinda amani na uhusiano wa kidiplomasia.

Alisema tukio hilo linaweza kuleta athari katika uhusiano wa kimataifa iwapo halitashughulikiwa kwa umakini, lakini akaeleza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam linaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha watuhumiwa wote wanatiwa nguvuni.

Mkuu huyo wa Mkoa alimpongeza Rais Dk. Samia, kuendelea kuimarisha Jeshi la Polisi kwa kuongeza ajira za vijana zaidi ya 710 watakaosaidia kuongeza nguvu kazi katika ulinzi, usalama wa taifa na kudumisha amani katika maeneo mbalimbali.

Previous Post

DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

Next Post

UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

Next Post
UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JK AMWOMBEA KURA DK. SAMIA

JK AMWOMBEA KURA DK. SAMIA

9 months ago
SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

SIMBA QUEENS MENO NJE, YANGA YALIA NA WACHEZAJI

5 months ago

Popular News

  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASTAA YANGA WAUTAJA UBINGWA LIGI KUU BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?