• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIGOMA KUMENOGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIGOMA KUMENOGA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali inaendelea kutekeleza ahadi ya kuufungua Mkoa wa Kigoma kiuchumi kupitia miradi ya kimkakati.

Aliyasema hayo mkoani Kigoma, baada ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi la miradi mikubwa ya kimkakati ya Reli ya Kisasa (SGR) na meli nne.

Alisema serikali inaendelea kutekeleza ahadi ya kuifufua Kigoma kwa kuwekeza katika miundombinu ya kisasa, itakayounganisha mkoa huo na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Rais Dk. Samia aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Tabora-Kigoma chenye urefu wa kilometa 506, kitakachogharimu sh. trilioni 7.4.

Alisisitiza Kigoma haitakuwa tena mwisho wa reli, bali kituo cha kati kinachofungua fursa mpya za uchumi.

FAIDA ZA MRADI

Akizungumza na wananchi wa Kigoma, Rais Dk. Samia alisema ujenzi wa reli ya kisasa, uendelezaji wa bandari, barabara na viwanja vya ndege, unalenga kupunguza gharama za usafirishaji.

Pia, kurahisisha bidhaa kufika sokoni na kuifanya Tanzania kutumia kikamilifu nafasi yake ya kijiografia, lango la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki, Maziwa Makuu, Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika.

Rais Dk. Samia alisema Kigoma ina nafasi ya kipekee kutokana na ukaribu wake na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jambo linaloifanya kuwa kitovu muhimu cha biashara na uwekezaji kupitia miundombinu inayojengwa.

Alisema mradi wa  SGR kipande cha Tabora–Kigoma, utaiunganisha Kigoma,Tabora, Dodoma, Morogoro na Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo na bidhaa haraka na uhakika.

“Kukamilika reli hii kutawanufaisha wakulima kwa kupunguza gharama za pembejeo na kuwafungulia masoko mapya ya mazao, wavuvi watapata urahisi wa kusafirisha mazao ya uvuvi kwenda katika masoko yenye uhakika ndani na nje ya nchi,” alieleza Rais Dk. Samia.

Pia, kukamilika reli hiyo kutachochea ukuaji wa miji iliyopo kando ya njia ya reli, kuongeza shughuli za kiuchumi na kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, biashara, madini na kilimo.

Rais Dk. Samia alisema serikali imejipanga  kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati  inaendelea kutekelezwa kwa wakati kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Aliwataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika utekelezaji  wa miradi ya maendeleo, kwa kutumia fursa zinazozalishwa na uwekezaji  wa serikali.

Alisisitiza SGR ni nguzo muhimu ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara ukanda wa Afrika Mashariki.

UZINDUZI WA MELI NNE

Rais Dk. Samia akizindua mradi wa ujenzi wa meli nne za mizigo katika Ziwa Tanganyika, alisema utaongeza uwezo wa kusafirisha mizigo kwenda Burundi, Zambia na DRC.

Alisema hatua hiyo itachochea biashara, kuvutia uwekezaji zaidi na kuzalisha ajira katika sekta mbalimbali zikiwemo bandari, maghala, hoteli, usafirishaji na matengenezo ya mitambo.

Alipongeza sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali kuwekeza katika miradi ya usafirishaji na kuhimiza wawekezaji wengine wajitokeze kuwekeza nchini.

Aidha, aliitaka Wizara ya Uchukuzi, kufanya mazungumzo na wawekezaji kukamilisha haraka ujenzi wa karakana kubwa ya kutengeneza na kufanyia matengenezo meli.

AMANI, ULINZI WA MIUNDOMBINU

Katika hatua nyingine, Rais Dk. Samia aliwataka Watanzania kuendelea kuilinda amani, usalama na miundombinu ya kimkakati inayojengwa nchini.

Alitoa wito kwa wananchi kuwaepuka wasaliti na maadui wa nchi wasipate nafasi ya kuhujumu uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Alisema pamoja na serikali kuwekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo, wananchi wana wajibu wa kuhakikisha miundombinu hiyo, inalindwa dhidi ya vitendo vya hujuma na uharibifu.

“Sisi sote tuwe macho, tuepuke wasaliti na maadui wa nchi, tuna wajibu wa kulinda amani, usalama na miundombinu hii kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho, wote tuwe na itikadi ya usalama kwanza, halafu maendeleo,” alisema Rais Dk. Samia.

Aliwataka viongozi, wananchi, vyombo vya ulinzi na usalama, kuendelea kushirikiana katika kuweka mikakati madhubuti ya kulinda miradi ya kimkakati.

AWASHUKURU KUIAMINI CCM

Vilevile, Rais Dk. Samia, aliwashukuru wananchi wa Mkoa wa Kigoma, kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema imani walioionesha wananchi, siyo hisani isipokuwa deni ambalo serikali italipa kwa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.

“Imani mliotupatia Chama Cha Mapinduzi siyo suala la hisani. Imani yenu kwetu ni deni tutakalowalipa kwa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo,” alisema.

Alikumbusha mwaka 2022 kuwa, aliahidi Kigoma haitakuwa tena mwisho wa reli, bali kituo cha kutoka Dar es Salaam kwenda mbele, akisema utekelezaji wa ahadi hiyo, tayari umeanza.

“Nilikuja Kigoma mwaka 2022 na kuwaahidi kwamba, Kigoma haitakuwa mwisho wa reli, bali itakuwa kituo cha katikati kutoka Dar es Salaam kufika Kigoma kwenda mbele na ahadi hiyo tumeanza kuitekeleza,” alisema.

Alisema serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji kupitia ujenzi wa reli ya kisasa, bandari, barabara na viwanja vya ndege kwa lengo la kuifungua Tanzania kibiashara na uwekezaji.

Alieleza kuwa, miradi ya reli, bandari, barabara na viwanja vya ndege, inajengwa kuiunganisha Tanzania na masoko ya ndani na nchi za Afrika Mashariki, maziwa makuu, Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika.

WAZIRI MBARAWA

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema serikali inaendelea kutekeleza uwekezaji mkubwa katika sekta ya uchukuzi, kuijenga Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji, biashara na huduma za ugavi Afrika Mashariki na Kati.

Alisema serikali imewekeza katika Reli ya Kisasa (SGR), bandari, viwanja vya ndege na usafiri wa majini, kwa lengo la kujenga mfumo jumuishi wa uchukuzi unaounganisha maeneo ya uzalishaji, masoko ya ndani na nchi jirani.

Aidha, Profesa Mbarawa, alisema uzinduzi wa meli nne mpya za mizigo katika Ziwa Tanganyika, utafungua enzi mpya ya usafirishaji wa majini kwa kuongeza uwezo wa kubeba mizigo, kuimarisha usalama wa safari, kupunguza gharama za usafirishaji na kukuza biashara kati ya Tanzania, Burundi na DRC.

Alisema uwekezaji huo, unatarajiwa kuzalisha ajira 600 za moja kwa moja huku Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa pamoja zikitarajiwa kujenga meli nane mpya, ambapo TRC itajenga meli nne na TPA meli nne katika Ziwa Tanganyika ifikapo  mwishoni mwa mwaka  2028.

Previous Post

DAKTARI AANIKA UNDANI UPANDIKIZAJI WA UUME

Next Post

YANGA, SIMBA MSHIKE MSHIKE

Next Post
YANGA, SIMBA MSHIKE MSHIKE

YANGA, SIMBA MSHIKE MSHIKE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

NITAONGOZA KWA KUZINGATIA USHIRIKIANO – SIMBACHAWENE

8 months ago
GONCALVES: MECHI NA AS FAR RABAT NI FAINALI

GONCALVES: MECHI NA AS FAR RABAT NI FAINALI

6 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?