• ePaper
Monday, June 1, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASIRA AELEKEZA MAMBO MATATU YA USHINDI CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 10, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WASIRA  AELEKEZA MAMBO MATATU YA USHINDI CCM
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na LATIFA GANZEL,

Morogoro 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, ameelekeza mambo matatu kwa viongozi wa Chama, kufanikisha ushindi wa kishindo kwa Mgombea Urais, Dk. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na udiwani.

Ameyataja mambo hayo ni kuvunja makundi, kueleza mambo mazuri na makubwa yaliyofanyika katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka minne.

Pia, kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na kuwashawishi kuwapigia kura wagombea waliosimamishwa na CCM.

Wasira, alieleza hayo mjini Morogoro, alipozungumza na viongozi wa CCM wakiwemo mabalozi na wenyeviti wa mashina katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Kwa hiyo ndugu zangu, baada ya kuwaeleza hayo, nataka niwakumbushe kuvunja makundi na kutangaza kazi zilizofanywa katika miaka minne ya kazi ya mgombea urais wetu, Dk. Samia Suluhu Hassan. 

“Ili watu wakapige kura, lazima sisi viongozi tuwahamasishe kwenda kupiga kura, maana kuna wengine wakiwemo wanachama wetu, wanasema si amepita Aboud,  situmemaliza? Anafikiri kura ya maoni inaweka mbunge.

“Kura ya maoni haijaweka mbunge, ndiyo maana Aboud tunamwita mbunge mteule, tena wa ndani ya CCM kwa sababu wa nje watakuja kuipinga CCM,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Sasa sisi kazi zetu ni kuhakikisha watu wanajitokeza na tunawashawishi kwa nini waipigie kura CCM, kazi nyingine ni kuwaambia watoke waende wakapige kura.”

Wasira alisema wajumbe wa mashina, ndiyo wenye Chama chao, kwa kuwa, Chama inaanzia chini na kwamba, mabalozi wote mwaka huu wamepewa usafiri.

“Kile ni kitendea kazi cha kutoka nyumba hadi nyumba, kuwaambia wananchi leo ni siku ya kupiga kura, tokeni nyote mkapige kura.

“Katika mfumo wetu, zamani ukikosa mpinzani unapita bila kupingwa, ila sasa kwa mfano, tuna mgombea wetu na wapinzani hawakujitokeza.

“Kule kunataka nguvu zaidi kwa sababu, watu watafikiri tayari, kumbe yule mgombea ili ashinde, lazima kura za ndiYo ziwe nyingi kuliko hapana, vilevile mgombea wa urais, anahitaji kura nyingi kila mahali, sasa atazipata wapi kama watu hawajitokezi kupiga kura?.

“Ndiyo maana, pamoja na kuona mkutano mkubwa wa ajabu wa mgombea urais mkoani Morogoro, mimi nimekuja kuwaambia haya, asanteni kwa mkutano mkubwa, waambieni watu wajitokeze kwenda kupiga kura.

“Wahimizeni wote, hata ambao hawataki kutupigia watoke wakapige kura, kimahesabu tutawazidi tu na wenyewe wanajua hilo,”alisema.

Alisema ushindi kwa CCM ni uhakika kutokana na wingi wa wanachama na wafuasi wake.

“Kwa mfano, Morogoro tuna wanachama 100,000, wapigakura wapo 200,000 hapo tayari tupo asilimia 50 ya wapigakura, maana hivi vyama vingine vinavyogombea, havina hata wanachama.

“Wito wangu kwa viongozi wa CCM hususan wenyeviti wa mashina na ninyi wenyeviti wa kata na jumuiya zote, kuwaambia wananchi kwanza, watupigie kura na sababu mnazo,  pili wajitokeze wakapige kura,” alisema.

Previous Post

BALOZI DK.  NCHIMBI ATAJA MISINGI YA CCM

Next Post

1,172,279 KUFANYA MTIHANI WA LA SABA

Next Post
1,172,279 KUFANYA MTIHANI WA LA SABA

1,172,279 KUFANYA MTIHANI WA LA SABA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

MIGOGORO ARDHI MFUPA MGUMU

3 months ago
DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

DANGOTE AIPONGEZA SERIKALI, AANGAZIA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

2 weeks ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?