• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

PANTEV ATAJA SABABU KUPOTEZA CAFCL

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 2, 2025
in Burudani, Michezo
0
PANTEV ATAJA SABABU KUPOTEZA CAFCL

MENEJA Mkuu wa Simba, Dimitar Pantev

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

BAADA ya kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Stade Malien, Meneja Mkuu wa Simba, Dimitar Pantev amesema sababu kubwa ya kushindwa kupata matokeo ni wachezaji wake kucheza chini ya kiwango.

Simba, juzi ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Stade Malien, katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), uliofanyika Uwanja wa 26 du Mars, Bamako nchini Mali.

Huo unakuwa mchezo wa pili kwa Simba kupoteza kufuatia kukubali kufungwa bao 1-0 dhidi ya Petro Atletico ya Angola, mechi ya kwanza iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kufuatia matokeo hayo, katika msimamo wa kundi D, Simba inaburuza mkia baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzao, Petro Atletico ipo kileleni kwa pointi nne sawa na Stade Malien zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku Esparace ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi mbili.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika juzi, Meneja Pantev alisema walishindwa kupata matokeo ugenini kutokana na wachezaji wake kucheza chini ya kiwango.

Pia walifanya mazoezi bila ya wachezaji waliotitwa katika timu ya Taifa Stars kitu ambacho kilisababisha kushindwa kupata ushindi.

Alisema japokuwa walicheza chini ya kiwango, wachezaji wake walijitahisi kupambana kupata ushindi lakini bahati haikuwa upande wao.

Alisisitiza kuwa hataki kujitetea, hivyo anakubali mashabiki kuchukia kwa sababu wana matarajio makubwa kwa muda mfupi.

Alisema ameshayaona baadhi ya makosa ambayo waliyafanya na kwamba anakwenda kuyatafutia ufumbuzi ikiwemo uboreshaji wa kikosi ili kuja kivingine na kuwapa raha mashabiki.

“Tulicheza chini ya kiwango katika mechi yetu ya ugenini awali tulifanya mazoezi bila ya wachezaji wa Taifa Stars kitu ambacho kilitugharimu.

“Nimeyaona baadhi ya makosa ambayo tuliyafanya ugenini, nitakwnda kuyafanyia kazi ikiwemo uboreshaji wa kikosi ili kuja kivingine na kuwapa raha mashabiki wetu,” alisema Pantev.

Aliongeza kwa kipindi cha miezi miwili aliyokaa klabuni hapo haitoshi kutimiza kile alichotakiwa kukifanya, lakini ni ukweli kwamba kwa timu kubwa kama hakuna muda wa kushuburi.

Alisema amekasirika kushindwa kuwafunga Stade Malien kwa sababu timu yake ni bora kuliko wapinzani wao.

Pantev alisema Simba ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini wachezaji wake walishindwa kuzitumia kupachika mabao wavuni.

Naye kiungo mshambuliaji wa Simba, Neo Maema alikiri kuumizwa na matokeo hayo kwani kama wachezaji walijiangusha wenyewe pamoja na mashabiki kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa.

Maema alisisitiza kuwa matokeo ya kupoteza mechi mbili mfululizo kwa timu kubwa kama Simba yanaumiza, lakini hawana cha kujitetea zaidi ya kurudi upya na kuanza kukusanya pointi katika mechi zilizobakia.

“Matokeo yanaumiza kwa kiasi kikubwa japokuwa tunaendelea kupewa sapoti na mashabiki wetu, hatuna cha kujitetea zaidi tunatakiwa kujipanga upya ili kuanza kukusanya pointi katika mechi zilizobakia,” alisema.

Previous Post

RAIS DK. MWINYI ANADI FURSA Z’BAR

Next Post

VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI

Next Post
VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI

VIONGOZI SIMBASC WATAKIWA KUJITATHMINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

4 months ago
MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI

MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?