• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 4, 2025
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AKOSHA VIONGOZI WA KISIASA, DINI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU

VIONGOZI wa kisiasa, dini na wasomi mbalimbali, wameunga mkono hotuba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa juzi katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam na kusisitiza Tanzania ni taifa huru, halipaswi kuingiliwa.

Wamesisitiza kuwa amani ya nchi, ndiyo msingi wa maendeleo yaliyopo, hivyo serikali ina wajibu wa kuendelea kulinda utulivu uliopo nchini kwa gharama yoyote.

Akizungumza na UHURU, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salim, alimpongeza Rais Dk. Samia, akieleza hotuba yake ilijaa weledi, mwongozo, dira na ustawi mzuri kwa taifa.

Alieleza kuwa Watanzania wanapaswa kuendelea kukemea vitendo vyenye kuhatarisha umoja na mshikamano nchini kwa kuwa siyo suluhisho la kutatua changamoto.

MHADHIRI MWANDAMIZI

Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Uchumi na Uongozi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dk. Phillip Daninga alisema hotuba iliyotolewa na Rais Dk. Samia, imejitosheleza kutolewa na kiongozi wa nchi.

“Rais Dk. Samia ameonyesha msimamo wa Taifa kwa kueleza ni kwa namna gani Watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa nchi yao. Ilikuwa ni lazima azungumze kwa sababu ya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yakiendelea nchini hasa baada ya uchaguzi mkuu.

Aliongeza: “Kutokana na mambo ambayo yalikuwa yanaendelea, hakuna kiongozi anaweza kukaa kimya ndiyo maana amezungumza kwa uchungu na ukali.”

Alisema hotuba hiyo ilionyesha ni kwa kiasi gani viongozi wa dini wanaweza kusimama katika jamii huku wakizingatia mipaka yao.

Dk. Daninga alisisitiza makundi yote kutafakari kwa kina hotuba hiyo, kwani inajitosheleza na inatoa mwanga wa namna gani Taifa linatakiwa kuendelea.

Mratibu wa Taasisi ya Taifa letu Kesho yetu, Charlisious Charles, alisema hotuba ya Rais Dk. Samia imekuwa ni mwanga kwa taifa kwa sababu imetoa msimamo kwa nchi kutotetereka.

“Hatuna Tanzania nyingine tofauti iliyopo, hivyo lazima tuungane tuwe wamoja kuilinda ili vizazi vijavyo vinufaike na matunda yaliyopo, hatupaswi kuruhusu makundi yoyote kuchafua taswira ya nchi iwe ni ndani au nje,” alisema.

Alitoa wito kwa vijana kutambua kuwa wanapoiharibu nchi yao wanajiharibia wenyewe kwa kuwa madhara ni makubwa.

MZEE KIMITI

Mwanasiasa mkongwe, Mzee Paul Kimiti, alisema hotuba ya Rais Dk. Samia, imebeba mambo mengi, wananchi wanatakiwa kukaa chini na kuichambua kwa kina kwa kuwa kagusa kila eneo.

Alisema suala la kulinda amani ya nchi ni jukumu la kila Mtanzania ambaye ni mzalendo, mwananchi hapaswi kusubiri polisi aje kuzuia fujo, yeye ndiyo anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kutengeneza amani ya nchi yake.

“Kimsingi hata sisi wazazi na walezi tunatakiwa kuwakanya vijana wetu, ulinzi na usalama unaanzia majumbani kwetu, tukiwaachia tunakuja kulaumu baadaye.

“Tunatakiwa kuwashauri vijana, ulinzi uanzie nyumbani kila mmoja ni jukumu lake kulinda amani na utulivu wa nchi yetu, hatuna sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya hapa,” alisisitiza mwanasiasa huyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa hotuba yake, ambayo imetoa msimamo na mwelekeo wa taifa.

“Nampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mwelekeo na rai kupitia wazee kuhusu mustakabali mzima wa nchi yetu, hasa utulivu na amani.

“Kubwa zaidi ni msimamo kuwa hatutayumba, tumejipanga kuhakikisha Tanzania inabaki moja,” alisisitiza.

Maganya alitoa wito kwa wazazi, kuwasihi vijana kuacha kufuata mkumbo, badala yake wawe mstari wa mbele kulinda nchi.

KATIBU MWENEZI SONGWE

Katibu wa Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe, Malimu Yusuph Rajab, alisema hotuba ya Rais Dk. Samia inaonesha msisitizo katika uongozi wake imara, ukweli, uwajibikaji huku akilenga kuwaeleza Watanzania hali halisi ya siasa za ndani ya nchi.

Alisema hotuba hiyo pia imeeleza namna ambavyo baadhi ya mataifa makubwa yanavyojaribu kuwatumia baadhi ya Watanzania waliokosa uzalendo kuharibu misingi ya amani, utulivu, umoja na mshikamano.

“Bila shaka kila Mtanzania mwenye akili timamu anajua kuwa yale hayakuwa maandamano bali zilikuwa ni vurugu zilizoambatana na uhalifu uliopangwa na kuratibiwa kutoka kwa watu maalumu wenye ajenda iliyojificha.

“Siasa siyo vurugu kwani siasa bora ni ile yenye kusaidia kutatua migogoro katika jamii na siyo kuzalisha migogoro, hivyo kuna kila sababu Watanzania wakajiepusha na wanasiasa wenye kuzua mitafaruku balada ya kujenga umoja,” alieleza.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Bhoke Ishengoma, alisema Rais Dk. Samia katika hotuba yake alisisitiza vijana kuwa wazalendo na kuepuka kutumika.

“Rais alisema wapo vijana ambao walifanya vitendo vya vurugu na kukubali kutumika kwa kukosa uzalendo, hivyo ni muhimu vijana tukaipenda nchi yetu na kuhakikisha tunailinda amani kwa nguvu zote.

“Amani ikiondoka hata sisi hatutasoma vizuri, hivyo tutashindwa kutimiza ndoto zetu ambazo tumezipigania kwa muda mrefu,” alieleza.

Kwa upande wake, Mdau wa Maendeleo na Mwanasiasa, Abdul Kambaya, alisema anaamini hakuna vijana wa Kitanzania ambao wamepanga kuandamana Desemba 9, mwaka huu wengi wao hawahitaji maandamano.

“Kauli ya Rais Samia ilinyooka haikusema kama kuna vijana Tanzania wanapanga kuandamana, anayehamasisha yupo nje ya Tanzania na tunaamini hakuna kijana wetu ambaye amepanga kuandamana.

Dereva bodaboda anayefanya shughuli zake UDOM, Meshack Ndimbwa, alisema amefurahishwa na kauli ya Rais Dk. Samia kwamba serikali imejipanga kuhakikisha maandamano hayatokei tena.

Alisema suala la maandamano siyo utamaduni wa Mtanzania kwa sababu athari zake ni kubwa kijamii, kiuchumi na kisiasa.

“Kuanzia siku ile ya Oktoba 29 maisha yetu hasa sisi vijana ambao lazima tutoke ndipo tupate rikizi yalikuwa magumu. Tunaomba serikali iimarishe ulinzi zaidi ili wale wenye nia ovu kutaka kuharibu amani yetu wadhibitiwe mapema,” alisema.

MWENYEKITI SOKO LA MAGOMENI

Mwenyekiti wa Soko la Magomeni, Daudi Dolle, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa kuhimiza amani jambo ambalo ni muhimu kwa nchi.

Alisema bila ya amani hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika, hivyo aliwasihi wajasiriamali wenzake kudumisha amani muda wote.

“Niwaombe sana wananchi tusikubali amani ya nchi ipotee na tusijihusishe na vikundi vyovyote vya watu wanaotaka kuhatarisha amani ya nchi,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wafanyabiashara wenye Ulemavu Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWADA), Jerome Chitumbi, aliwahimiza wananchi kutokubali kushawishiwa na mtu yoyote anayehatarisha amani ya nchi.

Alisema wafanyabiashara wengi wanapenda kufanya biashara zao kwa amani bila ya hofu yoyote, hivyo ni vyema jamii kuwa mstari wa mbele kulinda amani nchini.

“Tunakumbuka waasisi wetu wa taifa Hayati Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walivyopambana kuhakikisha nchi inakuwa na amani, niwaombe wananchi wenzangu kuenzi yale yote tuliyoachiwa na waasisi wetu,” alisema.

Previous Post

KUELEKEA DESEMBA 09, POLISI WABAINI MBINU OVU 12

Next Post

FOUNTAIN GATE KUITIBULIA YANGA?

Next Post
FOUNTAIN GATE KUITIBULIA YANGA?

FOUNTAIN GATE KUITIBULIA YANGA?

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MGODI WA KIHISTORIA WA NIOBIUM KUJENGWA MKOANI MBEYA

MGODI WA KIHISTORIA WA NIOBIUM KUJENGWA MKOANI MBEYA

3 weeks ago
TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?