• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 13, 2025
in Burudani, Michezo
0
‘MSAUZI’, MHISPANIA WACHUANA UKOCHA SIMBA
0
SHARES
20
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

BAADA ya kikao kizito cha viongozi wa klabu ya Simba, muda wowote kuanzia sasa wanatarajia kutangaza jina la kocha mpya ambaye atachukua mikoba ya kocha Dimatar Pantev.

Miongoni mwa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kupewa nafasi hiyo ni ni raia wa Afrika Kusini, Steve Becker ambaye ni Kocha wa Stellenbosch na raia wa Hispania, Antonio Casano anayekinoa kikosi cha Atletico Luanda ya Angola hivi sasa.  

Viongozi wa Simba juzi walikaa kikao kizito jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kujadili mchakato wa kocha wa kumrithi Pantev ambaye alidumu ndani ya klabu kwa siku 61 na kuiacha chini ya msaidizi wake Suleiman Matola.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi ambaye alikuwa katika kikao hicho, alisema jambo kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kocha mpya anatambulishwa haraka ili kuanza kazi mara moja.

“Viongozi ilibidi wafanye kikao cha haraka, lengo kubwa ni kujadili mchakato wa kocha wa kumrithi Pantev sambamba na kuunda benchi zima la ufundi ambalo kwa hivi sasa lipo chini ya Matola,”alisema.

Kiongozi huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema mbali na jambo hilo, pia viongozi hao wanahitaji kuimarisha kikosi chao ili kifanye vizuri kama ilivyokuwa awali.

“Baada ya kukaa katika kikao hicho tumeona ni bora kumleta kocha haraka ambaye atakuja kuungana na Matola.

“Lengo letu likiwa kuirejesha timu katika hali yake ya mwanzoni ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Tanzania B ara na Klabu Bingwa Afrika,” alisema kiongozi huyo.

Alisema kuwa Bodi ya Wakurugenzi imeutaka uongozi wa Simba kuharakisha mchakato wa kocha mpya, ili awahi kuanza maandalizi ya timu kabla ya mechi za mashindano kuendelea mapema mwakani.

SUALA LA USAJILI

Wakati huo huo kikao hicho kilikubaliana kuwa kazi ya usajili isubiri ujio wa kocha mpya kuangalia ubora wa wachezaji kisha atashauri  nini kifanyike.

“Tunajua usajili wa dirisha dogo unakaribia lakini hilo litamsubiria kocha mpya kujua nani atatolewa kwa mkopo na nani ataingia ni hadi pale tutakapomtangaza ndiyo kila kitu kitajulikana nay eye ndiye atakayeshauri nini kifanyike,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kuna majina ya wachezaji ambayo aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pantev aliyaacha ili kusajiliwa na wengine kuondolewa kwa lengo la kuimarisha kikosi.

Ligi Kuu Tanzania Bara kwa hivi sasa imesimama hadi mwezi Januari, mwakani  kupisha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinazotarajiwa kuanza Desemba 21 hadi Januari 18, mwakani.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika nchini Morocco na Taifa Stars itashiriki.

Simba ilikosa maelewano kufuatia kupoteza mechi mbili mfululizo za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Petro Atletico ya Angola na Stade Malien ya Mali na kusabisha kuachana na Pantev kabla ya kupoteza mabao 2-0 mbele ya Azam ikiwa chini ya Matola.

Simba yenye maskani yake katika Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam katika msimamo wa kundi C la michuano ya CAFCL inaburuza mkia kwa kupoteza mechi mbili.

Katika msimamo huo, timu za  Petro Atletico na Stade Malien zina pointi nne kila moja zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa huku Esperance ya Tunisia ikishikilia nafasi ya tatu kwa pointi mbili.

Previous Post

WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA MALI ZA SH. BILIONI 1.5

Next Post

TFF. BMT WANOGESHA SAFARI MASHABIKI AFCON

Next Post
TFF. BMT WANOGESHA SAFARI MASHABIKI AFCON

TFF. BMT WANOGESHA SAFARI MASHABIKI AFCON

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

ALAMA TATU KUMUENZI JPM

2 months ago
MAKUBWA YAFICHULIWA

MAKUBWA YAFICHULIWA

3 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?