LONDON, England
FAINALI za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025, msimu huu zinatarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Michuano hiyo mikubwa zaidi Afrika itafanyika kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026 katika viwanja mbalimbali nchini humo.
Tayari timu 24 zimeshafuzu michuano hiyo kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika na ratiba ilishapangwa.
Kwa mujibu wa ratiba, mchezo wa ufunguzi utapigwa Desemba 21, mwaka huu ukizikutanisha timu za Morocco na Comoros katika kundi A.
Mechi za hatua ya makundi zitaanza Desemba 21 hadi Desemba 31, mwaka huu, zikifuatiwa na hatua ya 16 bora kuanzia Januari 3, hadi 10, mwakani, nusu fainali zitachezwa Januari 14, mwakani huku mshindi wa tatu ikiwa Januari 17, mwakani na fainali itapigwa Januari 18, mwakani.
Timu zilizofuzu kushiriki fainali hizo kwa mwaka huu kundi A ni Morocco, Comoros, Mali na Zambia.
Katika kundi B zipo timu za Angola, Misri, Afrika Kusini na Zimbabwe, kundi C ni Nigeria, Tanzania, Tunisia na Uganda.
Kwa upande wa kundi D zimepangwa timu za Benin, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Senegal, kundi E ni Algeria, Burkina Faso Guinea ya Ikweta na Sudan wakati kundi F likiwa na timu za Cameroon, Gabon, Ivory Coast na Msumbiji.
Katika michuano ya AFCON 2025, mashabiki wanatarajia kuona vipaji vya hali juu kutoka kwa wachezaji wa timu mbalimbali zilizofuzu kushiriki fainali hizo msimu huu.
Vilevile soko la wachezaji linaweza kupanda zaidi kwa kuonyesha kiwango bora katika fainali hizo na kusajiliwa kutoka katika klabu zao wanazozitumikia hivi sasa na kwenda sehemu nyingine kwa dau kubwa.
Fainali hizo zimekuwa zikifuatiliwa na wadau mbalimbali wa soka Duniani wakiwemo mawakala ambapo baadhi ya wachezaji walishapata ulaji wa kwenda kucheza soka la kulipwa maeneo tofauti kupitia michuano ya AFCON.
ZAWADI HIZI HAPA
Katika fainali za AFCON msimu huu, bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kupatiwa kombe na kiasi cha dola milioni saba (zaidi ya sh. bilioni 17,290,000,000 za Kitanzania), mshindi wa pili dola milioni nne (zaidi ya sh. bilioni 9,880,000,000 za Kitanzania) huku timu zitakazoingia hatua ya nusu fainali zikiondoka na dola milioni 2.5 kila mmoja (zaidi ya sh. bilioni 6,175,000,000 za Kitanzania).
Katika michuano ya msimu huu ya AFCON 2025, baadhi ya wachezaji Waafrika wanaocheza Ligi Kuu ya England wataziwakilisha timu zao za taifa.
Katika makala hii, tunakuletea orodha ya wachezaji wanaocheza Ligi Kuu ya England ambao wataziwakilisha nchi zao katika michuano hiyo msimu huu.
wachezaji hao watazikosa baadhi ya mechi za michuano inayoendelea England ikiwemo Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Carabao na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal, Leeds United na Chelsea hazitakuwa na wawakilishi katika fainali za michuano ya AFCON 2025.
Aston Villa: Evann Guessand (Ivory Coast)
Bournemouth: Amine Adli (Morocco)
Brentford: Dango Ouattara (Burkina Faso), Frank Onyeka (Nigeria)
Brighton: Carlos Baleba (Cameroon)
Burnley: Lyle Foster (Afrika Kusini), Axel Tuanzebe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Hannibal Mejbri (Tunisia)
Crystal Palace: Ismaila Sarr (Senegal), Christantus Uche (Nigeria), Chadi Riad (Morocco), Cheick Doucoure (Mali)
Everton: Iliman Ndiaye (Senegal), Idrissa Gueye (Senegal)
Fulham: Alex Iwobi (Nigeria), Calvin Bassey (Nigeria), Samuel Chukwueze (Nigeria)
Liverpool: Mohamed Salah (Misri)
Manchester United: Bryan Mbeumo (Cameroon), Amad Diallo (Ivory Coast), Noussair Mazraoui (Morocco)
Manchester City: Omar Marmoush (Misri), Rayan Ait-Nouri (Algeria)
Newcastle United: Yoane Wissa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Nottingham Forest: Ola Aina (Nigeria), Wily Boly (Ivory Coast), Ibrahim Sangare (Ivory Coast)
Sunderland: Noah Sadiki (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC), Simon Adingra (Ivory Coast), Chemsdini Talbi (Morocco), Reinildo (Msumbiji), Ahmed Abdullahi (Nigeria), Habib Diarra (Senegal), Arthur Masuaku (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Blondy Noukeu (Cameroon), Bertrand Traore (Burkina Faso)
Tottenham: Pape Matar Sarr (Senegal), Yves Bissouma (Mali)
West Ham: El Hadji Malick Diouf (Senegal), Aaron Wan-Bissaka (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Wolves: Emmanuel Agbadou (Ivory Coast), Jackson Tchatchoua (Cameroon), Tawanda Chirewa (Zimbabwe), Marshall Munetsi (Zimbabwe) na Tolu Arokodare (Nigeria).




