• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

LEBRON JAMES NA MABADILIKO MAPYA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 14, 2025
in Burudani, MAKALA BURUDANI, Michezo
0
LEBRON JAMES NA MABADILIKO MAPYA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NEW YORK, Marekani

MCHEZAJI mahiri wa mpira wa kikapu, LeBron James yupo mbioni kuingia mabadiliko mapya katika mchezo huo.

Nyota huyo siri  yake imevuja ambapo Wakala wa LeBron James amedokeza uwezekano wa kuhama Lakers huku New York Knicks ikionekana kumwania.

KAULI YA TAJIRI

Tajiri Paul hivi karibuni ametoa maoni yake juu ya mshambuliaji huyo kuhama Los Angeles Lakers na kutua New York Knicks.

“Kuna kitu hicho, lakini ni mapema mno kusema zaidi juu ya jambo hilo,” alisema Paul.

LeBron James amehusishwa na uwezekano wa kufanya biashara na New York Knicks, licha ya kucheza mechi saba pekee msimu huu ndani ya timu yake ya sasa.

ALAMA ALIYOWEKA

LeBron James kwa asilimia kubwa tayari ameacha alama isiyoweza kusahaulika kwa  mashabiki wa Los Angeles Lakers.

Kwani kikosi hicho, kimefanikiwa kuweka rekodi ya 17-6 na kushika nafasi ya pili katika Mkutano wa Magharibi wa NBA.

MASWALI

Hata hivyo, maswali kuhusu uwezekano wa kutwaa ubingwa wa timu hiyo yameibuka.

Kulingana na tathmini ya uangalifu ya wakala wa James, Rich Paul ambaye amezungumzia hadharani tetesi za kuhamia New York Knicks alisema kuna uwezekano timu hiyo ikakosa ubingwa.

Lakini bado mashabiki wa timu hiyo, wana imani kwamba itafanya vizuri na kutwaa ubingwa NBA.

UTANI

LeBron hivi karibuni alimtania shabiki wa timu yake mbele ya umati kuwa bado hana furaha.

Katika kipindi cha hivi majuzi cha Game Over na Max Kellerman, Rich Paul aliweka msimamo wake wazi kuhusu nafasi ya Lakers kufanya vizuri.

"Sidhani wanatosha kufika fainali, lakini ubingwa kazi ipo, sidhani kama wana kikosi cha kushindana, kwa mtazamo wangu,”alisema Paul.

Licha ya utendaji mzuri wa Lakers, wakiwa na rekodi ya 6-1 katika michezo iliyomshirikisha James na rekodi ya 11-5 bila yeye, Paul alisema ana mashaka kuhusu uwezo wao wa kushindana.

MSISITIZO WA PAUL

Tajiri huyo alisisitiza kwamba James amejitolea kumaliza msimu wa 2025-26 akiwa na Lakers.

Lakini Paul, aliacha mlango wazi kwa uvumi wa nyota huyo kuhama.
UGUMU UPO HAPA

Lakers hivi sasa wanakabiliwa na njia ngumu ya kutwaa ubingwa wa kikapu.
Hata kwa uwepo wa James ,Luka Doncic na Austin Reaves bado kunaonekana timu hiyo ina shida.
UWAZI HUU HAPA
Tajiri Paul aliweka wazi kwamba LeBron anaweza kubaki ndani ya timu hiyo lakini kwa tathmini yake ya umakini.

Paul alithibitisha uaminifu wa wa mchezaji huyo wa Lakers kuwa muda uliosalia wa msimu huu ni mdogo.

"Ataondoka lakini swali la msingi anaenda wapi?, LeBron anafanya kazi nzuri ndani ya  Knicks kuwa bora zaidi,” alisema Paul.

UANGALIZI
Pasul alieleza kwamba uchezaji wa LeBron na uwezo wa Lakers umekuwa ni kitu kimoja cha  k ukuzau wezo wa mchezaji huyo.

“Lakini zaidi ya hayo, mlango ni wazi kwa biashara inayowezekana kufanyika ya kumuuza,”alidokeza Paul.

MJADALA WAZUKA

Baada ya kauli ya Paul, mjadala umezuka kuhusu uwezekano wa kufanyika biashara ya kuuzwa kwa mchezaji huyo kutoka Knicks.

Baadhi ya mashabiki na wachambuzi wameanza kujadili nini kitatokea kama mchezaji huyo ataondoka.

Mashabiki hao, wanaonekana kuhoji James ataiongoza Lakers katika kipindi kilichosalia cha msimu na matarajio mapya ya ubingwa.

Hali ya kutoridhishwa kwa Paul kunaonesha kwamba hata wasomi kama James wanahojia juu ya kuwepo jambo hilo.

KAULI YA  LeBRON JAMES
LeBron James hivi karibuni alikataa kuzungumzia mipango yake ya siku zijazo.
“ Kwa sasa nipo Lakers, inaweza kuwa wakati mechi za mchujo zitakapowasili mwezi Aprili, mwakani  nikawa bado ninacheza hapa,”alisema nyota huyo.
 Mshambuliaji huyo alikiri kwamba mawazo yake yapo katika mechi za mchezo wa robo fainali ya Kombe la NBA.
“Nafahamu tumepoteza mechi, Lakers tulifungwa na San Antonio Spurs kwa vikapu 132-119, kwa maana hiyo nina mambo mengi ya kufikiri, juu ya jambo hili,” alisema.
Alifafanua kuwa miaka miwili iliyopita, Lakers walipokwenda Las Vegas na kutwaa ubingwa wa kwanza wa Kombe la NBA, aliwahi kutahadharisha kwamba walikuwa na safari ndefu ya mafanikio.
“Lakini hii ilikuwa baada ya kuangalia baadhi ya mambo, nikasema hivyo, haikuwa njia ya kuashiria kitu kibaya,”alisema mchezaji huyo wa kikapu.
MAISHA YAKE

LeBron Raymone James Sr. ni mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu wa Los Angeles Lakers.
Mchezaji huyo alizaliwa  Desemba 30, mwaka 1984 na hivi sasa ana umri wa miaka 40.

Alizaliwa sehemu inayoitwa Akron, Ohio nchini Marekani na hivi sasa anaichezea timu ya Los Angeles Lakers.

Anatumia jezi namba 23 ambapo amekuwa anacheza nafasi ya  mshambulizi katika timu yake.

Alijiunga mwaka 2018 na Los Angeles Lakers kwa uhamisho wa thamani ya dola bilioni 1.3 za Marekani.

Jarida la Forbes liliwahi kutoa taarifa kwamba mchezaji huyo ana mchumba wake, Savannah James.

Wapenzi hao, wamejaliwa kupata watoto wawili ambao ni Bronny James na Bryce James.

Lakini mshambuliaji huyo ana marafiki zake wa karibu ambao ni Stephen Curry, Kobe Bryant na Kevin Durant.
Previous Post

WACHEZAJI LIGI KUU YA ENGLAND WATAKAOTIMKIA AFCON MOROCCO

Next Post

RAIS DK. SAMIA ASIMULIA UIMARA WA JENISTA

Next Post
RAIS DK. SAMIA ASIMULIA UIMARA WA JENISTA

RAIS DK. SAMIA ASIMULIA UIMARA WA JENISTA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

DK. NCHIMBI ATANGAZA NEEMA YA MAJI UBUNGO

7 months ago
NCHIMBI : NIDHAMU NGUZO KUIMARISHA DEMOKRASIA

NCHIMBI : NIDHAMU NGUZO KUIMARISHA DEMOKRASIA

7 months ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?