• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

BONDIA MWAKYEMBE AMKUBALI MMALAWI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 16, 2025
in Burudani, Michezo
0
BONDIA MWAKYEMBE AMKUBALI MMALAWI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

PAMOJA na kushinda kwa TKO bondia wa ngumi za kulipwa, Mtanzania Emmanuel Mwakyembe, amempongeza mpinzani wake Tionge Chingeni kutoka Malawi kwa kuonyesha ushindani mkubwa katika pambano hilo.

Mwakyembe alimchapa Chingeni kwa TKO raundi ya tano, mwishoni mwa wiki katika pambano la ‘Punch to Punch’,  lisilo la ubingwa uzito wa kati lililofanyika Ukumbi wa The Sea View Dome Banguel uliopo Kawe, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam, bondia huyo alisema mpinzani wake alionyesha ushindani mkubwa hatua ambayo ilifanya pambano hilo kuwa zuri.

Mwakyembe alisema ubora wa mpinzani wake ulimfanya kutumia muda mwingi kufikiria mbinu za kumchapa hadi alipofanikiwa katika raundi ya tano.

Pia, bondia huyo aliwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono katika pambano hilo.

“Haikuwa rahisi lakini nguvu ya Watanzania imeonekana maana wao wamenipa hamasa ya kupambana hadi nikapata ushindi kwa sababu mpinzani wangu alikuwa na nguvu na mgumu kupigika kwa urahisi.

“Ninashukuru Mungu nimetimiza ahadi ya kuwapa zawadi ya furaha Watanzania kwa kupata ushindi wa kishindo, hii inaniongezea kuaminika kwa kwa mashabiki zangu,” alisema.

Promota wa pambano hilo, Latifa Jabiri alisema mwisho wa mtanange huo ndiyo mwanzo wa pambano lingine, hivyo wadau wa masumbwi wategemee mambo mazuri kutoka kwa kampuni yake ya Three Sports Promotion.

Previous Post

TPLB YAGUSIA WAZO LA FIFA USAWA WA KALENDA

Next Post

TRA UNITED KAZI KAZI

Next Post
TRA UNITED KAZI KAZI

TRA UNITED KAZI KAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

2 weeks ago
HAPATOSHI ‘KNOCKOUT YA MAMA’ KIJITONYAMA

HAPATOSHI ‘KNOCKOUT YA MAMA’ KIJITONYAMA

4 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?