• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 23, 2025
in Burudani, Michezo
0
NI MWANZO WA SIMULIZI MPYA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

ILE ndoto ya Watanzania kuishuhudia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikipata ushindi wake wa kwanza katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inaanzia leo wakati miamba hiyo itakapocheza mchezo wake wa kwanza wa kundi C dhidi ya Nigeria.

Taifa Stars itachuana na Nigeria saa 2:30 usiku katika mchezo wa kundi hilo utakaopigwa katika Uwanja wa Fez uliopo jijini Fes, Morocco.

Katika michuano hiyo ya nne kwa Tanzania kushiriki, miamba hiyo haijawahi kushinda hata mechi moja kati ya mechi tisa ilizocheza katika AFCON, ikitoka sare mara tatu na kufungwa mara sita.

Leo Tanzania itahitaji kuvunja mwiko huo kwa kupata ushindi wake wa kwanza katika AFCON dhidi ya Nigeria ambayo mara ya mwisho kukutana nayo katika michuano hiyo ilikuwa miaka 45 iliyopita katika fainali za mwaka 1980 ambapo Stars ilikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Super Eagles.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kuanza vizuri katika fainali hizo.

“Wachezaji wako vizuri kipindi tulipokuwa mazoezi tumerekebisha makosa tunatambua Nigeria ni timu nzuri lakini tumejipanga kukabiliana nayo.

“Tunakwenda katika mchezo huu kwa nidhamu kubwa na kuwaheshimu Nigeria kwa sababu ni wazoefu katika mashindano haya,” alisema Gamondi.

Kocha huyo aliongezea kuwa, wachezaji wana morali ya hali juu na wanatambua kipi cha kufanya kupata matokeo mazuri katika mtanange huo.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, alisema wachezaji wako tayari kwa mchezo huo kwani wana nguvu za kutosha kupambania matokeo mazuri.

“Wachezaji wamekaa kambini nchini Misri siku 10 na kukaa hapa Morocco takribani siku tatu kwa muda huo siwezi kusema hawajajiandaa, timu imejiandaa vizuri, wachezaji wako tayari kwa mchezo,” alisema.

Katika kundi C linaloundwa na timu za Tanzania, Nigeria, Uganda na Tunisia, kikosi cha Gamondi ndicho pekee ambacho hakijawahi kuvuna pointi tatu wala kutinga hatua ya mtoano, ambapo mara zote tatu zilizopita iliishia makundi huku wapinzani wake wakipata mafanikio mbalimbali.

Nigeria iliyokata tiketi ya kushiriki mara 21 imetwaa ubingwa mara tatu (1980, 1994 na 2013), Tunisia iliyoshiriki mara 22 imebeba ‘ndoo’ hiyo ya Afrika mwaka 2004 na Uganda iliyoshiriki mara nane ikimaliza nafasi ya pili mwaka 1978.

Wakati rekodi ya Tanzania kutofanya makubwa AFCON ikimweka mtegoni Muargentina Gamondi, makocha wa soka nchini wanaamini kama Taifa Stars itafanya mambo sahihi kwa wakati sahihi basi hakuna kitakachoshindikana.

Kocha wa Mbeya City ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Mecky Mexime alisema kitu kikubwa ambacho Stars inapaswa inapaswa kujiandaa vyema kimbinu kuhakikisha inashinda katika mechi zake.

“Katika mpira lolote linatokea hata kama timu hapo zamani ilikuwa na historia nzuri inaweza kufungwa muhimu ni namna ya kujipanga kuhakikisha unapata ushindi katika kila mchezo,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar, alisema ushirikiano baina ya wachezaji na benchi la ufundi ni miongoni mwa sababu muhimu ambayo inaweza kuongeza makali katika kikosi dhidi ya miamba kama Nigeria na Tunisia.

Aliyekuwa kocha wa Yanga na Ruvu Shooting, Charles Mkwasa, alisema usikivu wa wachezaji juu ya mbinu za benchi la ufundi ni miongoni mwa sababu ya msingi inayoweza kuibeba Stars katika fainali za AFCON mwaka huu.

“Wachezaji wa Stars wafuate yale wanayoambiwa na benchi la ufundi, ninaamini wakishirikiana vyema watafanikiwa,” alisema.

Salvatory Edward ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Pamba Jiji, alisema umakini, kujitoa na usikivu mzuri wa mbinu za benchi la ufundi itakuwa silaha bora kwa Taifa Stars katika fainali hizo.

“Stars inapaswa kuzingatia umakini, kujitoa na kusikiliza maelekezo ya walimu, wakifuata hayo na wakishirikiana vyema basi watapata mafanikio makubwa na kufika mbali katika mashindano ya AFCON,” alisema Edward.

Kocha na mchambuzi wa soka, Kennedy Mwaisabula maarufu Mzazi, alikiri Stars kuwa katika kundi gumu, lakini anaamini kama wachezaji watasikiliza vyema mipango ya makocha basi hakuna kitakachowazuia kufanya vyema.

“Stars ipo katika kundi gumu kwa sababu  timu inazocheza nazo zina viwango vya juu, hivyo umakini unahitajika mfano timu kama Uganda ina wachezaji wengi ambao wanacheza soka la kulipwa Ulaya bado Nigeria na Tunisia,” alisema.

AFCON ZILIZOPITA

Katika fainali zote tatu zilizopita ambazo Stars ilishiriki, timu hiyo haijawahi kutinga hatua ya mtoano hata mara moja.

Katika michuano ya mwaka 1980 iliyofanyika Nigeria, Taifa Stars ilipangwa kundi A na timu za Nigeria, Misri na Ivory Coast.

Taifa Stars iliburuta mkia kwa pointi moja baada ya kutoka sare na Ivory Coast. Awali, ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Nigeria na mabao 2-1 ilipovaana na Misri.

Katika AFCON mwaka 2019 zilizofanyika nchini Misri, Tanzania ilipangwa kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya.

Taifa Stars ilimaliza katika kundi hilo ikiwa nafasi ya nne baada ya kufungwa mechi zote tatu.

Kikosi hicho kilichokuwa kikinolewa na Amunike, kilianza kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Senegal, kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kenya na kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.

Pia, Taifa Stars iliburuta mkia katika hatua ya makundi ya AFCON mwaka 2023 zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Ikiwa imepangwa kundi F, Stars ilivuna pointi mbili (nyingi zaidi ya AFCON ilizoshiriki awali), ikianza kwa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Morocco, sare ya bao 1-1 kutoka kwa Zambia na suluhu dhidi ya DRC.

Previous Post

FAHAMU MADHARA KULALA DAKIKA 30 BAADA YA KULA

Next Post

YAJUE MAENEO MAALUMU YA MASHABIKI AFCON MOROCCO

Next Post
YAJUE MAENEO MAALUMU YA MASHABIKI AFCON MOROCCO

YAJUE MAENEO MAALUMU YA MASHABIKI AFCON MOROCCO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

4 months ago
‘PENALTI’ STARS YAIGAWA DUNIA

‘PENALTI’ STARS YAIGAWA DUNIA

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?